Rais wa Tanzania anao uwezo kuzuia Bunge kumvua madaraka?

Mtaendelea kuorodhesha hayo hayo kila siku wakati mnajua hayana msingi na maamuzi yamefanyika na yanafanyika kwa Katiba ya JMT.

Kama yana mshiko nje ya Katiba, mahakama ipo na wanasheria mnao. Kwa nini msimuige marehemu Mchungaji Mtikila aliyekuwa akiendesha kesi za Kikatiba mwenyewe.

Mna Wabunge (watunga sheria), wenye uwezo wa kupeleka hoja binafsi Bungeni.

Badala yake, mnayaandika mitandaoni, kwenye vyombo vya habari, yanazungumzwa na kunung'unikiwa nje ya bunge, na kupigiwa kelele majukwaani.

Hivi mwazani Watanzania wote ni mbumbumbu wa Katiba, isipokuwa nyie!!

MTASUBIRI MACHEO HADI MACHEWO.
Nimejibu hoja kama ilivyo, habari ya wabunge wenu sijui takataka gani sina mda maana nahesabu bunge lote kama lilivyo sina wabunge wangu maana mimi si kamanda wala kada mkuu nayaongea mapungufu yaliyopo katika uhalisia na si ushabiki wa kijinga
 
Nitakujibu ukifafanua maana maana yako ya "ushabiki wa kijinga".
 
WASWAHILI husema: mfa maji haachi kutapatapa. Si raia wote wanaokubali mkondo wa sheria uwaingilie kirahisi. Wengine wanashawishika kuficha ushahidi, kuhonga, kusema uongo, kupandikiza mashahidi, kuwadhuru au wakati mwingine kuwaua mashahidi dhidi yao, na mbinu nyingine zilizo au zisizo halali.

Bunge likianza kumchunguza, kumshitaki, na ikibidi kumuondoa madarakani Rais wa nchi kwa mujibu wa katiba, hatakaa kimya au kusalimu, bali atafurukuta na kutumia kila silaha aliyonayo mkononi ili kuweka vigingi katika mkondo wa sheria.

Makosa yanayoweza kuchochea Bunge kupitisha azimio la kumshitaki Rais yameainishwa katika ibara ya 46 A (2) (a), (b), na (c) ya Katiba ya Tanzania. Baadhi ya hayo ni; vitendo ambavyo kwa ujumla vinaivunja Katiba au sheria ya maadili ya viongozi wa umma, au mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano. Pia, utaratibu unaofuatwa na Bunge kumuondoa Rais madarakani umeelezwa katika ibara ya 46 A kuanzia kifungu kidogo (3) mpaka (10) cha Katiba ya Tanzania.

Hatua muhimu ya Bunge kumshitaki Rais, inaanza wakati Spika wa Bunge anapopokea taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya Wabunge wote (rejea ibara ya 46 A (3) (a) (b) na (c) ya Katiba ya Tanzania). Taarifa hiyo inatakiwa iwasilishwe kwa Spika siku 30 kabla ya kikao ambamo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa bungeni, ikifafanua makosa aliyotenda Rais, na ikipendekeza kuwa kamati Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze mashitaka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais.

Baada ya Spika kupokea taarifa ya maandishi na kujiridhisha kuwa masharti ya katiba yametimizwa, mtoa hoja ataruhusiwa kutoa hoja hiyo bungeni, kisha wabunge, bila kufanya majadiliano, watapiga kura juu ya hoja ya kuunda Kamati Maalumu ya Uchunguzi. Ikiwa hoja hiyo itaungwa mkono na wabunge wasiopungua theluthi mbili ya wabunge wote, Spika atatangaza majina ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.

Je, Rais hawezi kutumia madaraka aliyonayo kuwatetemesha wajumbe wa kamati iliyoundwa kumchunguza, au kuvunja Bunge ili kusitisha jaribio la kumshitaki?

Hoja hiyo inajibiwa na ibara ya 90 (2) (a) ya Katiba ya Tanzania, ambapo, Rais anapokonywa mamlaka ya kuvunja Bunge ikiwa Spika atapokea taarifa rasmi inayopendekeza kuundwa kwa Kamati Maalumu ya Uchunguzi kwa madhumuni ya kumuondoa Rais madarakani.

