Rais wa wataalamu wa maabara Yahya Mnung'a yupo mubashara Clouds 360 anazungumzia utafiti wa Rais Magufuli

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Anaitwa Yahya Mnung'a yuko clauds tv kwa sasa.

Kaulizwa papai linaweza kuwa na corona
Majibu: papai haliwezi kuwa na corona ila linaweza kuwa aliyelipeleka alilitoa wapi na limepitia katika mikono ya watu gani.

Swali: je maabara yetu inaweza kuwa na hujuma na wataalamu hewa?

Majibu: maabara yetu ni ya kimataifa na inawataalam labda kama vifaa vilivyokuja ndio tatizo kwa sababu vifaa vyote vinatoka nje ya nchi
 
Mnung'a anasema ule utafiti wa timu ya Rais Magufuli ulifanyika vizuri na kwa uhakika.

Mtaalamu huyu amesema baada ya kuongea na wataalamu mbalimbali duniani kufuatia utafiti huo wengi wamemueleza kuna tatizo la ubora wa vifaa hata katika nchi zao na hasa hivi vinavyotoka China.

Rais wa chama cha wataalamu wa maabara amewataka watanzania kutulia na kusubiri majibu ya uchunguzi wa tume ya Dr Mwigullu Nchemba.

Chanzo: Clouds Tv
 
Anaitwa Yahya Mnung'a yuko clauds tv kwa sasa
Yaani hii serikali kuna watu waajabu sana. Yaani wananunua muda kwenye television kumjibu Mdude Nyagali? Yaani hii ni dalili ya woga wa kupindukia. Waseme basi hayo makamasi ya mapapai na mafenesi waliyatoa wapi? Yaani hii ndiyo serikali duniani badala isaidie wataalamu wake inawajaribu kama ibilisi.
 
Mimi nimemsikiliza vizuri sana Mkuu wewe ume mquote jamaa wrong kabisa jamaa kafafanua poa sana hapo kusema papai inaweza kuwa na corona alisema hawezi kuujua sampuli takers walichukua katika maźingira yapi? Ila pia aka add kuwa kwa vile the purpose was for investigation basi The likely efficiency kubwa kwa handling ya hio samples was accurate ila pia Maabara wao hawahusiki na Kucheck izo equipments kuwa ziko na efficiency kiasi gani zipo mamlaka kama TBS ndo zilipaswa kufanya earlier check up kama the gadgets ziko efficiency kiasi gani.
 
Rais wa chama cha wataalamu wa maabara amewataka watanzania kutulia na kusubiri majibu ya uchunguzi wa tume ya Dr Mwigullu Nchemba.
Kwenye upimaji huenda kukawa na technical problem na solution yake lazima itokee kwenye technical analysis. Sasa unawapowatilia shaka scientist wako na kuingiza siasa za ubeberu na sabotage sioni solution itapatikana vipi. Utakuwa huna wa kumuamini. Wasi wasi wa JPM ungewahusisha WHO na WHO COVID-19 Reference Laboratory Network. Nina imani tungepata majibu sahihi, approach nyingine yeyote itakuwa na shaka. Hivi kweli Nchemba economist "No 1" ndiye wa kuongoza tume? Nauliza tu.
 
  • Thanks
Reactions: SMU

Nchemba ni multpurpose bwashee!

Kwa sasa wizara ya afya iko chini yake!
 
Mnung'a anasema ule utafiti wa timu ya Rais Magufuli ulifanyika vizuri na kwa uhakika.

Mtaalamu huyu amesema baada ya kuongea na wataalamu mbalimbali duniani kufuatia utafiti huo wengi wamemueleza kuna tatizo la ubora wa vifaa hata katika nchi zao na hasa hivi vinavyotoka China.

Rais wa chama cha wataalamu wa maabara amewataka watanzania kutulia na kusubiri majibu ya uchunguzi wa tume ya Dr Mwigullu Nchemba.

Chanzo: Clouds Tv
Kwa nini Mwigulu Nchemba awe ndio wa kuchunguza hilo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ute ute kidogo tu unaochukuliwa kama sampuli.
Ukichukua ute ute kidogo kwenye papai ni ngumu kuutofautisha na ute wa kamasi
Kwanza kwenye papai hakuna ute, halafu chemical reaction inatokeaje kwenye sampuli tofauti? Ukumbuke kipimo kimekua calibrated kupima specific sample zenye sifa ambazo kipimo itazigundua ndo ifanye kazi sahihi!?. Anyway nadhani hamna corona.
 
Basi ilitakiwa hicho kipimo kisilete majibu amabayo ni positive kwenye Hilo papai. Vinginevyo vina tataizo hivo vipimo.
Kama vinatambua ute ute tu,maana yake sampuli ambayo sio ute ilitakiwa visionyeshe majibu maana hakuna Cha kupima.
As far as I know sampuli yoyote maabara inapimika. Majibu sahihi inategemea na ubora wa vifaa ikiwa vigezo vingine vyote vipo kamili.
Kwanza kwenye papai hakuna ute, halafu chemical reaction inatokeaje kwenye sampuli tofauti? Ukumbuke kipimo kimekua calibrated kupima specific sample zenye sifa ambazo kipimo itazigundua ndo ifanye kazi sahihi!?. Anyway nadhani hamna corona.

Sent using LEAGOO M12
 
Yaani hii serikali kuna watu waajabu sana. Yaani wananunua muda kwenye television kumjibu Mdude Nyagali? Yaani hii ni dalili ya woga wa kupindukia. Waseme basi hayo makamasi ya mapapai na mafenesi waliyatoa wapi? Yaani hii ndiyo serikali duniani badala isaidie wataalamu wake inawajaribu kama ibilisi.

Makamasi? Pathetic! Ni bora ukatumia muda wako kujielimisha badala ya kuongelea usichokijua! Do you know that you can swab even surfaces (metal, wood, plastic, etc.) and test them for the virus?
 
Wataalamu bongo!

Watuambie kwanza tafiti zao zimefikia wapi kuhusu chanjo ya Corona kama wanavyofanya Wataalamu OG huko duniani.
 
Kama walitumia rapid tests majibu hayo yanawezekana tu.

Kwani si mliambiwa virus hao walitoka kwenye nyoka na popo?

Si ajabu kuwakuta kwenye kware na mbuzi.
Mimea pia ina virusi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom