Rais Samia Suluhu Hassan ashiriki mkutano mkuu maalum wa uchaguzi wa viongozi wa jumuiya ya tawala za mitaa Tanzania - ALAT

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,831
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Samia suluhu hassan akishiriki mkutano mkuu maalum wa uchaguzi wa viongozi wa jumuiya ya tawala za mitaa tanzania - ALAT katika ukumbi wa Jakaya Kikwete convention center jijini Dodoma, tarehe 27 Septemba, 2021. Kuwa nami kukujuza yanayojiri.

===========

Rais Samia Suluhu: Mkutano huu ni wa kwanza kufanyika tangu kumalizika uchaguzi wa 2020, kwa msingi huo napenda kutumia fursa hii kuwapongeza madiwani wote nchini kwa kupewa imani na wananchi

=> Kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha, Serikali imeridhia madiwani waaze kulipwa posho ya kila mwezi na hii itasaidia madiwani kuacha kuhangaika na vile vijifedha vinavyokusanywa kule kujilipa kwenye maposho.

=> Kile ambacho mtakiacha tutataka kikatumike katika kazi za maendeleo na sio vinginevyo

=> Maagizo yangu kwa ALAT inayokuja ni kutumia mifumo ya mitandao katika kufanya kazi zenu, kazi za tawala za mikoa katika ukusanyaji wa mapato, matumizi na hata kutoa huduma hasa kwenye mambo ya Ardhi.

=> Kuna migogoro mikubwa ya ardhi na kwasababu takwimu au rekodi haziko sawa

=> Juzi nilikuwa namuona waziri mkuu sijui alikwenda wapi, alienda akapelekwa kwenye kakibanda ambacho kinaambiwa kimejengwa kwa mamilioni kadhaa lakini ukikitazama kile kibanda na milioni zilizotajwa ni tofauti, kimepakwa rangi vizuri mbele lakini ni kibanda kingejengwa ka milioni tatu au nne lakini mamilioni kadhaa yamemiminika pale.

----

ALIYOSEMA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE . SAMIA SULUHU HASSAN WAKATI AKIFUNGUA MKUTANO MKUU MAALUM WA ALAT SEPTEMBA 27, 2021 JIJINI DODOMA

#Nawaomba Wizara ya Afya mzidi kutoa elimu kwa wananchi kuhusu suala la UVIKO-19, watu wakubali kuchanja kwa hiari ili tupunguze vifo vinavyotokana na ugonjwa huu.

#Baadhi ya viongozi ni sehemu ya kero za wananchi, nendeni mkajitathmini na mkajirekebishe kwa sababu tumewapeleka mkaongoze katika maeneo hayo na mkawatumikie wananchi na sio kuwa miungu kwa wananchi.

#Wakati nimeingia nimekuta Tarafa takriban 250 hazina Vituo vya Afya, nawaahidi Tarafa zote zitajengewa vituo hivyo pia tutamaliza kujenga madarasa yote yanayotakiwa nchi nzima.

#Naomba ALAT mkasimamie 10% inayotolewa na Halmashauri zetu, naomba Halmashauri zianze kutoa fedha hizo kwa vikundi vikubwa kwenye miradi mikubwa ambayo manufaa yake yataonekana kuliko kutoa fedha kidogo kidogo kwasababu itaua mfuko huo kwa maslahi binafsi.

#Bado kuna shida kwenye thamani ya fedha kwa miradi mnayoitekeleza, fedha nyingi zinakuja kwenu lakini miradi haifanani na fedha zinazotolewa, pamoja na kwamba tutaendelea kuleta fedha naagiza thamani ya fedha katika miradi tunayoitekeleza ionekane.

#Nasisitiza kusimamia makusanyo na matumizi katika halmashauri zetu, Serikali za Mitaa wamekuwa watumizi wazuri wa fedha, ningependa kuona ALAT na uongozi wa TAMISEMI mnayasimamia haya.

#Nawaagiza kutumia mifumo ya mitandao katika kufanya kazi zenu za ukusanyaji wa mapato, matumizi na kwenye kutoa huduma. Muweke rekodi za huduma zinazotolewa hasa zinazowahusu wananchi ikiwemo masuala ya ardhi

#Tutaendelea kuleta wataalam wa kada mbalimbali na kuwajengea uwezo pia kwa kadri uwezo wa Serikali utakavyokuwa ukiongezeka tutaendelea kuangalia maslahi ya Madiwani na watendaji wengine kwenye Halmashauri zetu .

#TAMISEMI imetengewa TSH Trilioni 7.3 takriban 20% ya bajeti nzima (2021/22), naahidi kuwa Serikali itaendeleza ushirikiano na Mamlaka za Serikali za Mitaa hasa kwa kupeleka fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo na kuboresha huduma za jamii.

#Naishukuru Serikali kwa kuwezesha miradi mingi ya maendeleo katika sekta mbalimbali, tangu umeingia madarakani Halmashauri zetu zimeshapokea TSH Bilioni 298 kwa ajili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo - Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu.

#Nimepita katika baadhi ya Halmashauri na Madiwani wanakushukuru sana kwa uamuzi wako wa kulipa posho za kila mwezi kutoka Serikali Kuu kwani umethamini kazi za Madiwani - Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu.

#Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaongozwa na Kanuni za kudumu za mkutano na uongozi za 2008, uchaguzi hufanyika mara tu baada ya kuchaguliwa kwa viongozi ngazi za chini na kuundwa kwa Mabaraza ya Halmashauri - Katibu Mkuu ALAT, Elirehema Kaaya.