Jibu jingine linapatikana katika ibara ya 46 A (5), ambapo, endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazi na madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37 (3), yanayomtaka mmoja wapo kati ya Makamu wa Rais, Spika wa Bunge, au Jaji Mkuu, kuwa Rais wa muda.

Lakini tutakuwa tunajiongopea tukidhani kuwa wabunge wako salama dhidi ya njama za Rais wanayetaka kumuondoa madarakani. Mwaka 1992 Katiba ya Tanzania ilifanyiwa marekebisho ili kukidhi mageuzi ya kutoka mfumo wa chama kimoja kwenda katika mfumo wa vyama vingi vya siasa. Mojawapo ya marekebisho hayo ni ibara ya 71 (1) (e) ya Katiba ya Tanzania, ambapo mbunge atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge ikiwa ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa mbunge.

Hivyo basi, mbunge akifukuzwa uanachama wa chama chake cha siasa, hata kama Bunge halijakamilisha zoezi la kumshitaki Rais, anapoteza nafasi yake ya ubunge, na kiti chake kinakuwa wazi. Kwa mujibu wa ibara ya 64 ya kanuni za Bunge, inayoongezewa nguvu na ibara ya 95 ya Katiba ya Tanzania, Bunge laweza kutekeleza shughuli wakati wa vikao vyake bila kujali kwamba kuna kiti kilicho wazi miongoni mwa viti vya Wabunge. Hivyo, maamuzi ya vikao vya Bunge hayawezi kuharamishwa.

Katiba ya Tanzania na katiba za vyama vya siasa nchini hazijatamka kwamba Rais lazima awe au asiwe Mwenyekiti wa chama tawala. Hata hivyo, vyama vya siasa nchini vimejenga mazoea ambapo, Rais au mgombea urais kwa tiketi ya chama, anakuwa ndiye Mwenyekiti wa Chama husika. Ikitokea kuwa Rais amesimamishwa kwa muda ili achunguzwe kwa mujibu wa katiba, Mwenyekiti wa chama tawala, ambaye ndiye Rais mwenyewe, anaendelea na kazi yake ya uenyekiti wa chama tawala.

Mwenyekiti wa chama tawala (ambaye ni Rais aliyesimamishwa kwa muda), anaweza kuanzisha mchakato halali, bila kuvunja sheria za nchi, wa kuwafuta uanachama wabunge wote kutoka katika chama tawala ambao wanaunga mkono hoja ya kumshitaki. Hivyo basi, ni wazi kuwa ibara ya 46 A (5) ya Katiba ya Tanzania, inayomvua Rais madaraka kwa muda wakati anachunguzwa, na ibara ya 90 (2) (a) ya Katiba ya Tanzania, inayomnyima uwezo Rais kuvunja Bunge wakati anachunguzwa, zinazimuliwa na utaratibu wa kofia mbili.

Hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na azimio la Bunge linalothibitisha au kutokuthibitisha mashitaka dhidi ya Rais, linahitaji kuungwa mkono kwa kura za wabunge wasiopungua theluthi mbili ya wabunge wote. Lakini Rais (Mwenyekiti wa chama tawala), akifanikiwa kuwavua uanachama wabunge wa chama tawala wasiomuunga mkono, (ambao watapoteza ubunge wao papo kwa papo), atabakia na wabunge wa chama tawala wanaomuunga mkono na wabunge wote wa vyama vya upinzani.

Katika hali ya namna hii, jaribio la Bunge la kumshitaki Rais linaweza kuzimwa kutegemea wingi wa Wabunge wa upinzani wanaounga mkono jaribio hilo. Mfano wa kufikirika ni kutoka katika Bunge la mwaka 2005 – 2010, lenye idadi ya Wabunge 271 kutoka CCM, na Wabunge 45 kutoka vyama vya upinzani (CUF 32, CHADEMA 11, TLP mmoja, na UDP mmoja).

