Rais Samia ni kiongozi wa vitendo

Political Jurist

Senior Member
Sep 6, 2021
120
104
RAIS SAMIA NI KIONGOZI WA VITENDO

Na.Amon Nguma

Tumetimiza miaka miwili kwa mafanikio makubwa na sasa tumeingia mwaka wa tatu kwa kishindo kikubwa zaidi chini ya Uongozi wa Mama Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa kiongozi wa vitendo na kazi zaidi kuliko maneno.

Kazi yetu ni kutambua, kumtia moyo, kumpongeza na kumuombea heri kwa mambo mazuri anayolifanyia Taifa letu ikiwemo;

1). Utoaji wa Vibali vya Ajira na mazingira bora ya Ajira nchini .
Katika kipindi kifupi cha Uongozi wa Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan tumeshuhudia maelfu ya ajira zikitolewa kwa watanzania
-Maelfu ya Ajira katika Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama.

-Kada ya Afya na Elimu
Ajira 9675(mwaka 2021)
,Ajira 17412 (mwaka 2022) na tarehe 12/04/2023 zimetangazwa ajira 21,200 ajira hizi zimetolewa mfululizo kwa miaka mitatu katika sekta ya Afya na Elimu kwa wenye sifa tutumie fursa hii.

-Ajira mbalimbali za mamlaka za Serikali na Mashirika ya Umma zinazoendelea kutangazwa kila siku na Sekretariet ya Ajira ( Recruitment Portal)

-Ajira zilizotengezezwa na zinazoendelea kutengenezwa kupitia uwekezaji na miradi inayotekelezwa nchini ikiwemo SGR na STIGLERS .

2). Kuinua Sekta ya Kilimo Nchini .

Chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia sekta ya Kilimo imepata mapinduzi makubwa ya Teknolojia na miundombinu ikiwemo ya umwagiliaji, uanzishwaji wa mashamba makubwa (block farming), ruzuku ya Mbolea, uwezeshaji wa mbegu na utaalamu kwa wakulima na kubwa kuliko ni Mradi mkubwa wa kuwaingiza vijana kwenye kilimo (Building Better Tommorow) ambapo vijana 812 (awamu ya kwanza) wapo kwenye hatua ya mafunzo ,vijana watapewa ardhi na fedha lakini pia na mengine mengi katika sekta ya Kilimo.

3). Uwazi na Uwajibikaji;
Ni kipindi hiki ambacho tunaendelea kuchambua Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ufanisi wa Ripoti hii umetokana na maamuzi ya Rais Samia kuiongezea Ofisi ya Mkaguzi (CAG) Fedha na watumishi ,hatua hii imeiwezesha ofisi kufanya kazi kwa ufanisi na mambo yote kuwa wazi hatua iliyopo ni wahusika kuwajibika kwa kujibu hoja na baadae hatua za kisheria kuchukuliwa kama ilivyoekekezwa na Mhe. Rais .

4). Uboreshwaji wa Sekta ya Afya na Elimu
Rais Samia amekuwa mlezi bora wa sekta hizi muhimu na nyeti katika utoaji huduma .
-Ujenzi wa Shule za Sayansi za Wasichana kila Mkoa .
-Ujenzi wa Madarasa zaidi ya 20,000 .
- Ajira za Afya na Elimu
-Ugawaji wa Vifaa vya TEHAMA kwa Walimu .
-Ujenzi wa Zahanati, Vituo vya Afya ,Hospitali za Wilaya ,Mkoa na za Rufaa.
-Uzinduzi wa Mitambo na Teknolojia za Kisasa ya Afya.
-Uendelezaji wa Wataalamu wa Afya katika Taasisi za ndani na nje ya Nchi.

5). Ujenzi na Uboreshwaji wa Miundombinu.

Ujenzi wa Viwanja vya Ndege ikiwemo vya Mikoani, Uboreshwaji wa Uwanja wa Kimataifa Julius Nyerere, Ujenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Msalato, ujenzi wa Barabara na Bandari ikiwemo ya Uvuvi ya Kilwa ( Bil.266.7).

Chini ya Uongozi wa Rais Samia tumeshuhudia mafanikio makubwa katika Diplomasia ya Uchumi, Demokrasia, Utawala wa Sheria, Uhuru wa Vyombo vya Habari, Maboresho ya Miundombinu ya Michezo uwezeshaji na hamasa katika Michezo na mengine mengi ambayo hayajaorodheshwa hapa .

Pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi hii njema katika Taifa letu.

Tulipo ni pazuri, tunapokwenda matumaini ni makubwa zaidi chini ya Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

KAZI IENDELEE


Samia-Suluhu-Hassan-time100-2022.jpg
 
Sahihi, ila kuna baadhi ya viongozi wasio na hofu ya Mungu Wana hujumu nia na dhamira njema ya Mhe. Rais.
Tunawaombea watu hao kwa Mungu awape maradhi sugu wateseke nayo Hadi kifo.
 
kalazimishwa kufanya au niwajibu wake yani hizi ng'ombe zimekaliana CCM sijui zinaishi tofauti na sisi
 
Back
Top Bottom