Rais wa Gabon abwaga manyanga

Mabbyjr

Member
Aug 19, 2007
29
1
Rais wa Gabon Bw. Omar Bongo ameachia ngazi ya urais kwa muda kwa sababu ya matatizo ya kiafya.
Rais huyu kutoka Afrika ya Magharibi amekuwa madarakani tangu mwaka 1967 amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa ambao hadi sasa haujawekwa hadharani.
Wananchi pamoja na viongozi wa upinzani nchini humo wamekuwa na wasiwasi wa hali hii ambayo wanahisi itasababisha utupu katika utawala. Viongozi wa upinzani nchini humo wanahofia kuwa Mtoto wa kiume wa Rais huyo aitwaye Ali Ben Bongo yuko tayari kubeba majukumu ya baba yake. Kwa sasa mwana huyo wa Rais Bongo ndiye waziri wa ulinzi nchini humo.

Hadi sasa serilaki ya Gabon haijaweza kueleza Rais wao anasumbuliwa na ugonjwa gani na wala hawajawa tayari kutaja ni nchi gani anakotibiwa na tangu lini yuko hospitalini.
 
Sii huyu2 mke wake amefariki dunia hivi karibuni?

Pia haikuelezwa mke kapata alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa gani!
 
Rais huyu kutoka Afrika ya Magharibi amekuwa madarakani tangu mwaka 1967

42 yrs!!! I think he has outdone all African leaders in terms of longevity of leadership. Even Libya's Gadaffi; Zaire's Mobutu Sese Seko and Malawi's Kamuzu Banda, who proclaimed themselves as presidents-for-life.
 
Je ukweli wowote ktk hizi habari??

Mkuu unaweza kwenda kwenye vyombo vya habari vya kimataifa utakuta habari hii. Mfano New York Times, Reuters, CNN.

Huyu Prezidaa ni mla rushwa mkubwa barani Afrika, akaunti yake iliwahi kuwa frozen na serikali ya Ufaransa baada ya kulipwa maelfu ya dola za kimarekani ili kumwachia huru mfanyabiashara wa kifaransa Rene Cardona. Iliwekewa dola za kimarekani zaidi ya 580,000 kwenye akaunti yake nchini Ufaransa.
 
Sii huyu2 mke wake amefariki dunia hivi karibuni?

Pia haikuelezwa mke kapata alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa gani!

Ni kweli mkewe alifariki mwezi Machi mwaka huu ingawa hadi leo hakuna ambaye anajua zaidi ya mmewe na madaktari nini kilichomuua huyu Mrs Bongo ambaye pia alikuwa ni mtoto wa Rais Denis Sassou Nguesso wa Congo. Kitu kikubwa kilichokuwa kinawaunganisha hawa marais zaidi ya kuolea binti ilikuwa ni RUSHWA. Naamini hata huu uchafu Bongo kwetu nako upo. Kuna viongozi ambao wameoleana ndugu wakajikweza juu ya vinara vya uongozi wa Taifa letu huku wakishirikiana kugawana RUSHWA.
 
Back
Top Bottom