Wabunge wa vyama vya upinzani hawawezi kufanikiwa kutoa taarifa ya maandishi kwa Spika, mpaka waungwe mkono na wabunge wasiopungua 18 kutoka CCM (sidhani kama inawezekana). Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa taifa wa CCM, akipata fununu za kuwapo wabunge wanaotaka kumuondoa madarakani, anaweza kuitisha kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM (rejea ibara ya 107 (2) ya katiba ya CCM), kwa lengo la kuwafuta uanachama wabunge wote wa CCM wanaotaka kumuondoa madarakani (rejea ibara ya 108 (8) ya katiba ya CCM), hata kabla ya kikao ambamo hoja yao inakusudiwa kutolewa bungeni. Hoja ya kumshitaki Rais itakosa idadi ya kutosha ya wabunge watakaoiunga mkono, hivyo, itakufa kifo cha kawaida.

Bahati mbaya katiba za vyama vya siasa nchini, zimetoa mianya ya Mwenyekiti wa taifa wa chama husika kuwa na madaraka makubwa sana. Vilevile, kwa kiasi kikubwa, madaraka makubwa ya vyama vya siasa yanahodhiwa na kamati au vyombo vya kitaifa, ambavyo wajumbe wake wengi hawapatikani kwa kuchaguliwa moja kwa moja na wananchama, bali wanapendekezwa au kuteuliwa, halafu kuthibitishwa na chombo au mkutano mkuu wa chama.

Mfano, Wajumbe 14 wa Kamati Kuu ya CCM wanapatikana kwa kupigiwa kura kutoka katika orodha ya majina 30 iliyotayarishwa na Mwenyekiti wa Taifa CCM. Vile vile, wajumbe 10 wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wanateuliwa na Rais kwa mujibu wa ibara ya 108 (13) (e) ya katiba ya CCM. Vilevile, kwa mujibu wa ibara ya 7.7.14 (l) ya katiba ya CHADEMA, Mwenyekiti, kwa kushauriana na Katibu wa chama, anateua wajumbe 6 wa Kamati Kuu, ambao wanathibitishwa na Baraza Kuu la CHADEMA.

Kwa mujibu wa ibara ya 108 (8) ya katiba ya CCM, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ndicho chombo chenye mamlaka ya kumfuta uanachama Mbunge wa CCM. Pia, kwa mujibu wa ibara ya 110 (7) ya katiba ya CCM, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, ndicho chombo kinachoweza kusimamisha kiongozi yeyote wa CCM, isipokuwa Mwenyekiti wa Taifa na Makamu wake wawili. Lakini wajumbe wengi wa kamati hizi mbili wanapatikana baada ya Mwenyekiti wa CCM, akishirikiana na kamati hizo hizo mbili kuwachuja (rejea “kanuni za uchaguzi wa CCM” ibara ya 99 mpaka 116 toleo la Februari, 2005).

Mwenyekiti wa taifa wa CCM (ambaye ni Rais), Makamu wake wawili na Makatibu ngazi ya taifa, ambao wanapatikana kwa kupendekezwa na Mwenyekiti mwenyewe, halafu kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM, ni viongozi wenye mamlaka makubwa katika chama. Wakishikamana na kutaka kuwafuta wabunge uanachama, ni nadra kwa mjumbe yeyote wa hizi kamati mbili kuwapinga bila kugonga ukuta. Muundo wa chama umewawekea mazingira ya kupitisha jambo lolote wanalolitaka bila kupingwa na wanachama wa CCM.

Mfano, katika barua kwa Mwenyekiti wa CCM: Joseph Butiku anaeleza; “Mwenyekiti aliamua, yeye mwenyewe katikati ya kikao na bila ushauri wa kiongozi mwingine yeyote, kubadili kanuni ya uchaguzi wa mjumbe mmoja kura tatu. Kanuni hii ilikuwa imejadiliwa awali, kabla ya kikao cha Halmashauri Kuu cha tarehe 4/8/2005.

