Rais Samia: Tanzania itafanya demokrasia kuendana na mila na tamaduni zetu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizundua miradi ya maendeleo mkoani Mtwara, leo tarehe 15 Septemba, 2023.


Rais Samia amesema Tanzania itafanya demokrasia kuendana na mila na tamaduni zetu, demokrasia ni utawala unaojali haki za watu. Tusiharibu amani na utulivu, hasa mwakani tunapoanza uchaguzi wa na Serikali za mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu mwaka 2025.

Hakuna haja ya kuwa na ugomvi majimboni, kila aliyefanya kazi yake vizuri wananchi wamemuona, watamrudisha. Tufanye demokrasia vizuri bila kuvunja mila na desturi zetu.

Aidha, Rais Samia amesema wananchi wasibaguliwe kwa kuwa demokrasia ina lengo la kukuza maendeleo na sio kudumaza maendeleo.

Amewaomba watu wa Mtwara kuchangamkia fursa za maendeleo zinazokuja ili wapate kujiajiri au kuajiriwa ili usitawi wa hali zao ukue.

Mkoa wa Mtwara umekuwa na matukio mengi ya vifo na migogoro kati ya wafugaji na wakulima, amewaomba viongozi wa mkoa huo kutazama jambo hili kwa umakini.
 
Back
Top Bottom