kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 118
- 237
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wanufaika wa mradi wa kunusuru kaya maskini (TASAF) kwa kuuongezea muda mradi huo hadi mwaka 2025 ambapo awali ulikua uishie mwaka 2023.
Moja ya manufaa ya mpango huo ni kuendelea kuwanusuru wananchi na umaskini uliokithiri ambapo Kaya 173,076 zimehitimu zinaweza kujitegemea bila ruzuku. Kaya hizo zinaweza kumudu gharama za matibabu, kusomesha watoto na zina vitega uchumi na biashara za uhakika zinazoongeza pato la familia na zinakopesheka kwa kuwa na rasilimali zalishi.
Kaya hizo zilizohitimu ni miongoni mwa kaya 886,724 zilizohakikiwa na kuongeza kuwa kaya 730,138 bado zina hali duni kiuchumi na hivyo zinaendelea kuwepo katika kipindi cha pili cha mpango na kupokea ruzuku huku kaya nyingi zikiwa ni zile za wazee na zinaoongozwa na watoto.