Halmashauri Kuu chini ya Mwenyekiti, ikaamua kanuni hiyo isibadilishwe. Lakini baadaye kanuni hiyo, ndiyo iliyobadilishwa, bila sababu yoyote ya msingi, kwa usimamizi wa shinikizo la Mwenyekiti wakati wa kikao cha uteuzi wa wagombea” (Tanzania Daima Oktoba 17, 2007).

Miundo ya vyama vingine haina tofauti sana na muundo wa CCM. Baadhi ya vyama vinakiuka katiba na kuendeshwa kama familia, tena familia za kizamani, ambapo Mwenyekiti wa chama ni kama Baba mwenye nyumba, kwa maana kuwa, kama hayupo chakula hakipakuliwi. Ndio maana baadhi ya vyama, Mwenyekiti asipogombea urais, chama hakisimamishi mgombea urais. Sitarajii mazoea ya kukiuka katiba za vyama kubadilika baada ya kuchukua madaraka ya kuongoza nchi. Badala yake, mazoea mabaya yatahamishiwa katika uongozi wa nchi.

Rais anatumia kofia mbili kama kinga ya kuondoa karaha. Bunge likitaka kumdhibiti, anavaa kofia ya Mwenyekiti wa chama tawala na kulinyamazisha kwa kupitia mlango wa nyuma. Wanachama wa chama tawala wakitaka kumdhibiti, anavaa kofia ya Rais wa nchi na kuwanyamazisha. Ndiyo maana kama Bunge lina idadi kubwa ya wabunge kutoka katika chama tawala, uwezekano wa kumwajibisha Rais ni mdogo sana.

Labda nitoe mfano wa kufikirika, ambapo baada ya uchaguzi mkuu Bunge likawa na jumla ya Wabunge 320, vyama vya upinzani vikawa vinaongoza kwa jumla ya wabunge 220 na chama tawala kikawa na Wabunge 100. Uwiano wa namna hii ndio unaweza kufanikisha azima ya Bunge kumshitaki Rais, kwa sababu Rais kama Mwenyekiti wa chama tawala hana madhara kwa wabunge wa vyama vya upinzani.

Idadi ya wabunge wa vyama vya upinzani itatosha kumwajibisha Rais, bila kuhitaji kuungwa mkono na wabunge wa chama tawala. Bahati mbaya, uwiano wa namna hii hauwezi kutokea chini ya katiba ya sasa. Ikitokea kwamba wananchi wamechagua idadi kubwa ya wabunge wa vyama vya upinzani kuzidi wabunge wa chama tawala, Rais anaweza kuvunja Bunge chini ya ibara ya 90 (2) (e) ya Katiba ya Tanzania.

Katika mada: “Nafasi ya Bunge kama mhimili wa Dola”, Spika mstaafu, Pius Msekwa, anaeleza kuwa; “ibara ya 90 (2) (e) iliwekwa baada ya kuingia katika mfumo wa vyama vingi kutokana na kutambua kwamba Bunge la vyama vingi vya siasa ni Bunge la ushindani wa kushindania madaraka ya Serikali. Ushindani huo unaanza wakati wa kampeni za uchaguzi na unahamia bungeni baada ya uchaguzi kumalizika.

Kwa hiyo Wabunge wa chama tawala wanawajibika kwa mujibu wa kanuni hizo za ushindani kuunga mkono hoja za Serikali iliyoundwa na chama chao. Madhumuni ya kanuni hiyo ni kutaka kuepusha madhara kwa Serikali iliyoundwa na chama chao yanayoweza kutokea kwa mujibu wa ibara ndogo za (b), (c), na za ibara hiyo ya 90 (2) ya katiba, ikisomwa pamoja na ibara nyingine, zinazotoa nafasi kwa Serikali iliyopo kuweza kuondolewa madarakani na Bunge” (Raia Mwema Januari 2, 2008).

Hoja ya Pius Msekwa ina ukweli ndani yake, kwani ikitokea, kama nilivyoainisha katika mfano wangu wa juu, wabunge wa upinzani wakawa wengi kuzidi wa chama tawala, miswada ya sheria au bajeti za serikali ya chama tawala zinaweza kukwamishwa bungeni, na hata serikali kuondolewa madarakani.

