Rais Samia amemteua Dkt. Jabir Bakari Kuwe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akichukua nafasi ya Eng. James Kilaba.

Duh nasuburia vifurushi vishuke. Mtenguliwaji kafaidi vya kutosha kashiba katupandishia mabando
 
Pia lilikuwa jambo la busara kusubiri siku 21 zipite.

Hizi teuzi na tenguatengua zinaanza kutia shaka wananchi wengi.

Monong'ono imeanza mitaani kuulizia haya mavitu.

Ni nani alie nyuma za hizi pilikapilika?

Majibu yote yaja twangojea.
Ushaambiwa zege halilali...
 
Pia lilikuwa jambo la busara kusubiri siku 21 zipite.

Hizi teuzi na tenguatengua zinaanza kutia shaka wananchi wengi.

Monong'ono imeanza mitaani kuulizia haya mavitu.

Ni nani alie nyuma za hizi pilikapilika?

Majibu yote yaja twangojea.
Mtaani mama Rais samia anakubalika sana na wananchi. Wanaoleta maneno ni wale waliokuwa wananufaika na utawala uliopita.
 
Kazi nzuri, kabla week haijaisha tunaomba mama utufurahishe zaidi kwa kumng’oa yule mpuuzi alieenda kutuhadaa katika kipindi cha clouds 360!

Apate anachostahili nae... Hawezi kubariki ule ujinga wa sie wananchi kuuziwa 1GB kwa hela ya kununulia mboga
 
Uteuzi ndicho wanachojua kufanya
Bei ya vifurushi ndiyo ishapita hivyo
No ajira
No nyongeza ya mshahara
Hakuna kupandishwa madaraja
Kesho sijui atateuliwa nani tena... Kila siku teuzi teuzi teuzi wananikera sana. Hata. Mwendazake naye alikuwa hivyo hivyo
Teuzi teuzi
Yani kwako unaona chupa ileile na mvinyo uleule!
Kwani lazima unywe?
Mataputapu yapo kibao
 
Back
Top Bottom