Rais Samia peleka zabuni tuinunue Manchester UTD tupate FDI ya uhakika

SHANTI

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
296
365
Habari wana jamvi JF,

Baada ya muda mrefu leo nimeona nitoe ushauri kwa serikali yetu pendwa ya JMT chini ya Rais wetu shupavu Samia Suluhu Hassan, Lengo langu ni kumuomba aione haja ya taifa letu Tanzania kuwa na uwekezaji wenye tija nje ya taifa letu la Tanzania.

Hivi karibuni wamiliki wa Klabu ya Manchester United wametangaza kuiuza klabu hiyo kwa dau nafuu na la kutupa la dola 4.8 BN (TZS 14 Trillion ).Mpaka hapa ninavyoongea ni mtu mmoja tu kajitokeza hadharani kuonesha nia ya kuinunua timu hiyo ambaye ni mmiliki wa kampuni Ineos bwana Jim Ratcliffe Mimi naona sio vibaya kupitia wizara yetu ya utalii tukajitokeza hadharani kupeleka ofay a kuinunua Klabu hiyo kwa dhana kuongeza Foreign Direct Investment kwa sababu itatupa faida nyingi sana ukifananisha na ilivyosasa.

Hivi majuzi ndugu zetu Rwanda waliwekeza kwenye Klabu ya PSG kwa dhana ile ya VISIT RWANDA na kuitambulisha nchi y ana faida utalii wanazivuna vizuri.

Kwa nini Tanzania inatakiwa kuinunua Manchester United sasa hivi na sio klabu nyingine?

Kuinuna klabu kuna faida chanya nyingi sana lakini leo nataja chache tu.Endapo tutapeleka zabuni ya ununuzi wa klabu ya Man UTD tufaidika na vitu vifuatavyo/

1.FDI & FPI
- FDI ni kifupi cha neno Foreign Direct Investment, yaani uwekezaji wan chi Fulani kwenye nchi nyingine kwa dhana ya kunufaika fursa za kiuchumi zilizopo kwenye nchi husika. Tanzania tuna FDI chache sana, majirani zetu Kenya wametuzidi sana kwenye uwekezaji kwenye nchi za kigeni. Uwkezaji huu hufanywa na taifa fulamni knunua au kuaznia kampuni kwenye nchi ya kigeni kwa lengo la kunufaika na fursa za kiuchumi.Endapo tutafanikiwa kuinunua nchi yetu itafanikiwa kumiliki kitega uchumi chenye mvuto na thamani kubwa sana hapa duniani ukilinganisha vitega uchumi tulivyo nanvyo hivi sasa.

-FPI, kifupi cha Foreign Portfolio Investment, yaani kwa lugha nyepesi ni itaongeza Asset za nchi katika lile jedwali letu la mahesabu pale benki kuu ya Tanzania, na moja ya faida ni serikali ya Tanzania kuingia katika masoko makubwa hisa duniani kama vile NYSE,LSE, n.k kila mtu anajua kuwa hisa za Manchester kwenye soko la dunia zilzivyo na thamani so kwa dhana ya kuongeza asset labda tushindwe kwa ujinga na ulofa wetu maana tutaamua wenye tufungamanishe bidhaa gani kwenye product za Manchester kwa kipindi kijacho ila hilo ndio tobo la kuingia mjini.

2.KUKUZA BRAND ZETU ZA UTALII
Chapa yetu ya Utalii inaenda slogani inaitwa Tanzania UNFORGETTABLE, vivutio vifuatavyo vya utalii vinapatikana kwenye nchi yetu , mlima kilimanajaro,mbuga za Wanyama kama Serengeti,Ngorongoro kreta,fukwe za bahari nzuri kama kendwa kule Zanzibar.

Hebu fikiria kama mimi, Mbele ya Jezi ya Manchester kumewekwa neno la udhamini Serengeti, uwanja wa mazoezi wa Manchester umeandikwa RUAHA PARK TRAINING, halafu mkononi kwenye jezi upande wa kushoto kumeandikwa VISIT TANZNIA. Hii kwa mechi za ligi kuu tu.

Ukienda kwenye michuano ya ulaya mbele ya jezi pameandikwa Mount Kilimanjaro, upande wa kushoto Tanzania unforgettable. Nyieee hamuogopi kuona mashabiki bilioni moja wa mnchester united wakisoma vivutio vya utalii vya Tanzania ?

