Rais Samia Walinde Watanzania Dhidi ya Mauaji ya Pikipiki

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Leo hii, japo pikipiki zimekuwa ni chombo kinachotegemewa na wengi kwa usafiri lakini kwa upande mwingine zimekuwa janga kwa Taifa. Hazijawa janga kwa Taifa kwa sababu zenyewe ni janga kwa asili yake bali kwa sababu ya unafiki wa Serikali.

Kuna wakati Polisi walitaka kudhibiti uendeshaji ovyo wa pikipiki lakini wanasiasa na viongozi wa Serikali wanafiki wakazuia zoezi hilo.

Kwa wakati tofauti, nimeshuhudia vifo vya watoto wawili, watu wazima watatu waenda kwa miguu, waebdesha pikipiki wawili na ulemavu wa mama mmoja, vyote vikiwa vimesababishwa na uendeshaji wa ovyo wa pikipiki.

Kifo cha kwanza kilikuwa cha mtoto wa shule wa kike mjini Singida. Nilitoka Dodoma, naelekea Mwanza, watoto walikuwa wametoka shule, nikawa naendesha gari taratibu kwaajili ya usalama wa watoto, lakini mbele yangu ilkuja pikipiki, uendeshaji wake ni kama wa mtu kichaa, kwa kasi ilipishana na gari langu, nilishangaa. Mara nilisikia kishindo kwa nyuma, nikatizama kwenye side mirror, mwendesha pikipiki akawa tayari amemgonga binti mdogo, wa darasa la 4. Niligeuza haraka gari, nikasaidiana na akina mama wawili walikuwa karibu, tukamkimbiza mtoto hospitali ya mkoa wa Singida. Simanzi ikiwa imenijaa, masikitiko yasiyoelezeka. Sikuondoka, nilitaka nijue maendeleo yake. Baadaye mama mzazi wa mtoto alifika. Baadaye nikaongea na daktari tena, naye akanihakikishia kuwa mtoto amepata fahamu anaendelea vizuri. Nikashusha pumzi nikaondoka. Lakini nilipenda sana nijue maendeleo ya yule mtoto, bahati mbaya sikuchukua mawasiliano ya mtu yeyote.

Wiki 2 baadaye nilipopita eneo lile, nilisimama kuulizia yule mtoto aliyegongwa na pikipiki alikuwa anaishi wapi. wakanionesha nyumba, lakini hawakuniambia kuwa alifariki. Kumbe haikuwa mbali na pale, nikaoneshwa, hatua kama 30 tu toka barabarani. Mama yake mzazi alikuwa ameketi nje. Nikamsalimia, nikamwuliza yule mama, mtoto anaendeleaje, ndipo akanikumbuka, mara akaanza kulia, akaniambia, "Baba, ulipoondoka, ilipita kama nusu saa tu, mtoto akafariki. Nilikuwa na mtoto huyo tu". Machozi yalinitoka, mpaka leo nikipita pale Singida, eneo lile, kumbukumbu mbaya ile haikosi kunijia.

Mwezi huo huo, siku moja nilimpigia rafiki wa siku nyingi, nilitaka nimpe kazi fulani, akanijibu kuwa yupo msibani Ifakara, kumzika Kaka yake aliyegongwa na pikipiki mjini Dar es Salaam.

Siku nyingine, nimetoka Dodoma, naelekea Kahama, nikawa nimekubaliana na jamaa mmoja, kuwa nipitie Tabora kwa mazungumzo ya kikazi. Nikiwa nimefika Itigi, akanipigia simu kuwa haitawezekana kukutana kwa sababu Dada yake amegongwa na pikipiki, amefariki Dunia.

Nikiwa Dar es Salaam, nilipigiwa simu na Admin Manager, kuwa mfanyakazi wetu mmoja, mama yake mzazi amegongwa na pikipiki hujo Njombe, amevunjika vibaya sehemu mbalimbali. Baadaye nilitumiwa picha za majeruhi, ni ngumu kuamini kuwa ni ajali ya pikipiki, mpaka leo hii, hajaweza kutembea, na hana fahamu kwa sababu ya damage ya kichwa.

Kazini tuliamua kuwapa mikopo wafanyakazi wetu. Baadhi waliamua kununua pikipiki. Naambiwa jioni wakitoka kazini waliamua kuzitumia pikipiki zao kubebea abiria. Mmoja aligonga nguzo ya umeme, alitaka kulipita gari kwa upande wa kushoto, gari aliyotaka kuipita ilikuwa inapishana na gari nyingine kwenye barabara za mtaani, akafariki palepale.

Mwingine alianguka baada ya kugonga pavement ya barabara, akafariki.

Mtu mmoja, kaka yake, mama mmoja niliyekuwa nafahamiana naye sana, akiwa amesimama pembeni ya barabara, aligongwa na pikipiki, naye kwenda kugongesha kichwa kwenye barabara Shinyanga mjini, karibu na daraja la kuelekea Mwanza, alifariki palepale. Nilihudhuria maziko yake.

