Rais Samia anaheshimika na kukubalika sana na Watanzania

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,354
9,784
Ndugu zangu watanzania,

Kwa hakika Rais Samia Anaheshimika Na kukubalika Sana na mamillion ya watanzania,ndio maana kila utakakopita mitaani unaona namna mh Rais anavyozungumzwa kwa mema,kila mtanzania ni mtetezi wa Rais Samia,watu wengi Sana wanamuunga mkono yeye na serikali Yake kutokana na namna anavyoendesha nchi yetu.

Huwezi ukasikia mtu mwenye Akili Timamu na anayejishughulisha na kazi za kujipatia ridhiki yake akisema na kumsema vibaya Rais Samia,kwa kuwa kila mtu anampongeza mh Rais kwa namna alivyoweka mazingira wezesha kwa kila mwenye kufanya kazi kunufaika na jasho lake.

Watanzania wanasema Rais Samia Amekidhi matarajio yao,amekata kiu Yao juu ya kuhitaji kiongozi wa kuwaongoza njia,kuwafariji penye shida,kuwa tumikia kwa upendo , unyenyekevu na usikivu,kutambua kuwa wao ndio wenye nchi na wenye mamlaka juu ya nchi na Taifa lao, wenye kuhitaji mipango ya serikali yenye kutoa kipaombele katika maisha Yao, wanaona serikali ya Rais Samia imekata kiu Yao ya kumhitaji kiongozi mwenye huruma wapatapo maumivu, mwenye masikio ya kusikia sauti za wote hata zikwaluzazo masikioni na mwenye kupokea ushauri na kushaurika kwa maslahi mapana ya Taifa letu na mwenye kutambua kuwa yeye ni mwanadamu aliyeinuliwa na Mwenyezi MUNGU Kati ya mamillioni ya watanzania kwa ajili ya kuwasaidia na kuwatumikia watu pasipo ubaguzi.

Ndio maana kauli na matamko ya Rais Samia yanaheshimika na kusikilizwa Sana na watanzania,ndio maana hakuna migogoro Wala chuki Wala vinyongo vilivyotawala katika mioyo na vifua vya watanzania,ndio maana serikali Yake inaungwa mkono na watanzania wa makundi yote.ndio maana ya kutamalaki kwa amani na utulivu hapa nchini, ndio maana ya Taifa letu kuchanua na kung'aa kwa furaha na Tabasamu Katika nyuso za watanzania.

Ndugu zangu watanzania tunataka Nini Tena kutoka kwa Rais na mama huyu muungwana,mpole,mwenye busara,hekima,mzalendo wa kweli,mkarimu,mwenye huruma na unyenyekevu wa Hali ya juu,mcha Mungu na mwenye hofu ya Mwenyezi Mungu. Afanye nini mama na Rais huyu Jasiri na shujaa muongoza njia ambacho bado hajakifanya katika kulitumikia Taifa letu? Kipi ambacho hajakifanya ama kukigusa ama kukiweka katika mipango ambacho tumekiomba watanzania? Tunataka Nini watanzania Zaid ya haya mema na makubwa aliyotufanyia Rais na mama huyu wa kipekee kabisa na mwenye karama na kipaji Cha uongozi?

Kwanini Tusimuunge mkono watanzania Rais huyu mchapa kazi na mwenye Ari na dhamira ya dhati katika kuliongoza Taifa letu? Kwanini tusimpiganie na Kuendelea kumuombea Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia watanzania? Hatuoni namna anavyotupenda na kutuheshimu watanzania? Hatuoni namna alivyo msikivu na mwenye busara katika maamuzi yake ya kiuongozi? Tunataka nini Watanzania wenzangu?

Tufanyiwe nini turidhike? Tutendewe Nini tukubali kuwa mama yetu amejitoa na kujitolea kututumikia watanzania? Mama yetu ni mwanadamu na katika uanadamu wake amejitahidi na kutimiza wajibu wake katika kututumikia watanzania na hivyo Hatuna Budi Kuendelea kumuunga mkono Rais na mama yetu.

Kazi iendeleee, Mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Jinsi sukuma geng wanavyoingia kwenye huu uzi

20230503_080814.jpg
 
KATIKA HAO WATANZANIA ,MIMI NITOE
RIPOTI ZA CAG UNAFUATILIA?
Wahusika wote watachukuliwa hatua kali za kisheria watakapobainika kuhusika moja kwa moja katika ubadhirifu wa fedha za umma,katika Hilo mh Rais wetu Hana Subira Wala mzaha kwa mtu atakayechezea Senti yoyote ya mtanzania
 
Wewe ni mpumbavu. Yule aliyewekwa ndani kwa kisingizio cha kumtukana rais hakuwa mtanzania?

Anampenda Samia?

Mmetufanya punda wenu, mnakusanya tozo mnakula.

Tumenyamaz kwa kuwa hatujui pakuanzia na mnasaidiwa sana na polisi kutunyamazisha.

Mlaaniwe ninyi na vizazi vyenu.
 
Wahusika wote watachukuliwa hatua kali za kisheria watakapobainika kuhusika moja kwa moja katika ubadhirifu wa fedha za umma,katika Hilo mh Rais wetu Hana Subira Wala mzaha kwa mtu atakayechezea Senti yoyote ya mtanzania
Hatafanya lolote. Hana ujanja wowote. Ameibiwa mara ngapi na anawatazama tu?

Kama anaweza akaanze na Mwigulu, Januari na Nape.
 
Wewe ni mpumbavu. Yule aliyewekwa ndani kwa kisingizio cha kumtukana rais hakuwa mtanzania?

Anampenda Samia?

Mmetufanya punda wenu, mnakusanya tozo mnakula.

Tumenyamaz kwa kuwa hatujui pakuanzia na mnasaidiwa sana na polisi kutunyamazisha.

Mlaaniwe ninyi na vizazi vyenu.
Tangia lini matusi yamekuwa Ni ushujaa?
 
Hatafanya lolote. Hana ujanja wowote. Ameibiwa mara ngapi na anawatazama tu?

Kama anaweza akaanze na Mwigulu, Januari na Nape.
Hakuna aliye mkubwa mbele ya Sheria ,yeyote atakayebainika kufuja pesa za umma bila kujari cheo chake atawajibishwa kwa mujibu wa Sheria.
 
Hapana Mimi sitafuti uteuzi Bali naandika uhalisia wa mambo kutoka mitaani nakoishi na watanzania wa Rika na makundi yote,Ambao kwa kiasi kikubwa Wameonyesha kuridhishwa na uchapa kazi na utendaji kazi wa mh Rais wetu mama Samia suluhu Hassani
huu upuuz wk usihushe watu eti watu wachn wanamkubal pumbav sn ww
 
Hapana Mimi sitafuti uteuzi Bali naandika uhalisia wa mambo kutoka mitaani nakoishi na watanzania wa Rika na makundi yote,Ambao kwa kiasi kikubwa Wameonyesha kuridhishwa na uchapa kazi na utendaji kazi wa mh Rais wetu mama Samia suluhu Hassani
Nimekuuliza kuhusu namba mkuu maelezo marefuu ya nini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom