Rais simama ulikomboe Taifa

Pantosha

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
351
466
Ni mapema alfajiri nimeamka na kuanza kuyatafakari haya maisha tunayoishi. Najiuliza hadi lini serikali itajua ni wajibu wake kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma zote muhimu kwa viwango vinavyostahili?

Serikali naona inachelewa sana kuwaletea wananchi maendeleo.

Leo hii watu maji majumbani hakuna,
Leo hii umeme siyo wa uhakika,
Leo hii miundombinu ya barabara mibovu,
Leo hii miji uchafu umetapakaa kila kona,
Leo hii shule zina uhaba wa madarasa, vitabu, walimu wenye ujuzi nk.

Tunakuomba Rais utusaidie nchi ikae sawa.

Tunakuombea afya njema wewe na familia yako ili na wewe uhakikishe na sisi tunaishi maisha mazuri.
 
Jukumu la kuishi maisha unayoyaita 'mazuri' sio la rais

Jukumu hili ni la kibinadamu ambalo wewe mwenyewe ndio unatakiwa uyafanye maisha yawe 'mazuri'

Mathalani, baadhi ya mbinu za kufanya maisha yako yawe mazuri ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii, kuisimamia vizuri kazi au biashara au shughuli yako unayoifanya kwa ufasaha ili upate matokeo chanya na kujiongezea maarifa, stadi na ujuzi katika ulimwengu huu wa kibiashara na teknolojia

Hivyo tu yaan. Lakini ukitegemea eti dunia au serikali iyatengeneze maisha yako kuwa mazuri sio rahisi usikute hata wewe sio priority kwa serikali hii. Ishi humo
 
Acha kuomba, hamna kitu hapa. Ni sissi watanganyika kukomboa nchi yetu. Fikiria on that lines, siyo kuomba
 
Tangu uchaguzi mkuu wa 1995 CCM hiwaahidi watu
Maji
Afya
Shule/elimu
N k
Leo hii mwana CCM mmoja anazurura akijifanya katumwa na Rais eti kasikia kilio cha wananchi.
Mwafrika hatoboi mpaka Dunia iishe
Mtawala anashangaa
Wateule wanashangaa
Wananchi wanashangaa.
Nani sasa hapo atamkomboa mwenzake?
 
Tatizo wanaiba pakubwa,pesa za kusambazia huduma zinapelea.Ibeni kidogo tu mtukumbuke na Sisi huku tunauhitaji.Mnatapanya Mali hovyo mkifa hawawaziki nazo zinaendelea kuchezewa hovyo Kabisa.Kuweni na huruma,Mwenyezi Mungu anapokupa hakupi ule peke yako wasambazieni na wengine.Mwenyezi Mungu awakumbushe hili.🙏🏽
 
Akiifanyia kazi ripoti ya CDF atafanikiwa kulikomboa Taifa
 
Ni mapema alfajiri nimeamka na kuanza kuyatafakari haya maisha tunayoishi. Najiuliza hadi lini serikali itajua ni wajibu wake kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma zote muhimu kwa viwango vinavyostahili?

Serikali naona inachelewa sana kuwaletea wananchi maendeleo.

Leo hii watu maji majumbani hakuna,
Leo hii umeme siyo wa uhakika,
Leo hii miundombinu ya barabara mibovu,
Leo hii miji uchafu umetapakaa kila kona,
Leo hii shule zina uhaba wa madarasa, vitabu, walimu wenye ujuzi nk.

Tunakuomba Rais utusaidie nchi ikae sawa.

Tunakuombea afya njema wewe na familia yako ili na wewe uhakikishe na sisi tunaishi maisha mazuri.
Jana niliponunua sukari kwa Shilingi 6500 nilitafakari sana!! Rais anajua au hajui? Kama hajui kwanini haambiwi? Kama anajua kwanini anakaa kimya?

Juzi tumeshuhudia yule Waziri wa Kilimo Msomali aking'aka kwamba hakuna wa kumhoji zaidi ya watu watatu tu! Kwamba hata Wananchi aliowadanganya kuhusu sukari na bei yake elekezi hawana haki ya kumhoji!!

Kwanini Rais hashughuliki na huyu Msomali? Anamuogopa Kinana?

Rais jitokeze hadharani tuzungumze na Taifa. Nchi usimuachie Makonda peke yake. Jitokeze, unasuburi kujitokeza kwenye jambo Gani??

JK alisema kwenye Mkutano Mkuu mwaka juzi, na Sasa Watanzania na wana CCM kwa ujumla tunaendelea kusubiri MAMBO YAHARIBIKE ZAIDI.
 