Mjini Mwanza, nililetewa taarifa kuwa mtoto wa shule amegongwa na pikipiki akiwa anavuka barabara, ikanilazimu kuhudhuria msiba kwa sababu mmoja wa ndugu wa marehemu ni mfanyakazi wetu.

Nimeyataja matukio haya kuonesha ukubwa wa tatizo lililopo. Mimi ni mmoja, nimeshuhudia haya, ni mangapi ambayo yanaendelea kutokea, ambayo sikupata kuyasikia?

Serikali imekuwa kama mzazi ambaye anaogopa kumpokonya mtoto mdogo anayechezea kisu kwa hofu kuwa akimpokonya atalia, huku akimweka mtoto wake kwenye hatari. Mzazi wa namna hiyo ni mjinga, mnafiki, na ni muuaji kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kama mzazi.

Leo hii, waendesha pikipiki, hawafuati sheria yoyote ya barabarani.

Hawasimami kwenye taa inapotakiwa kusimama, hawasimami kwenye vivuko vya waenda kwa miguu hata kama watu wanavuka, wana-overtake upande wowote wanaoutaka, hawafuati speed limits, wanabeba mizigo hata isiyoendana na uwezo wa pikipiki (fikiria pikipiki inabeba mbao)! Hii ni nchi ya namna gani?

Ukiuliza ni kwa nini wameachwa hivi, Polisi wanasema kuwa Serikali imewazuia wasibughudhiwe, kwa kuwa waendesha pikipiki ni wengi, wataichukia Serikali, na kisha kuinyima CCM kura. Jambo la ajabu sana. Hivi kuwaachia hawa waende tu ovyo barabarani, hiyo Serikali haioni inawaweka kwenye hatari ya kifo waendesha pikipiki wenyewe, abiria wanaowabeba na waenda kwa miguu?

Serikali, ina maana ipo tayari wananchi waendelee kufa na wengine kuwa vilema, lakini wao wapate tu kura? Huu ni unafiki wa hali ya juu.

Nimeenda baadhi ya nchi, moja ya nchi ambazo nilivutiwa sana na uendeshaji pikipiki ni Burkina Faso. Pikipiki zinafuata sheria zote, kama yalivyo magari. Kwa nini hatupendi kuiga mambo mazuri kama hayo?

Kujifanya watu wema, kwa waendesha pikipiki wavunja sheria, hakuwasaidii wavunja sheria wenyewe, wala raia wengine wote kwa ujumla.

PENDEKEZO
1) Waendesha pikipiki wote (hasa za biashara), wapewe mafunzo kwa awamu kwa gharama ya Serikali. Akishamaliza mafunzo, apewa tag atakayoivaa shingoni. Abiria watahadharishwe kutopanda pikipiki ya waendeshaji wasio na tag.

2) Waendesha pikipiki za biashara wote, wapewe miezi 3, kila mmoja awe amehudhuria mafunzo na kupewa tag. Baada ya kipindi hicho kwisha, kusiruhusuwe mwendesha pikipiki asiye na mafunzo na tag, kuonekana na pikipiki barabarani.

3) Mwenye tag, akivunja sheria, anyang'anywe tag, azuiwe kuendesha, aende mafunzoni tena, kisha apewe tag nyingine.

Jukumu la msingi la Serikali yoyote Duniani ni usalama wa watu wake. Serikali ikishindwa kwenye hili, inakuwa haina uhalali wa kendelea kuwepo.

Nchini mwetu, siasa za unafiki, uwongo na hila, mara nyingi zimelididimiza na zinaendelea kuliangamiza Taifa letu, kila awamu yake, kwa viwango tofauti, kutegemeana na kiongozi mkuu wa nchi ni mtu wa namna gani.

Ni vema kwenye katiba mpya, iwekwe wazi katika kyzuia uongozi wa unafiki unaohatarisha usalama wa wananchi.
 
Boda boda wanachonikera zaidi ni hii tabia ya kuovertake upande wowote yaan yeye atakapoona upenyo tu anaovertake haijalishi ni kulia au kushoto

Afu mwingine ambae sio boda boda akifanya makosa barabarani huwa wanawaka sana lakin wao ndo wakosaji wakubwa,mtu anaovertake hata hajilizisha usalama uliopo mbele
 
Uko sahihi,Pikipiki ni majanga sana kwa nchi hii, mimi mpaka sasa nimeshapata ajali zaidi ya saba na zote wananisababishia boda kwa uzembe wao,nikiona pikipiki sasa hivi inanikaribia naingia na woga na kuamua tu nimpishe njia, ni bora nipaki apite then niendelee.

Kuna siku siisahau nilikuwa naovertake gari, boda yuko mbele ya ile gari kwa hiyo nilishafanya timing ya kuovertake gari pamoja na boda, nikaona kama ameyumba kutaka kuja upande wangu,nikapiga honi nikiashiria kuwa ninaovertake, akarudi upande wake nikajua kanielewa, nilipokuwa naimaliza ile gari ili nimpite na yeye akakatiza mbele yangu ghafla kuja upande wangu akavuka upande wa pili, yani ilibidi nipark gari nianze kumtafakari,na hapo alikuwa kabeba abiria nyuma...
 
