Raisi Mwenye nguvu ndani ya serikali yake,Kikwete au Karume

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Wajamani kutokana na hali ya mivutano katika mambo ya muungano ,kunaonekana kuna mivutano iliyowazi ambayo imefikia hadi viongozi wa juu wa serikali mbili zilizopo kurushiana maneno ya ubabe na hata kufikia baadhi ya viongozi kutoshiriki katika mikutano inayohusisha Chama na serikali zao.
Kuna mvutano uliotokea Musoma ,ambapo genge la Kikwete liliendeshwa puta na kutishiwa ikiwa halitafuata matakwa ya serikali ya Karume Muungano utakuwa mwisho na juzi baadhi ya viongozi wa serikali ya Karume hawakushiriki katika mkutano wa NEC akiwemo Karume na Waziri wa Nishati aliesema wazi kuwa mafuta hayamo katika muungano ,na baada ya kuundwa kamati ya kushughulikia wananchama wakorofi wanaozua mijadala migumu ndani ya chama cha CCM ,Zanzibar wamesema hawatishwi na kamati hiyo na haitaweza kumfunga mtu mdomo.
Inaonyesha Karume anawamiliki walio ndani ya serikali yake na Kikwete hana conrol yeyote ile ,je mnaonaje kwa hili ?
 
Kuna tetesi kuwa Karume kasikika akisema kuwa "sitaki upuuuzi wao siendi popote...." na Shamsi kenda kama mtuhumiwa na kutetea mradi wake wa 2010 tu.
 
Back
Top Bottom