Rais Samia, imulike Bandari ya Dar nchi inahujumiwa, kaweke Kambi pale Bandarini

Just thinking aloud: unaweza kuwa mpango wa kuaminisha watu kuwa bandari ya Dar imeelemewa hivyo solution ni kujengwa bandari ya Bagamoyo. Tutafakari: Thread kama hizi zinazoweza kufuatiliwa na matamko kutoka kwa viongozi kuwa ''hata kwenye mitandao kelele zinapigwa kuwa bandari ya Dar imeshindwa kuhimili msongamano hivyo bila bandari ya Bagamoyo ni bure''
Nimekuelewa sana...
Nilikuwa sijafikiria hiki kitu,umenifungua.!
 
Meli za kutoka Dubai kuja DSM huchukua siku 14, Mzigo ukifika Dar Es Salaam bandarini utakaa siku hata 20-28 ukisubiri kupakuliwa.

Meli ikitoka UK au China itatumia siku 28-30 kufika Dar, Mzigo ukifika hapo Bandarini unachukua siku 20-28 zingine kupakuliwa.

Gharama za Usafiri imebidi SHIPLINERS waziongeze kufidia muda mrefu wa kusubiri hapo Bandarini.

Sasa hivi Wafanyabiashara kutoka CONGO DR, RWANDA, MALAWI, ZAMBIA, UGANDA wameanza kukimbilia Bandari ya Mombasa kupitisha mizigo yao.

Mheshimiwa Rais Samia, ukicheka na nyani utavuna Mabua., wananchi vitu vitazidi kupanda bei bila sababu yoyote ya maana.

Nimekuwekea na VIDEO uisikilize kama ushahidi mwingine.

KAZI IENDELEE
Rais huyu huyu Chifu Hangaya au ni yupi? Kama ni Hangaya alishabariki wizi wa watumishi wa Serikali,hakuna jipya
 
Meli za kutoka Dubai kuja DSM huchukua siku 14, Mzigo ukifika Dar Es Salaam bandarini utakaa siku hata 20-28 ukisubiri kupakuliwa.

Meli ikitoka UK au China itatumia siku 28-30 kufika Dar, Mzigo ukifika hapo Bandarini unachukua siku 20-28 zingine kupakuliwa.

Gharama za Usafiri imebidi SHIPLINERS waziongeze kufidia muda mrefu wa kusubiri hapo Bandarini.

Sasa hivi Wafanyabiashara kutoka CONGO DR, RWANDA, MALAWI, ZAMBIA, UGANDA wameanza kukimbilia Bandari ya Mombasa kupitisha mizigo yao.

Mheshimiwa Rais Samia, ukicheka na nyani utavuna Mabua., wananchi vitu vitazidi kupanda bei bila sababu yoyote ya maana.

Nimekuwekea na VIDEO uisikilize kama ushahidi mwingine.

KAZI IENDELEE
Hakuna Rais hapa.
 
Mama hataki makuu, anajiandaa na kusheherekea mwaka mmoja wa kuongoza watanzania 'hoehae'
 
Ukweli tuliokua tunampinga Magufuli sasa ni kama tunaona aibu tu; mambo mengi kwasasa yapo yapo tu, maadamu kunakucha! Bandari, umeme, maji, ajali barabarani, vibaka is almost vyote vimerudi kama zamani. JPM alikua mwamba, wabishi wote wanaongelea mdomoni tu but mioyoni mwao wanamkubali!
 
Maboresho kadhaa yamefanyika lakini bado wanahitaji kufanya investment zaidi hasa katika masuala ya kupakua mizigo kwa wakati , hii itasaidia efficiency katika utendaji wa kazi wa Bandari, nakumbuka Kagame alishawahi kusema akipewa hiyo bandari hata fanya kazi nyingine yoyote na ataendesha nchi kwa mapato yatokanayo na Bandari. Cha msingi baada ya kulalamika washauriwe jinsi ya kuboresha maana tukiwa watu wakutupa lawama tuuu bila ku suggest solutions itakua kama tunapiga blah blah tu. Kadhalika tungepanua capacity ya Mtwara na Tanga tusingekua na malalamiko ya ucheleweshaji wa mizigo ya wateja. Korea wenzetu wamefanikiwa sana kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwao hasa masuala ya port and cargo management
 