Boda boda wanachonikera zaidi ni hii tabia ya kuovertake upande wowote yaan yeye atakapoona upenyo tu anaovertake haijalishi ni kulia au kushoto

Afu mwingine ambae sio boda boda akifanya makosa barabarani huwa wanawaka sana lakin wao ndo wakosaji wakubwa,mtu anaovertake hata hajilizisha usalama uliopo mbele
Nyie mbona mnatusimanga sana sie bodaboda....yaani hivi vidogo mnashindwa kuvumilia lakini ufisadi mnavulimia. Wacha tunapambana life mzeya
 
Boda boda wanachonikera zaidi ni hii tabia ya kuovertake upande wowote yaan yeye atakapoona upenyo tu anaovertake haijalishi ni kulia au kushoto

Afu mwingine ambae sio boda boda akifanya makosa barabarani huwa wanawaka sana lakin wao ndo wakosaji wakubwa,mtu anaovertake hata hajilizisha usalama uliopo mbele
Muda mwingi uendeshaji wao ni wa kuhatarisha usalama, hata wa kwao wenyewe. Wana-overtake mpaka kushoto kwako mwenye gari, wakati unapopishana na gari, ikitokea tatizo lolote, ili kuzuia headon collission, mwenye gari ataenda upande wa kushoto kwake, sasa upabde wako wa kushoto wanapita bodaboda!!
 
Leo hii, japo pikipiki zimekuwa ni chombo kinachotegemewa na wengi kwa usafiri lakini kwa upande mwingine zimekuwa janga kwa Taifa. Hazijawa janga kwa Taifa kwa sababu zenyewe ni janga kwa asili yake bali kwa sababu ya unafiki wa Serikali. Kuna wakati Polisi walitaka kudhibiti uendeshaji ovyo wa pikipiki lakini wanasiasa na viongozi wa Serikali wanafiki wakazuia zoezi hilo.

Kwa wakati tofauti, nimeshuhudia vifo vya watoto wawili, watu wazima watatu waenda kwa miguu, waebdesha pikipiki wawili na ulemavu wa mama mmoja, vyote vikiwa vimesababishwa na uendeshaji wa hovyo wa pikipiki.

Kifo cha kwanza kilikuwa cha mtoto wa shule wa kike mjini Singida. Nilitoka Dodoma, naelekea Mwanza, watoto walikuwa wametoka shule, nikawa naendesha gari taratibu kwaajili ya usalama wa watoto, lakini mbele yangu ilkuja pikipiki, uendeshaji wake ni kama wa mtu kichaa, kwa kasi ilipishana na gari langu, nilishangaa. Mara nilisikia kishindo kwa nyuma, nikatizama kwenye side mirror, mwendesha piki akawa tayari amemgonga binti mdogo, wa darasa la 4. Niligeuza haraka gari, nikasaidiana na akina mama wawili walikuwa karibu, tukamkimbiza mtoto hospitali ya mkoa wa Singida. Simanzi ikiwa imenijaa, masikitiko yasiyoelezeka. Sikuondoka, nilitaka nijue maendeleo yake. Baadaye mama mzazi wa mtoto alifika. Baadaye nikaongea na daktari tena, naye akanihakikishia kuwa mtoto amepata fahamu anaendelea vizuri. Nikashusha pumzi nikaondoka. Lakini nilipenda sana nijue maendeleo ya yule mtoto, bahati mbaya sikuchukua mawasiliano ya mtu yeyote.

Wiki 2 baadaye nilipopita eneo lile, nilisimama kuulizia yule mtoto aliyegongwa na pikipiki alikuwa anaishi wapi. wakanionesha nyuma, lakini hawakuniambia kuwa alifariki. Kumbe haikuwa mbali na pale, nikaoneshwa, hatua kama 30 tu toka barabarani. Mama yake mzazi alikuwa ameketi nje. Nikamsalimia, nikamwuliza yule mama, mtoto anaendeleaje, ndipo akanikumbuka, mara akaanza kulia, akaniambia, "Baba, ulipoondoka, ilipita kama nusus saa tu, mtoto akafariki. Nilikuwa na mtoto huyo tu". Machozi yalinitoka, mpaka leo nikipita pale Singida, eneo lile, kumbukumbu mbaya ile haikosi kunijia.

Mwezi huo huo, siku moja nilimpigia rafiki wa siku nyingi, nilitaka nimpe kazi fulani, akanijibu kuwa yupo msibani Ifakara, kumzika Kaka yake aliyegongwa na pikipiki mjini Dar es Salaam.

Siku nyingine, nimetoka Dodoma, naelekea Kahama, nikawa nimekubaliana na jamaa mmmoja, kuwa nipitie Tabora kwa mazungumzo ya kikazi. Nikiwa nimefika Itigi, akanipigia simu kuwa haitawezekana kukutana kwa sababu Dada yake amegongwa na pikipiki, amefariki Dunia.