Kwm
Jukumu la kuishi maisha unayoyaita 'mazuri' sio la rais

Jukumu hili ni la kibinadamu ambalo wewe mwenyewe ndio unatakiwa uyafanye maisha yawe 'mazuri'

Mathalani, baadhi ya mbinu za kufanya maisha yako yawe mazuri ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii, kuisimamia vizuri kazi au biashara au shughuli yako unayoifanya kwa ufasaha ili upate matokeo chanya na kujiongezea maarifa, stadi na ujuzi katika ulimwengu huu wa kibiashara na teknolojia

Hivyo tu yaan. Lakini ukitegemea eti dunia au serikali iyatengeneze maisha yako kuwa mazuri sio rahisi usikute hata wewe sio priority kwa serikali hii. Ishi humo
Kwamba ukifanya kazi kwa bidii Umeme unapatikana, Sukari inashuka bei, Wakandarasi tunalipwa, miradi inakamilika na safari za kutalii nje zinakoma!!!?

Hii ndo tabu ya hili kundi likipata madaraka
 
Ni mapema alfajiri nimeamka na kuanza kuyatafakari haya maisha tunayoishi. Najiuliza hadi lini serikali itajua ni wajibu wake kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma zote muhimu kwa viwango vinavyostahili?

Serikali naona inachelewa sana kuwaletea wananchi maendeleo.

Leo hii watu maji majumbani hakuna,
Leo hii umeme siyo wa uhakika,
Leo hii miundombinu ya barabara mibovu,
Leo hii miji uchafu umetapakaa kila kona,
Leo hii shule zina uhaba wa madarasa, vitabu, walimu wenye ujuzi nk.

Tunakuomba Rais utusaidie nchi ikae sawa.

Tunakuombea afya njema wewe na familia yako ili na wewe uhakikishe na sisi tunaishi maisha mazuri.
Rais yupi huyo wa kuyafanya haya unayoyasema yote? Watanzania wengi ni hamnazo
 
Tatizo wanaiba pakubwa,pesa za kusambazia huduma zinapelea.Ibeni kidogo tu mtukumbuke na Sisi huku tunauhitaji.Mnatapanya Mali hovyo mkifa hawawaziki nazo zinaendelea kuchezewa hovyo Kabisa.Kuweni na huruma,Mwenyezi Mungu anapokupa hakupi ule peke yako wasambazieni na wengine.Mwenyezi Mungu awakumbushe hili.
Unataka hao unaowaita wezi, wazisambaze hizo pesa za wizi kwa style ipi mkuu
 
Kwm
Kwamba ukifanya kazi kwa bidii Umeme unapatikana, Sukari inashuka bei, Wakandarasi tunalipwa, miradi inakamilika na safari za kutalii nje zinakoma!!!?

Hii ndo tabu ya hili kundi likipata madaraka
Achana nae.
kunawatu sijui wanatumia Nini kufikiri ndugu.
 
Jukumu la kuishi maisha unayoyaita 'mazuri' sio la rais

Jukumu hili ni la kibinadamu ambalo wewe mwenyewe ndio unatakiwa uyafanye maisha yawe 'mazuri'

Mathalani, baadhi ya mbinu za kufanya maisha yako yawe mazuri ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii, kuisimamia vizuri kazi au biashara au shughuli yako unayoifanya kwa ufasaha ili upate matokeo chanya na kujiongezea maarifa, stadi na ujuzi katika ulimwengu huu wa kibiashara na teknolojia

Hivyo tu yaan. Lakini ukitegemea eti dunia au serikali iyatengeneze maisha yako kuwa mazuri sio rahisi usikute hata wewe sio priority kwa serikali hii. Ishi humo
Umeandika vizuri kwa upande wa mtu kujikwamua kiuchumi yeye kama yeye. Ndiyo maana hujasikia nikisema serikali inijengee nyumba. Huko hatujafika. Ila zipo serikali zingine katika dunia hii tunayoishi wote zinawapa hadi viwanja wananchi wake, elimu bure, matibabu bure, nk.
Jifunze kazi/majukumu/wajibu wa serikali kwa wananchi wake. Utanielewa.

Ila hapa naongelea serikali kufanya majukumu yake ya kutuletea maendeleo. Hiyo ndiyo sababu serikali inasimamia rasilimali zetu pamoja na kodi zetu.

Hapa tunaidai serikali ituletee maji, umeme, barabara nzuri, shule mzuri, walimu wazuri, hospitali nzuri, kukusanya taka, nk.
 
Tatizo wanaiba pakubwa,pesa za kusambazia huduma zinapelea.Ibeni kidogo tu mtukumbuke na Sisi huku tunauhitaji.Mnatapanya Mali hovyo mkifa hawawaziki nazo zinaendelea kuchezewa hovyo Kabisa.Kuweni na huruma,Mwenyezi Mungu anapokupa hakupi ule peke yako wasambazieni na wengine.Mwenyezi Mungu awakumbushe hili.🙏🏽
Hiki ndiyo kilio chetu sote!
 