Imeandaliwa na Idara ya Habari - MAELEZO

BAADHI YENU HAMUHESHIMIANI,HAMSIKILIZANI,NENDENI MKAHESHIMIANE -RAIS SAMIA

"Kuna baadhi yenu hamuheshimiani, hamusikilizani nendeni mkaheshimiane, DC anasema hili DAS wake anasema hili, DED anasema hili mwingine anasema hili mnavutana, sioni kwanini mnavutana lakini kuna sababu"

"Moja fedha zinapoingia kila Mtu anataka amege fungu atie mfukoni mmoja akikataa mivutano inaanza, pili mwingine akisimamia Sheria mnavutana"

"Nilishasema sitokaa kufoka sijaumbwa hivyo, msitegemee nitamuita fulani na fulani njoo kwanini mnafanya hivyo!? nitaongea kwa kalamu , namwambia tu Waziri huyu hanifai tunaweka mwingine, kuna Watu wengi wanataka hizo nafasi” ——— Rais Samia leo Dodoma.

"Najua kuna wanaonitazama nilivyo na wakasema 'huyu Mama hamna kitu huyu' , najua nilisema ndani ya miezi 6 nilikuwa nawasoma na nyinyi mmenisoma, kwahiyo sasa tumesomana kazi iendelee, najua wote ni Watu wazima, najua wote ni Watu wazima mnayajua mazuri na mabaya mkifanya mnafanya makusudi, sitofoka, nitaongea kwa kalamu"

"Katika Mkutano mmoja nilisema sitaki mabango yenye masikitiko, mabango ya shukrani acha yaandikwe lakini mabango ya masikitiko ni kwasababu Viongozi hamfanyi wajibu wenu, nendeni mkajitathmini, haujaenda kule kuwa Mungu wa Wananchi umeenda kutumikia Wananchi na sio kuwatesa Wananchi"

KUNA KERO NYINGI KWENYE MIRATHI NA ARDHI NENDENI MKASIMAMIE HATA KAMA ZINAMGUSA MTU UNAYEMJUA SIMAMA KWENYE HAKI - RAIS SAMIA

"Kuna kero nyingi kwenye mirathi na ardhi nendeni mkasimamie, hata kama zinayemgusa ni Mtu unayemjua simama kwenye haki, Duniani tunapita tu utakwenda kuuliza ulipata madaraka uliyafanyia nini!? usiposimama kwenye haki laana inakutafuna kuanzia Duniani hadi kesho kwa Mungu" ——— Rais Samia akizungumza kwenye Ufunguzi wa Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Viongozi wa ALAT - Taifa Dodoma leo.
 
FASQ9VfVIAcNMiO.jpg
 
Tumemsikia, tunasubiri utekelezaji huko ndiko kuna shughuli pevu.
 
"Moja fedha zinapoingia kila Mtu anataka amege fungu atie mfukoni mmoja akikataa mivutano inaanza, pili mwingine akisimamia Sheria mnavutana mmmh shida iko hapa
 
Mh. Rais wetu kanena vema sana sanaa, sisi wananchi wako tunasubiri uwapige kalamu nyekundu watu kibaoo, wako bado vichwa maji na wagumu mnooo, tena wanakusikiliza, wanaelewa, na bado wanajifanyia mambo yao ya ufisadi, uonevu wa wananchi maskini, Miungu watu, wala rushwa hadi rushwa za ngono, Mh. Waziri Ummy kasema jana wako Wakurugenzi wanaume wanagonganisha wanawake huko halmashauri hadi wanawake wanapigana.. Waziri Ummy kasema hayo jana..

Mm nakuomba Mh. Rais hili la Waziri Ummy hadi kasema hivyo anawajua wakurugenzi gani hao, ana majina yao, wapige chini, piga kalamu nyekundu, na watangaze umma ujue, utaona nidhamu itarudi haraka sana huko halmashauri zote. Ukute wanawake wasio toa rushwa ya ngono labda no one wanawasikiliza shida zao.
 
Tumemsikia, tunasubiri utekelezaji huko ndiko kuna shughuli pevu.
Chief Hangaya sio wa mchezo mchezo ,vituo vya afya 250 at once na vyumba vya madarasa 15,000 by January sio jambo dogo.

Kongole sana madam hakuna kudhalilishana ila Kazi inaonekana..

Hapa ni lami za mil.500 kila Jimbo zikiendelea kujengwa km 2.5👇

IMG_20210927_164444_508.jpg

IMG_20210927_164451_373.jpg

IMG_20210927_165108_245.jpg

IMG_20210927_165355_334.jpg

IMG_20210927_165455_637.jpg

IMG_20210927_165730_853.jpg

IMG_20210927_165833_106.jpg
 
Mama amebadilika sana siku za hivi karibuni, hata maelekezo anayoyatoa ni mazito. Kweli hii miezi 6 alikuwa anawasoma.
Yeah, hata mimi nimeona hicho kitu. Leo ameongea vema sana na kwa kujiamini mno. Tena hata hajaonesha unafiki, amesema kabisa 'mimi sio mtu wa kufokafoka kwani sijaumbwa hivyo'. Amewakata ngebe wale waliozoea mikelele na kujisifusifu. Kama yatatekelezeka haya, kwa amani na utulivu kama hivi, nakwambia tutakuja kusimulia hapa. Nakaona kale 'kaushuzi' ka uongozi ka yule jamaa asiyeeleweka km ni mzee au kijana kikipotea taratiiibu.
 
Mama kaamua kupiga kazi, umbea na maneno kawaachia wengine.
 
Mama hataki unafiki na unoko
Mwenye kujipendekeza au kumponda imekula kwake

Naona watu wamepewa ukweli ingawa wengi wao ni sikio la kufa
Hapo Kalamu itatembea tu
 
Back
Top Bottom