Nikiwa Dar es Salaam, nilipigiwa simu na Admin Manager, kuwa mfanyakazi wetu mmoja, mama yake mzazi amegongwa na pikipiki hujo Njombe, amevunjika vibaya sehemu mbalimbali. Baadaye nilitumiwa picha za majeruhi, ni ngumu kuamini kuwa ni ajali ya pikipiki, mpaka leo hii, hajaweza kutembea, na hana fahamu kwa sababu ya damage ya kichwa.

Kazini tuliamua kuwapa mikopo wafanyakazi wetu. Baadhi waliamua kununua pikipiki. Naambiwa jioni wakitoka kazini waliamua kuzitumia pikipiki zao kubebea abiria. Mmoja aligonga nguzo ya umeme, alitaka kulipita gari kwa upande wa kushoto, gari aliyotaka kuipita ilikuwa inapishana na gari nyingine kwenye barabara za mtaani, akafariki palepale.

Mwingine alianguka baada ya kugonga pavement ya barabara, akafariki.

Mtu mmoja, kaka yake, mama mmoja niliyekuwa nafahamiana naye sana, akiwa amesimama pembeni ya barabara, aligongwa na pikipiki, naye kwenda kugongesha kichwa kwenye barabara Shinyanga mjini, karibu na daraja la kuelekea Mwanza, alifariki palepale. Nilihudhutia maziko yake.

Mjini Mwanza, nililetewa taarifa kuwa mtoto wa shule amegongwa na pikipiki akiwa anavuka barabara, ikanilazimu kuhudhuria msiba kwa sababu mmoja wa ndugu wa marehemu ni mfanyakazi wetu.

Nimeyataja matukio haya kuonesha ukubwa wa tatizo lililopo. Mimi ni mmoja, nimeshuhufldia haya, ni mangapi ambayo yanaendelea kutokea, ambayo sikupata kuyasikia?

Serikali imekuwa kama mzazi ambaye anaogopa kumpokonya mtoto mdogo anayechezea kisu kwa hofu kuwa akimpokonya atalia, huku akimweka mtoto wake kwenye hatari. Mzaxi wa namna hiyo ni mjinga, mnafiki, na ni muuaji kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kama mzazi.

Leo hii, waendesha pikipiki, hawafuati sheria yoyote ya barabarani. Hawasimami kwenye taa inapotakiwa kusimama, hawasimami kwenye vivuko vya waenda kwa miguu hata kama watu wanavuka, wana-overtake upande wowote wanaoutaka, hawafuati speed limits, wanabeba mizigo hata isiyoendana na uwezo wa pikipiki (fikiria pikipiki inabeba mbao)! Hii ni nchi ya namna gani?

Ukiuliza ni kwa nini wameachwa hivi, Polisi wanasema kuwa Serikali imewazuia wasibughudhiwe, kwa kuwa waendesha pikipiki ni wengi, wataichukia Serikali, na kisha kuinyima CCM kura. Jambo la ajabu sana. Hivi kuwaachia hawa waende tu hovyo barabarani, hiyo Serikali haioni inawaweka kwenye hatari ya kifo waendesha pikipiki wenyewe, abiria wanaowabeba na waenda kwa miguu? Serikali, ina maana ipo tayari wananchi waendelee kufa na wengine kuwa vilema, lakini wao wapate tu kura? Huu ni unafiki wa hali ya juu.

Nimeenda baadhi ya nchi, moja ya nchi ambazo nilivutiwa sana na uendeshaji pikipiki ni Burkina Faso. Pikipiki zinafuata sheria zote, kama yalivyo magari. Kwa nini hatupendi kuiga mambo mazuri kama hayo?

Kujifanya watu wema, kwa waendesha pikipiki wavunja sheria, hakuwasaidii wavunja sheria wenyewe, wala raia wengine wote kwa ujumla.

PENDEKEZO

1) Waendesha pikipiki wote (hasa za biashara), wapewe mafunzo kwa awamu kwa gharama ya Serikali. Akishamaliza mafunzo, apewa tag atakayoivaa shingoni. Abiria watahadharishwe kutopanda pikipiki ya waendeshaji wasio na tag.

2) Waendesha pikipiki za biashara wote, wapewe miezi 3, kila mmoja awe amehudhuria mafunzo na kupewa tag. Baada ya kipindi hicho kwisha, kusiruhusuwe mwendesha pikipiki asiye na mafunzo na tag, kuonekana na pikipiki barabarani.

3) Mwenye tag, akivunja sheria, anyang'anywe tag, azuiwe kuendesha, aende mafunzoni tena, kisha apewe tag nyingine.

Jukumu la msingi la Serikali yoyote Duniani ni usalamawa watu wake. Serikali ikishindwa kwenye hili, inakuwa haina uhalali wa kendelea kuwepo.

Nchini mwetu, siasa za unafiki, uwongo na hila, mara nyingi zimelididimiza na zinaendelea kuliangamiza Taifa letu, kila awamu yake, kwa viwango tofauti, kutegemeana na kiongozi mkuu wa nchi ni mtu wa namna gani.