Nakuomba mama samia mtume balozi wa Tanzania pale uingereza atafute dalali tupeleke zabuni ya kuinunua klabu hii tutapata faida sana, hata tusipoinunua tutapata mention za kutosha kutoka vyombo vyote vya Habari dunia nzima na tutaita press kwamba tumenyimwa haki ya kununua timu wakati uwezo tunao ( kuitwa press wala usihangaike mkole huu mwachie Haji Manara anaiweza kazi)
Inawezekana kabisa watume Tanapa wafungue kampuni Uingereza kisha wape 20 trilion ishirini kama mtaji wa kununua timu na kuiendesha kwa miaka mitano ya kwanza, utakuja kunishukuru baadaye. Sasa hivi hatutangazi kiviiile lakini utalii ndio sekta inaingiza pato kubwa sana Tanzania na wamekuja mpaka kina David Beckham, na wachezaji wengine maarufu itakuwaje tukiimili timu hii yenye ushawishi mkubwa dunia nzima.


3.KUAMSHA MORALI YA SOKA LA TANZANIA

Endapo tutafanikiwa kuinunu Manchester united tutaweka sharti la vipaji vipya kutoka bongo kulelewa kwenye akademi ya Watoto ya Manchester na kuanzia hapo tutafanya biashara kukuza na kuinua vipaji vyetu, bila kujali wanaweza au hawawezi na labda baada ya miaka kumi tutapata world class player wa kutupeleka world cup 2042.

Narudi tena kama huamini katika maono haya huenda unashauriwa na watu waoga. Lets Gamble tukipata tumebutua na tukikosa tumekosa ila brand yetu ya utalii itapaaa mara bilioni moja na kuanzaia hapo visokolokwinywo watani zetu Kenya watatuheshimu.

Nawakaribisha kwa mjadala mpana wenye afya na kujenga, kukosoa inaruhusiwa ila usitoe matusi.
 
FB_IMG_16735438333205303.jpg
 
Kwa American Glaziers Kununua Man United kuliongezea nini Taifa la Marekani zaidi ya Chuki za Mashabiki kuona jamaa wanatumia Timu yako kukopea mikopo hence kuifilisi na kuiongezea Madeni ?

Hujui kwamba they are among the Most Hated ? au Haukuona yaliyotokea Goodison Park Majuzi mechi ya Everton ?

In Short alisema Sir Allan Sugar ukitaka kupoteza Pesa Miliki Timu.... Unless una brand yako na pesa za ziada za kutupa hapa na pale ili uweze kununua goodwill ila kama wewe ni mtembeza Bakuli kujifanya mifuko imejaa na kufanya unachosema tufanye, bakuli unalotembeza litakosa wachangiaji (kwamba hauhitaji msaada)

Pili umeongelea deals tofauti, tofauti kumiliki timu haimaanishi utapewa exclusive rights za kutangaza kwenye Team Kits (hio ni biashara / mkataba tofauti) umiliki wako jua unategemea kufanya manunuzi ya wachezaji ambao malipo yao ya pesa ni lukuki ndio maana timu zote huko Ulaya zina Operations Costs zinazidi mapato
 
Haiwezekani mkuu coz hiyo pesa Ni ndefu sana
Makusanyo ya TRA, 12 TRLN na tuanyo reserve ya Gold na Tanzanite na madini pale BOT tunaweza kuzibadili kuinunua timu.

Na kupitia matangazo ya utaliii tutaongeza mapato
 
Umetaja bei ya kuinunua pekee, lakini hujamulika kwenye gharama za uendeshaji...
KLABU inajiendesha yenyewe, shida ni usimamizi.

Level ya Man UTD ,ukiinunua hauangaiki na operation cost Kama simba na Yanga.

Lakini Kama nchi tunaweza kunitumia Kama kitega uchumi tutakopa mara kumi ya tunavyokopa Sasa.

So, I believe wage bill haiwezi kutusumvua Sana.
 
Kwa Ameuona jgezea Madeteza Pesa Miliki Timu.... Unless una branhosema tufanye bakuli unalotembeza litakuwa wachangiaji (kwamba hauhitaji msaada)

Pili umeongelea deals tofauti, tofauti kumiliki timu haimaanishi utapewa exclusive rightsba tofauti) umi yao ya pesa ni lukuki ndio maana timu zote huko Ulaya zina Operations Costs zinazidi mapato
ile timu alinunua glazer kwa faida yake na sio taifa la marekani. Hapa anaongea kununua kama taifa la tanzania kwa faida yake.

ni kweli timu zinafilisi lakini kama taifa tunaweza kupata faida ya kutangaza vivutio vyetu kwa upana zaidi.

hizo pesa tutakazopata kwenye biashara ya utalii ndio zitasaidia operation cost.

timu namiliki mimi deals za kutangaza biashara kwa nini? Wewe ukiwa unamiliki timu utatangaza unachotaka wewe au chingine ambacho kinaweza kukuingizia zaidi ya ile biashara yako.

tunaweza tusiwe na hizo trilion 14 lakini jamaa ana wazo zuri na naona umeongea mengi out of point.
 
Back
Top Bottom