Watanzania tutatoka tulipo mwaka tutaojielewa tunataka nini!
Nakumbuka wakati wa JK watu walisema mpole anacheka cheka tuu ... tupate dictator tena kwa kutolea mfano wa Rwanda PK ....
Mungu akasikia kilio akawapa JPM ... bado mkalalamika.... mmeletewa mpole 😂
Mnalalamika 😂
Nyie mnataka nini?
Chagueni moja hamuwezi kuwa na vyote... you can not eat your cake and still have it ... moto Au baridi? Uvugu vugu ni unafiki 🤣
 
Mkuu kwa Bandari nadhani hata angekuja kutawala nani! Pale ni pagumu.
Kama kwa Mwendazake ambaye alikuwa mkali na akamweka mtu wa karibu yake aliyekuwa mkali lakini upigaji ulikuwa palepale sembuse Mama?

Pale unamsingizia tu mwenda zake mbona mambo yalinyooka sana pale vitendo vya watu kugawana manoti kwanye buti za gari mbona vikoma . Hivi sasa naina mambo yameshaarudi kwq kasi na hao ndo wanampamba mama na kumtukuza kuww ameifungua nchi mara anaupiga mwingi
 
Iyo bandari ni jipu sana hopeless kabisa Hapo wafanya kazi wengi wa hapo amna kitu kichwani
 
Kagame alituambia kwamba tumpe Bandari ya DSM tu ataiendesha Tanzania na kisha hela inayobakia tusimuulize - tukagoma.
 
Hajapatikana kiongozi anayetumia akili tu. Hakuna kitu kinachoshindikana pale. Magufuli alikuwa anaongoza kwa style za zamani sana. Ni lazima angeshindwa. Samia yeye ni kama Kikwete. Bora liende. Nakuapia akipatikana kiongozi mzuri akija na mikakati ya kisayansi pale kila kitu kinanyooka.

Mikakati ya kisayansi ambayo wew mwenyewe umeshindwa kuitwja ni ipi wew unadhani mpaka mtu anacheze scaner na mifumo ya TPA kuna sayansi tena au ni kufukuzana tu
 
Mkuu kwa Bandari nadhani hata angekuja kutawala nani! Pale ni pagumu.
Kama kwa Mwendazake ambaye alikuwa mkali na akamweka mtu wa karibu yake aliyekuwa mkali lakini upigaji ulikuwa palepale sembuse Mama?
Pale sio pagumu hata kuna washenzi wachache wanaiharibu Ile bandari mm nimeshaongea wee na wakuu mpaka nimechoka pale ni pakiwaki Sana kuna ushenzi mwingi mno nimefanya KAZI pale miaka mi 2 nimesoma ushenzi mwingi mno mpaka nimeamishwa nao nipo songea we fikiria mbona TICTS wako vzr kwann TPA kuna shida Sana ni PA kishenzi hujuma nyingi mno Yani wanamlolongo mkubwa usio na maana yeyote wateja kila siku Wanalalamika rushwa kila sehemu. Kuanzia walinzi mpaka ma ofisa wai ni rushwa tuu Ile bandari ni ya ajabu mno....
 
Umeongea kitu kikubwa sana, shida sio ukali na shida sio upole.
Hapondio balaa lilipo, na bahati mbaya wa kutumia akili ili mambo yaende hayupo

Hiyo akili umeishindwa kuitumia wew nacviongozi wote waliopita wote hawakuwa na akili ila wew ndo unaakili . Mtu anaharibu scsnner unataka utumie saicence ip tena bwashee kama dawa sio kufukuza tu
 
Mtanikumbuka!
hata wakati wake watu walikula sanaaa tu, sema walikuwa ni wachache kula kwa mduara wao, of course sasa hivi kinacho determine ni urefu wa kamba yako.

Hapa ndipo watanzania mtaelewa kwamba M0 Energy na mishikaki ni mlo wa usiku.
 
Back
Top Bottom