Ni vema kwenye katiba mpya, iwekwe wazi katika kyzuia uongozi wa unafiki unaohatarisha usalama wa wananchi.
Huku kwetu ndani ya wiki mbili wamefariki dereva wawili.. mmoja alikuwa ni mwanangu sanaa bado ni ngumu kuamini kama jamaa ndo hatorudi tena

Kweli Dunia tunapita..
 
Uko sahihi Pikipiki ni majanga sana,kwa nchi hii,mimi mpaka sasa nimeshapata ajali zaidi ya saba na zote wananisababishia boda kwa uzembe wao,nikiona pikipiki sasa hivi inanikaribia naingia na woga nakuamua tu nimpishe njia,ni bora nipaki apite then niendelee.Kuna siku siisahau,nilikuwa naovertake gari,boda yuko mbele ya ile gari kwa hiyo nilishafanya timing ya kuovertake gari pamoja na boda,nikaona kama ameyumba kutaka kurudi barabarani nikapiga honi nikiashiria kuwa ninaovertake,akarudi upande wake nikajua kanielewa,nilipokuwa naimaliza ile gari ili nimpite na yeye akakatiza mbele yangu ghafla kuja upande wangu akavuka upande wa pili,yani ilibidi ni park gari nianze kumtafakari,na hapo alikuwa kabeba abiria nyuma...
Yaani waendesha boda boda, ni kama maisha yao wameyakabidhi kwa watu wengine wawatunzie. Wao wanaona hawana wajibu wa kutunza maisha yao wala ya watu wengine, including abiria wao.
 
Leo hii, japo pikipiki zimekuwa ni chombo kinachotegemewa na wengi kwa usafiri lakini kwa upande mwingine zimekuwa janga kwa Taifa. Hazijawa janga kwa Taifa kwa sababu zenyewe ni janga kwa asili yake bali kwa sababu ya unafiki wa Serikali. Kuna wakati Polisi walitaka kudhibiti uendeshaji ovyo wa pikipiki lakini wanasiasa na viongozi wa Serikali wanafiki wakazuia zoezi hilo.

Kwa wakati tofauti, nimeshuhudia vifo vya watoto wawili, watu wazima watatu waenda kwa miguu, waebdesha pikipiki wawili na ulemavu wa mama mmoja, vyote vikiwa vimesababishwa na uendeshaji wa hovyo wa pikipiki.

Kifo cha kwanza kilikuwa cha mtoto wa shule wa kike mjini Singida. Nilitoka Dodoma, naelekea Mwanza, watoto walikuwa wametoka shule, nikawa naendesha gari taratibu kwaajili ya usalama wa watoto, lakini mbele yangu ilkuja pikipiki, uendeshaji wake ni kama wa mtu kichaa, kwa kasi ilipishana na gari langu, nilishangaa. Mara nilisikia kishindo kwa nyuma, nikatizama kwenye side mirror, mwendesha piki akawa tayari amemgonga binti mdogo, wa darasa la 4. Niligeuza haraka gari, nikasaidiana na akina mama wawili walikuwa karibu, tukamkimbiza mtoto hospitali ya mkoa wa Singida. Simanzi ikiwa imenijaa, masikitiko yasiyoelezeka. Sikuondoka, nilitaka nijue maendeleo yake. Baadaye mama mzazi wa mtoto alifika. Baadaye nikaongea na daktari tena, naye akanihakikishia kuwa mtoto amepata fahamu anaendelea vizuri. Nikashusha pumzi nikaondoka. Lakini nilipenda sana nijue maendeleo ya yule mtoto, bahati mbaya sikuchukua mawasiliano ya mtu yeyote.

Wiki 2 baadaye nilipopita eneo lile, nilisimama kuulizia yule mtoto aliyegongwa na pikipiki alikuwa anaishi wapi. wakanionesha nyuma, lakini hawakuniambia kuwa alifariki. Kumbe haikuwa mbali na pale, nikaoneshwa, hatua kama 30 tu toka barabarani. Mama yake mzazi alikuwa ameketi nje. Nikamsalimia, nikamwuliza yule mama, mtoto anaendeleaje, ndipo akanikumbuka, mara akaanza kulia, akaniambia, "Baba, ulipoondoka, ilipita kama nusus saa tu, mtoto akafariki. Nilikuwa na mtoto huyo tu". Machozi yalinitoka, mpaka leo nikipita pale Singida, eneo lile, kumbukumbu mbaya ile haikosi kunijia.

Mwezi huo huo, siku moja nilimpigia rafiki wa siku nyingi, nilitaka nimpe kazi fulani, akanijibu kuwa yupo msibani Ifakara, kumzika Kaka yake aliyegongwa na pikipiki mjini Dar es Salaam.

Siku nyingine, nimetoka Dodoma, naelekea Kahama, nikawa nimekubaliana na jamaa mmmoja, kuwa nipitie Tabora kwa mazungumzo ya kikazi. Nikiwa nimefika Itigi, akanipigia simu kuwa haitawezekana kukutana kwa sababu Dada yake amegongwa na pikipiki, amefariki Dunia.

Nikiwa Dar es Salaam, nilipigiwa simu na Admin Manager, kuwa mfanyakazi wetu mmoja, mama yake mzazi amegongwa na pikipiki hujo Njombe, amevunjika vibaya sehemu mbalimbali. Baadaye nilitumiwa picha za majeruhi, ni ngumu kuamini kuwa ni ajali ya pikipiki, mpaka leo hii, hajaweza kutembea, na hana fahamu kwa sababu ya damage ya kichwa.

Kazini tuliamua kuwapa mikopo wafanyakazi wetu. Baadhi waliamua kununua pikipiki. Naambiwa jioni wakitoka kazini waliamua kuzitumia pikipiki zao kubebea abiria. Mmoja aligonga nguzo ya umeme, alitaka kulipita gari kwa upande wa kushoto, gari aliyotaka kuipita ilikuwa inapishana na gari nyingine kwenye barabara za mtaani, akafariki palepale.

Mwingine alianguka baada ya kugonga pavement ya barabara, akafariki.

Mtu mmoja, kaka yake, mama mmoja niliyekuwa nafahamiana naye sana, akiwa amesimama pembeni ya barabara, aligongwa na pikipiki, naye kwenda kugongesha kichwa kwenye barabara Shinyanga mjini, karibu na daraja la kuelekea Mwanza, alifariki palepale. Nilihudhutia maziko yake.

Mjini Mwanza, nililetewa taarifa kuwa mtoto wa shule amegongwa na pikipiki akiwa anavuka barabara, ikanilazimu kuhudhuria msiba kwa sababu mmoja wa ndugu wa marehemu ni mfanyakazi wetu.

Nimeyataja matukio haya kuonesha ukubwa wa tatizo lililopo. Mimi ni mmoja, nimeshuhufldia haya, ni mangapi ambayo yanaendelea kutokea, ambayo sikupata kuyasikia?

Serikali imekuwa kama mzazi ambaye anaogopa kumpokonya mtoto mdogo anayechezea kisu kwa hofu kuwa akimpokonya atalia, huku akimweka mtoto wake kwenye hatari. Mzaxi wa namna hiyo ni mjinga, mnafiki, na ni muuaji kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kama mzazi.

Leo hii, waendesha pikipiki, hawafuati sheria yoyote ya barabarani. Hawasimami kwenye taa inapotakiwa kusimama, hawasimami kwenye vivuko vya waenda kwa miguu hata kama watu wanavuka, wana-overtake upande wowote wanaoutaka, hawafuati speed limits, wanabeba mizigo hata isiyoendana na uwezo wa pikipiki (fikiria pikipiki inabeba mbao)! Hii ni nchi ya namna gani?

Ukiuliza ni kwa nini wameachwa hivi, Polisi wanasema kuwa Serikali imewazuia wasibughudhiwe, kwa kuwa waendesha pikipiki ni wengi, wataichukia Serikali, na kisha kuinyima CCM kura. Jambo la ajabu sana. Hivi kuwaachia hawa waende tu hovyo barabarani, hiyo Serikali haioni inawaweka kwenye hatari ya kifo waendesha pikipiki wenyewe, abiria wanaowabeba na waenda kwa miguu? Serikali, ina maana ipo tayari wananchi waendelee kufa na wengine kuwa vilema, lakini wao wapate tu kura? Huu ni unafiki wa hali ya juu.

Nimeenda baadhi ya nchi, moja ya nchi ambazo nilivutiwa sana na uendeshaji pikipiki ni Burkina Faso. Pikipiki zinafuata sheria zote, kama yalivyo magari. Kwa nini hatupendi kuiga mambo mazuri kama hayo?

Kujifanya watu wema, kwa waendesha pikipiki wavunja sheria, hakuwasaidii wavunja sheria wenyewe, wala raia wengine wote kwa ujumla.

PENDEKEZO

1) Waendesha pikipiki wote (hasa za biashara), wapewe mafunzo kwa awamu kwa gharama ya Serikali. Akishamaliza mafunzo, apewa tag atakayoivaa shingoni. Abiria watahadharishwe kutopanda pikipiki ya waendeshaji wasio na tag.

2) Waendesha pikipiki za biashara wote, wapewe miezi 3, kila mmoja awe amehudhuria mafunzo na kupewa tag. Baada ya kipindi hicho kwisha, kusiruhusuwe mwendesha pikipiki asiye na mafunzo na tag, kuonekana na pikipiki barabarani.

3) Mwenye tag, akivunja sheria, anyang'anywe tag, azuiwe kuendesha, aende mafunzoni tena, kisha apewe tag nyingine.

Jukumu la msingi la Serikali yoyote Duniani ni usalamawa watu wake. Serikali ikishindwa kwenye hili, inakuwa haina uhalali wa kendelea kuwepo.

Nchini mwetu, siasa za unafiki, uwongo na hila, mara nyingi zimelididimiza na zinaendelea kuliangamiza Taifa letu, kila awamu yake, kwa viwango tofauti, kutegemeana na kiongozi mkuu wa nchi ni mtu wa namna gani.

