Rais Samia kufanya ziara ya kikazi ya Siku Tano Nchini Uturuki kuanzia Tarehe 17-21 Mwezi huu

Rais Samia anatarajia kuanza ziara ya siku 4 Nchini Uturuki tarehe 17/4/2024 Kwa Mualiko wa Rais huyo wa Taifa kubwa bwana Recep Yayib Erdogan.

Huenda Samia ndio atakuwa Rais wa kwanza kufanya ziara rasmi baada ya bwana Erdogan kuchaguliwa Kwa awamu nyingine ya Uongozi.

Kila la Heri madam president,tunatarajia harakati zako za kufungua masoko ya bidhaa za Tanzania zitaendelea.

Msisahau kuwaambia Waturuki wanazingua kwenye ujenzi wa Sgr na Barabara.

View: https://twitter.com/Hakingowi/status/1779887483766866125?t=w3QblGwyYqLwGvJj2VXQBQ&s=19

My Take
Chini ya Samia diplomasia imeimarika sana ,Kila mbabe wa Dunia anataka Urafiki na Tanzania kuanzia Kwa Joe Hadi Kwa Putin na Sasa ni Kwa wazee wa Yappi Merkez.

Kazi iendelee.

View: https://www.instagram.com/p/C5zjL_niAYz/?igsh=MWkzaXBmYWUxNXU2

Utafikiri amegundua nuclear! Kumbe matembezi tu!
 
Nchi za wenzetu wakifanya hizi ziara zina ambatana na kutoa vikwazo vyote baina ya nchi husika ikiwemo Visa kwa raia wa pande zote mbili na vyengine kama kutafuta masoko, kuondoa vikwazo vya kiuchumi nk.
Lakini mbona hatuoni haya sisi raia wa kawaida au ni kwa wakubwa tu?
Yote kwa yote safari njema rais wethu.
Kaa kwa kutulia mambo mazuri yataendelea kumiminika hapa nchini kupitia mkono wa Rais Samia
 
Ameenda kukopa fedha za ujenzi wa SGR maana yap markez wameacha kufanya kazi hivo baada ya serikali kuomba mfumo wa ukopeshwaji Kwa riba ndogo ndio matokeo hayo ya ziara
 
Ndugu zangu Watanzania,

Habari ni kuwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan anatarajia kufanya ziara ya kikazi nchini Uturuki kwa mualiko maalum wa Rais wa nchi hiyo Mheshimiwa Erdogan. Hii

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Rais ana raha gani kufanya ziara wakati raia wa Rufiji wanaogelea kwenye mafuriko kama mamba yaliyosababishwa na serikali?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Habari ni kuwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan anatarajia kufanya ziara ya kikazi nchini Uturuki kwa mualiko maalum wa Rais wa nchi hiyo Mheshimiwa Erdogan. Hii imeelezwa na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mheshimiwa Januari Makamba.

Inaelezwa kuwa ziara hii inalenga kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia,biashara,uchumi,siasa na masuala mengine mbalimbali.inaeleza ya kuwa akiwa nchini humo Mheshimiwa Rais atapata fursa ya kuhudhuria kongamano kubwa la biashara na uwekezaji litakalofanyika mji wa Instanmbul ,ambapo hapo Mheshimiwa Rais atakutana na wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali wakubwa.

Lakini pia Mheshimiwa Rais atakutana na makampuni makubwa 15,ambapo atatumia nafasi kuweza kuwashawishi kuja kuwekeza hapa nchini.imeelezwa pia ya kuwa imepita miaka 14 tangia Rais kutoka Tanzania kuitembelea nchi hiyo,lakini pia imepita miaka 7 tangia Rais wa nchi hiyo aje aitembelee Tanzania,ambapo mara ya mwisho ilikuwa ni 2017 wakati wa utawala wa hayati dkt John Pombe Magufuli.

Imeelezwa pia kuwa uturuki ni miongoni mwa nchi 20 zenye uchumi mkubwa hapa Duniani,na hivyo kuwa nchi muhimu katika kushirikiana nayo na kuweza kufaidika kwa fursa mbalimbali.lakini pia imeelezwa pia kuwa biashara na maingiliano ya nchi hizi mbili yameongezeka sana kwa sasa jambo linalochochea umuhimu wa kukaa pamoja kwa viongozi wetu katika kuimarisha ushirikiano zaidi kwa maslahi ya pande zote mbili.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Waende huko ili wapate per diem zao, lakini siyo kuiletea nchi maendeleo
 
Sijui tunaenda kuuza SGR yetu.
 
Back
Top Bottom