Raisi Wangu 2015

Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,412
4,559
Nguvu aliyo nayo huyu jamaa kwa sasa tutegeme maajabu 2015.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akicheza muziki sambamba na Wanachama wa VICOBA Tanzania wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Biashara ya Miaka Kumi yam Wajasilia Mali wa VICOBA tangu kuanzishwa kwakwe,iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

 
Kuliko kuendelea kuwa chini ya ccm, nitamuomba sheikh farid na ponda waendeleze makongamano nchi isitawalike! Yaani cjui nani alituloga, watu mnajua kabisaaaaa sifa za huyu mwafulani, lakini bado tumo tu! Aiseeee, kazi ipo!
 
mbona watu mnapa promo sana uyu mzee,kwan hakuna watu wengine wanaofaa kuongoza nchi
 
My friend kwa matukio niliyo yaona kwenye chaguzi za ccm. huyu jamaa anaweza chukua nchi so softly.

hana jipya huyo ni bwebwe tu hizo HAMUULIZE SILAHA NA JOHN CHEYO alikosa mpaka kula ya Mkwewe..BARIADI na SILAHA alitangaza INNCHI HATAWALIKI...zisikutishe izo PICTURE hapa ndio TZ RAISI apangwa mitaaani anapgwa ndani ya CHAMA HUSIKA
 
My friend kwa matukio niliyo yaona kwenye chaguzi za ccm. huyu jamaa anaweza chukua nchi so softly.
Kwa mazingira ya Tanzania ya leo sidhani ni rahisi kama unavyofikiria mkuu,watu wako makini kuliko mtu anaweza kuelezea.Mimi sielewi vizuri kama Mh.Lowasa keshapitishwa na Chama chake kupeperusha bendera kwa nafasi ya urais ambayo haijatangazwa popote,naweza kudhani kuwa anayo nia.Sasa kama hivyo ndivyo bado siamini kama mtu akipitishwa na chama chake basi amechukua nchi kiulaini,sitaki kuamini urahisi huo upo Tz na kwa mazingira ya kisiasa kwa sasa.Labda unisaidie chama cha mapinduzi kina wapiga kura waaminifu wangapi?na vyama vingine pia vinawapiga kura waaminifu kwa vyama vyao wangapi then wangapi hawatabiriki inaweza kuwa sehemu nyingine ya kuanzia vinginevyo nadhani safari ni ndefu na ngumu sana.Labda wewe mkuu unatumia vigezo gani vya kumkabidhi Mh.Lowasa Madaraka ya urais sasa?
 
Tatizo kubwa la watanzania ni kuwa hawana imani - FAITH. Ukijua kuwa atakalo Mola mwanadamu haliwezi na akijitahidi atachelewesha tu.

Leo kuna watu wanahoji kwanini JK na ndivyo itakavyokuwa kwa EL.

Acheni kazi za mola ziwe za mola na kazi za wanadamu ziwe za wanadamu. Mola huwapenda wenye dhambi isipokuwa huchukia dhambi(God loves sinners but hate sins) ukizingatia sisi sote tuna dhambi wachache wetu hukumbuka kutubu dhambi zetu na kusamehewa ila wengine hubaki kufikiria dhambi za wengine na kusahau kutubu dhambi zao mwisho wa siku wanabaki kulalamika na kulaumu.
Mungu siku zote huongea na wanadamu kupitia wanadamu-unabii. Na unabii siku zote unatimia kwa sababu ni mdomo wa Mungu ukiongea na wanadamu.
 
picha zinaonyesha michezo ile ile ya kuwadanga watu kwa kuwanunulia sare za kanga na matishirt + kofia, kwa umaskini wa watanzania sishangai kuwaona wanamshangilia jamaa lakini significant meaning ninayo ipata hapo ni kwamba wananchi hawa baada ya kuona wameibiwa vyakutosha na mafisadi sasa wanakuja kwa style ya kuwalia pesa zao kwa viwasha km hivyo then finally kila m2 anajua yeye atakacho kiofanya 2015, km unapata chance ya kula mali ya fisad we tumbua tu bt kwenye ballout box itakiua ni siri ya kila m2. lakini ngoja kwa sasa waendelee tu kupendeza kwa kanga na kofia, lowasa hata kwa jik hasafishif pamoja na kwamba ananafasi kubwa ya kupitishwa na cc ya ccm:A S-rap:
 
Back
Top Bottom