Nikiona watu mnalalamika hali mbaya nawahurumia na mimi nashangaa...Nchi hii ni kama Ndege inayojiendea endea angani mana hali ya kila eneo iko hovyo hakuna anaejali hakuna anaeogopa yaani Magufuli alituacha pagumu sana lakini pia Tukubali uongozi sio kupeana tu hali ya uomgozi ni ngumu..Ukiangalia mfano rahisi safari ya Dar Motogoro tu kuja hali mbaya sana hapo masaa 5 mpaka 6 kusafiri hapo km 200 tu na hawa watu hawajali wala hawaoni soni...Kila kitu kinajiendea hovyo..enzi za Magufuli alikua mkali sana ujinga ujinga huu usingekuepo...Serikali ilikua ipo na inasikika leo hii hamna kitu...ni Kuiba kuiba tuu ukiangalia mvua zimeharibu miundombinu ambayo enzi za Magufuli hata kama hakukuepo lami barabara zilikua nzuri sana...
 
Ni mapema alfajiri nimeamka na kuanza kuyatafakari haya maisha tunayoishi. Najiuliza hadi lini serikali itajua ni wajibu wake kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma zote muhimu kwa viwango vinavyostahili?

Serikali naona inachelewa sana kuwaletea wananchi maendeleo.

Leo hii watu maji majumbani hakuna,
Leo hii umeme siyo wa uhakika,
Leo hii miundombinu ya barabara mibovu,
Leo hii miji uchafu umetapakaa kila kona,
Leo hii shule zina uhaba wa madarasa, vitabu, walimu wenye ujuzi nk.

Tunakuomba Rais utusaidie nchi ikae sawa.

Tunakuombea afya njema wewe na familia yako ili na wewe uhakikishe na sisi tunaishi maisha mazuri.
Kwenye afya yake na familia yake mko pamoja ila uhakika wa maisha mazuri kwa raia sidhani
 
Jukumu la kuishi maisha unayoyaita 'mazuri' sio la rais

Jukumu hili ni la kibinadamu ambalo wewe mwenyewe ndio unatakiwa uyafanye maisha yawe 'mazuri'

Mathalani, baadhi ya mbinu za kufanya maisha yako yawe mazuri ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii, kuisimamia vizuri kazi au biashara au shughuli yako unayoifanya kwa ufasaha ili upate matokeo chanya na kujiongezea maarifa, stadi na ujuzi katika ulimwengu huu wa kibiashara na teknolojia

Hivyo tu yaan. Lakini ukitegemea eti dunia au serikali iyatengeneze maisha yako kuwa mazuri sio rahisi usikute hata wewe sio priority kwa serikali hii. Ishi humo
Umezungumza kwa uwazi ila nikukumbushe kitu kimoja tu. Serikali yeyote inayojitambua inategemea zaidi raia wake kama rasilimali kuu kuliko ambavyo unaweza kudhani. Watu wafanye kazi ikusanye mapato kwa ajili ya kuboresha mazingira ya hao watu na hali zao kwa ujumla.

Nikupe mfano halisi tu juu ya uhusiano wa serikali na mwananchi.

Unaweza ukaajiriwa mahala kama mhasibu katika kampuni kubwa ambapo kazi ni nyingi. Kwa dunia ya sasa kila kitu kinakuwa computerized ili kuleta ufanisi ila itokee kwamba kampuni yako kwa makusudi tu na visingizio lukuki haitaki kununua software za kurahisisha kazi kwa sababu tu hesabu zinawezekana kufanyika manually. Chukulia we mwajiriwa kama raia na kampuni kama serikali. Utatumia masaa mengi kuumiza kichwa sana na kufanya kazi ndogo kwa muda mrefu sana kitu ambacho kinapunguza ufanisi ilihali unaisaida kampuni kupitia mchango wako wa kitaaluma.

Hiki hakina tofauti na unachotetea kwamba mwananchi afanye kazi kwa bidii ili ajiletee maendeleo. Analipa kodi za serikali ila maji anatumia ya chumvi na alishalipia bomba la majisafi serikalini, umeme hana na alishalipia kufungiwa meter na luku ya Tanesco. wakati mwengine umeme hakuna. Serikali yetu ina dodge kuwajibika kwa raia kwenye mambo mengi sana na haitaki kuwa Questioned.
 
Kwm
Kwamba ukifanya kazi kwa bidii Umeme unapatikana, Sukari inashuka bei, Wakandarasi tunalipwa, miradi inakamilika na safari za kutalii nje zinakoma!!!?

Hii ndo tabu ya hili kundi likipata madaraka
Huyo jamaa ni tatizo. Wanafikiria mpaka pale njaa zao zinapoishia.
 
Wakati linazama alikuwepo,liko limezama yupo,sasa atalikomboa vipi wakati yeye mwenyewe alishiriki kulizamisha!
 
Back
Top Bottom