Lakini ukweli wa hoja ya Pius Msekwa, hauwezi kupiku mantiki ya ibara ya 8 (1) (a) (b) na (c) ya Katiba ya Tanzania. Ushindi halali wa serikali na vyama vya siasa bungeni, unatokana na utashi wa wananchi, ambao ndio msingi wa mamlaka yote. Chama kilichojizatiti katika ushindani wa nguvu ya sera, na si sera ya nguvu, ndio hutwaa madaraka ya serikali.

Ibara ya 90 (2) (e) ya Katiba ya Tanzania inapingana na makusudio ya ushindi unaopatikana baada ya kushindanisha sera za vyama. Wamarekani wanasema, “we are defeating our own purpose”. Hata kabla kura hazijapigwa, katiba imekwisha wekewa mazingira ya kufuta matokeo yasiyoingia akilini mwa Rais wa chama kitakacho tawala. Je, uchaguzi mwingine ukiitishwa, na uwiano ukawa kama uliokataliwa mwanzo, Bunge litavunjwa tena?

Vile vile, ibara hii inalenga kuendeleza ukiritimba wa mfumo wa chama kimoja, kwa sababu inajenga mazingira ya kuhakikisha kuwa, chama kinachotawala ndicho kitakuwa na wabunge wengi.

Binafsi, nilidhani ikitokea wabunge wa vyama vya upizani wakawa wengi kuzidi wabunge wa chama tawala, maana yake ni kwamba wananchi wanataka mseto wa sera, au uundwaji wa serikali ya kitaifa inayoshirikisha viongozi kutoka vyama vya upinzani. Kufuta matokeo ya kura ya wananchi ni sawa na kuwaambia kwamba ni wajinga, hawajuhi kuchagua.

Rais akiweza kuzima jaribio la Bunge la kumshitaki (kama nilivyobainisha), basi ibara ya 46 A (1) ya Katiba ya Tanzania inayosema “Bunge laweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani” inabaki kuwa nakshi ya kufurahisha macho. Hakuna njia nyingine halali ya kumdhibiti Rais kwa sababu ibara ya 46 (1), (3) ya Katiba ya Tanzania, inapiga marufuku kumshitaki au kuendesha mashitaka ya aina yoyote juu ya Rais Mahakamani kwa kosa lolote la jinai. Kwa mantiki hii, Rais anakuwa juu ya sheria, na akistaafu anapumzika salama salimini.

Ndiyo maana si vema kupuuza hoja za kudai katiba mpya, ambayo haitakuwa na mizengwe katika utaratibu mzima wa Bunge kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani.
KAMA ULIKUWA HUJUI MADARAKA YA RAIS WA JAMHURI MUUNGANO WA TANZANIA NI MAKUBWA KUPITA KIASI. TULISHUHUDIA AWAMU ILIYOPITA RAIS AKISAINI MIKATABA LUNDO BILA HATA KUISOMA NA KUITAFISIRI KWA WANANCHI WAKE UTAFIKIRI NCHI NI MALI YAKE.

SIKU HIZI MAMBO YOTE YANAAMULIWA NA WACHACHE UTAFIKIRI SERIKALI NI KAMPUNI YA MTU BINAFSI.

HIVI PESA ZA UPANUZI WA BARABARA YA MWANZA IENDAYO UWANJA WA NDEGE ZILIPITISHWA NA NANI?

HIVI GHARAMA ZA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE CHATO ZILIJADILIWA NA AKINA NANI?

YAPO MENGI ILA ... MUNGU NDO ANAYEJUA..
 
Safari ineanza kuna siku tutafika huko. Hata Roma haikujengwa siku moja.
 
Kwa ujinga na kutokomaa Kidemokrasia bado Tanzania hatustahili kumpa raisi mamlaka kupitiliza.
topcombofr.jpg

John Leonard Minja

Mkuu kuna mambo mengine yapo ndani ya uwezo wa mwanadamu, Mungu unamsumbua bure kwa yanayoendelea Tanzania na Afrika
 
Back
Top Bottom