Ni vema kwenye katiba mpya, iwekwe wazi katika kyzuia uongozi wa unafiki unaohatarisha usalama wa wananchi.
CCM na serikali wameshindwa kujenga viwanda na kufufua mashamba iliyoyaua ili vijana wakafanye kazi huko kwahiyo wameleta ajira mbadala ya bodaboda ambazo nyingine wanawapa vijana wakafilie mbali.
 
Leo hii, japo pikipiki zimekuwa ni chombo kinachotegemewa na wengi kwa usafiri lakini kwa upande mwingine zimekuwa janga kwa Taifa. Hazijawa janga kwa Taifa kwa sababu zenyewe ni janga kwa asili yake bali kwa sababu ya unafiki wa Serikali.

Kuna wakati Polisi walitaka kudhibiti uendeshaji ovyo wa pikipiki lakini wanasiasa na viongozi wa Serikali wanafiki wakazuia zoezi hilo.

Kwa wakati tofauti, nimeshuhudia vifo vya watoto wawili, watu wazima watatu waenda kwa miguu, waebdesha pikipiki wawili na ulemavu wa mama mmoja, vyote vikiwa vimesababishwa na uendeshaji wa ovyo wa pikipiki.

Kifo cha kwanza kilikuwa cha mtoto wa shule wa kike mjini Singida. Nilitoka Dodoma, naelekea Mwanza, watoto walikuwa wametoka shule, nikawa naendesha gari taratibu kwaajili ya usalama wa watoto, lakini mbele yangu ilkuja pikipiki, uendeshaji wake ni kama wa mtu kichaa, kwa kasi ilipishana na gari langu, nilishangaa. Mara nilisikia kishindo kwa nyuma, nikatizama kwenye side mirror, mwendesha pikipiki akawa tayari amemgonga binti mdogo, wa darasa la 4. Niligeuza haraka gari, nikasaidiana na akina mama wawili walikuwa karibu, tukamkimbiza mtoto hospitali ya mkoa wa Singida. Simanzi ikiwa imenijaa, masikitiko yasiyoelezeka. Sikuondoka, nilitaka nijue maendeleo yake. Baadaye mama mzazi wa mtoto alifika. Baadaye nikaongea na daktari tena, naye akanihakikishia kuwa mtoto amepata fahamu anaendelea vizuri. Nikashusha pumzi nikaondoka. Lakini nilipenda sana nijue maendeleo ya yule mtoto, bahati mbaya sikuchukua mawasiliano ya mtu yeyote.

Wiki 2 baadaye nilipopita eneo lile, nilisimama kuulizia yule mtoto aliyegongwa na pikipiki alikuwa anaishi wapi. wakanionesha nyumba, lakini hawakuniambia kuwa alifariki. Kumbe haikuwa mbali na pale, nikaoneshwa, hatua kama 30 tu toka barabarani. Mama yake mzazi alikuwa ameketi nje. Nikamsalimia, nikamwuliza yule mama, mtoto anaendeleaje, ndipo akanikumbuka, mara akaanza kulia, akaniambia, "Baba, ulipoondoka, ilipita kama nusu saa tu, mtoto akafariki. Nilikuwa na mtoto huyo tu". Machozi yalinitoka, mpaka leo nikipita pale Singida, eneo lile, kumbukumbu mbaya ile haikosi kunijia.

Mwezi huo huo, siku moja nilimpigia rafiki wa siku nyingi, nilitaka nimpe kazi fulani, akanijibu kuwa yupo msibani Ifakara, kumzika Kaka yake aliyegongwa na pikipiki mjini Dar es Salaam.

Siku nyingine, nimetoka Dodoma, naelekea Kahama, nikawa nimekubaliana na jamaa mmoja, kuwa nipitie Tabora kwa mazungumzo ya kikazi. Nikiwa nimefika Itigi, akanipigia simu kuwa haitawezekana kukutana kwa sababu Dada yake amegongwa na pikipiki, amefariki Dunia.

Nikiwa Dar es Salaam, nilipigiwa simu na Admin Manager, kuwa mfanyakazi wetu mmoja, mama yake mzazi amegongwa na pikipiki hujo Njombe, amevunjika vibaya sehemu mbalimbali. Baadaye nilitumiwa picha za majeruhi, ni ngumu kuamini kuwa ni ajali ya pikipiki, mpaka leo hii, hajaweza kutembea, na hana fahamu kwa sababu ya damage ya kichwa.

Kazini tuliamua kuwapa mikopo wafanyakazi wetu. Baadhi waliamua kununua pikipiki. Naambiwa jioni wakitoka kazini waliamua kuzitumia pikipiki zao kubebea abiria. Mmoja aligonga nguzo ya umeme, alitaka kulipita gari kwa upande wa kushoto, gari aliyotaka kuipita ilikuwa inapishana na gari nyingine kwenye barabara za mtaani, akafariki palepale.

Mwingine alianguka baada ya kugonga pavement ya barabara, akafariki.

Mtu mmoja, kaka yake, mama mmoja niliyekuwa nafahamiana naye sana, akiwa amesimama pembeni ya barabara, aligongwa na pikipiki, naye kwenda kugongesha kichwa kwenye barabara Shinyanga mjini, karibu na daraja la kuelekea Mwanza, alifariki palepale. Nilihudhuria maziko yake.

