johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 84,915
- 143,469
Rais wa JMT mh Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Kanisa la Anglikana na Viongozi wengine wa Dini kuzidi kuliweka Taifa letu katika Mikono salama ya Mungu na kuilinda Amani Yetu na tusikubali Kuyumbishwa na mtu yoyote asiyelitakia mema Taifa letu
Rais Samia amesema hayo Wakati akifungua Jengo la Kitega Uchumi la Kanisa Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika jijini Dodoma
Jengo hilo la kisasa kabisa jijini Dodoma linaitwa NMB Safina House
Mlale unono 😀😀
---
Rais Samia leo Agosti 15, 2023 Wakati akifungua Jengo la Kitega Uchumi la Kanisa Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika jijini Dodoma amesema:
“Serikali inatambua na kuthamini mchago mkubwa unaotolewa na taasisi pamoja na mashirika ya kidini nchini, mbali na kutoa huduma za kiroho ambazo zinachangia sana kujenga taifa la watu wenye uadilifu na uchaji Mungu, taasisi hizi zinasaidia sana Serikali katika kutoa huduma kwa wananchi hususani afya, elimu, maji na hata kilimo.”
“Nawasihi viongozi wa kanisa hili [Anglikana] na viongozi wote wa dini nchini kuendelea kuliweka taifa letu katika mikono salama ya Mwenyezi Mungu ili lidumu katika amani, umoja na mshikamano. Kamwe tusikubali kuyumbishwa na mtu yeyote yule asiyelitakia taifa letu mema.”
Nataka kuhimiza kazi ya kulinda maadili na kukemea maovu. [Viongozi wa dini] Muwafundishe vijana, lakini mbali na vijana hata wakubwa wale ambao wanalitumia kanisa kufanya mambo ya hovyo, naomba kemeaneni.”
Source: Swahili Times