Rais Samia chukua hatua dhidi ya TAKUKURU; Wanatumia taarifa za rushwa kwa manufaa binafsi

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,251
2,875
Ukiangalia mtandao wa TAKUKURU kuna njia nyingi za mawasiliano ambazo wanazitaja kama njia mojawapo ya kutoa taarifa za siri kuhusiana na rushwa/ufisadi. Tumefanya majaribio tukiwa watu watatu kwa kuwapa taarifa tofauti nne; tatu zikieleza matatizo ya rushwa ktk idara za serikali na moja ndani ya wizara pamoja na vielelezo. Tumethibitisha taarifa hizi kuwafikia TAKUKURU Makao makuu. Baadaye tena tumethibitisha taarifa hizi kuwafikia watuhumia wakiwa ktk majadiliano na maafisa wa TAKUKURU, siyo kwa kutaka taarifa, bali kwa kutaka mambo yasawazishwe kimya kimya. Bahati mbaya maafisa wa TAKUKURU wanahitaji pesa toka kwa waliotuhumiwa na kuwaongoza nini kifanyike ili mambo yatulie.

Kwa ufupi, TAKUKURU ni hovyo! Wapo kutafuta michongo toka kwa wananchi. Mwenye madaraka juu ya TAKUKURU ni rais. Anatakiwa kuchukua hatua kuonesha kwamba yeye siyo sehemu ya ufisadi hadi TAKUKURU i.e hadi ndani ya ikulu.
 
Back
Top Bottom