Mjini Mwanza, nililetewa taarifa kuwa mtoto wa shule amegongwa na pikipiki akiwa anavuka barabara, ikanilazimu kuhudhuria msiba kwa sababu mmoja wa ndugu wa marehemu ni mfanyakazi wetu.

Nimeyataja matukio haya kuonesha ukubwa wa tatizo lililopo. Mimi ni mmoja, nimeshuhudia haya, ni mangapi ambayo yanaendelea kutokea, ambayo sikupata kuyasikia?

Serikali imekuwa kama mzazi ambaye anaogopa kumpokonya mtoto mdogo anayechezea kisu kwa hofu kuwa akimpokonya atalia, huku akimweka mtoto wake kwenye hatari. Mzazi wa namna hiyo ni mjinga, mnafiki, na ni muuaji kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kama mzazi.

Leo hii, waendesha pikipiki, hawafuati sheria yoyote ya barabarani.

Hawasimami kwenye taa inapotakiwa kusimama, hawasimami kwenye vivuko vya waenda kwa miguu hata kama watu wanavuka, wana-overtake upande wowote wanaoutaka, hawafuati speed limits, wanabeba mizigo hata isiyoendana na uwezo wa pikipiki (fikiria pikipiki inabeba mbao)! Hii ni nchi ya namna gani?

Ukiuliza ni kwa nini wameachwa hivi, Polisi wanasema kuwa Serikali imewazuia wasibughudhiwe, kwa kuwa waendesha pikipiki ni wengi, wataichukia Serikali, na kisha kuinyima CCM kura. Jambo la ajabu sana. Hivi kuwaachia hawa waende tu ovyo barabarani, hiyo Serikali haioni inawaweka kwenye hatari ya kifo waendesha pikipiki wenyewe, abiria wanaowabeba na waenda kwa miguu?

Serikali, ina maana ipo tayari wananchi waendelee kufa na wengine kuwa vilema, lakini wao wapate tu kura? Huu ni unafiki wa hali ya juu.

Nimeenda baadhi ya nchi, moja ya nchi ambazo nilivutiwa sana na uendeshaji pikipiki ni Burkina Faso. Pikipiki zinafuata sheria zote, kama yalivyo magari. Kwa nini hatupendi kuiga mambo mazuri kama hayo?

Kujifanya watu wema, kwa waendesha pikipiki wavunja sheria, hakuwasaidii wavunja sheria wenyewe, wala raia wengine wote kwa ujumla.

PENDEKEZO
1) Waendesha pikipiki wote (hasa za biashara), wapewe mafunzo kwa awamu kwa gharama ya Serikali. Akishamaliza mafunzo, apewa tag atakayoivaa shingoni. Abiria watahadharishwe kutopanda pikipiki ya waendeshaji wasio na tag.

2) Waendesha pikipiki za biashara wote, wapewe miezi 3, kila mmoja awe amehudhuria mafunzo na kupewa tag. Baada ya kipindi hicho kwisha, kusiruhusuwe mwendesha pikipiki asiye na mafunzo na tag, kuonekana na pikipiki barabarani.

3) Mwenye tag, akivunja sheria, anyang'anywe tag, azuiwe kuendesha, aende mafunzoni tena, kisha apewe tag nyingine.

Jukumu la msingi la Serikali yoyote Duniani ni usalama wa watu wake. Serikali ikishindwa kwenye hili, inakuwa haina uhalali wa kendelea kuwepo.

Nchini mwetu, siasa za unafiki, uwongo na hila, mara nyingi zimelididimiza na zinaendelea kuliangamiza Taifa letu, kila awamu yake, kwa viwango tofauti, kutegemeana na kiongozi mkuu wa nchi ni mtu wa namna gani.

Ni vema kwenye katiba mpya, iwekwe wazi katika kyzuia uongozi wa unafiki unaohatarisha usalama wa wananchi.
Hivyo vifo vinaitwa "gharama za maendeleo".
 
Bunduki au sumu,visu ,hazijawahi kuwa tatizo,tatizo ni mtumiaji..
 
Bodaboda imekuwa chanzo kikuu cha ajira kwa vijana.... kijana akimaliza darasa la saba ama form four wazo la nalo ki maisha maisha ni kujiajili kama Bodaboda, Bajaji ama uchuuzi wa barabarani.

Mazingira ya kufanya kilimo kwa Vijana Tanzania ni magumu, maisha ya vijijini ni magumu kwa hiyo vijana wote wanasongamana mijini kufanya uchuuzi na kuwa mabodaboda.

Tuna kazi nzito mbele yetu kama taifa, tuwe makini. Watunge Sera za Taifa hebu kigeukieni kilimo ili hawa vijana wapate ajira za uhakika wa kesho yao.
 
Boda boda wafe tu!
Polisi wamewachoka, nasi tumewachoka!
Wanapendwa na Makala tu hapa Darisalama.
 
Ni kama.vile wqmeruhusiwa kuvunja sheria tu. Yaani mbele ya urafiki wanavuta taa nyekundu???
 
Back
Top Bottom