Rais Samia aitetemesha Afrika na dunia, hotuba yake yavunja rekodi ya kufuatiliwa duniani siku ya leo

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,301
9,727
Ndugu zangu watanzania,

Siku zote naawaambieni watanzania wenzangu ya kuwa Mwenyezi MUNGU ndiye aliyempatia Rais Samia Urais ,ndiye aliyemuinua na kumfikisha hapo Alipo,Ndiye aliyempatia kibali Cha uongozi wa kufika hapo,ndiye aliye mpatia maarifa na njia katika kuliongoza Taifa letu, Ndiye anayeendelea kuwa upande wa Rais Samia na Taifa letu,Ndio sababu ya kuona kila anapogusa Rais Samia panafanikiwa,kila afanyacho Rais Samia kinasonga mbele,kila atamkacho Rais Samia kinapokelewa na watanzania kwa mikono miwili,kila apangacho na kudhamiria Rais Samia kinatokea kwa mafanikio makubwa Sana.

Katika siku ya leo Rais Samia Amejiandikia na kujiwekea Rekodi ya peke yake ambayo haitafutwa na yeyote baada yake, Amefanya tukio la kipekee ulimwenguni kwote ambalo huwezi ukalikuta likitokea katika nchi yeyote Ile Barani Afrika Na Duniani kwote kwa kwenda kujumuika na akina mama na viongozi kutoka chama kikuu cha upinzani na kuzungumza nao Kama Rais wa nchi, Kitendo na Hatua hiyo imevuta hisiaa za watu wengi Sana ulimwenguni kwote.

vyombo mbalimbali vya Habari vya kimataifa Duniani kwote vimejikuta vikitekwa na Rais Samia kana kwamba Rais Samia ndiye kiongozi wa ulimwengu huu, kila Kona kila mahali kila kurasa ya magazeti kila chombo cha habari Ni juu ya habari za Rais Samia na hotuba yake ya karne ambayo itabaki katika kumbukumbu za walimwengu na kusikilizwa na kusimuliwa kwa vizazi na vizazi,

Rais Samia kawagusa watanzania na Afrika yote kwa ujumla,watu wengi wametokwa na machozi na kulia kwa furaha kwa namna Rais Samia alivyowagusa, watanzania wametamka na kusema hakika Taifa Leo limekuwa na kujaa furaha na Tabasamu utafikiri ndio tumetoka kupata Uhuru kutoka kwa mwingereza, Bendera za furaha shangwe vifijo na Nderemo zimepepea katika mioyo ya watanzania, Watanzania kwa umoja wao huku mitaani wameshikana mikono na kukumbatiana kwa furaha na upendo, Tanzania ya Ndoto ya nyerere imeoteshwa na kuzaliwa upya, watanzania wanasema Hayati Baba wa Taifa Amezaliwa ndani ya Rais samia,.

Hakika Rais Samia Ni zawadi kwetu watanzania,Afanye Nini Rais Samia kwetu watanzania Hadi tuamini kuwa na kusadiki ya kuwa hii Ni zawadi kwetu? Afanye Nini Rais wetu Tumkubali kuwa huyu Ni mkombozi wetu katika kuponya wenye majeraha na maumivu na kuleta Tabasamu mioyoni mwetu? Nani ambaye hajaguswa na uchapa kazi wa Rais Samia? Watanzania tuna taka Nini Tena? Nini shida yetu Tena? Kwani tuna taka tufanyiwe Nini ili Turidhike? Rais Samia Ni mwanadamu na katika wanadamu wake kafanya kila linalowezekana kumpa furaha kila mmoja wetu,kagusa maisha ya kila mtu, kasikiliza sauti za watu wote wamakundi yote.

Sasa kwanini Tusimuunge mkono Rais wetu na mama yetu? Kwanini tusimuombee Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia watanzania? Kwanini Tusimpe nafasi ya muhula wa pili ili aendeleze kazi njema ya kulijenga Taifa letu na kumuinua kiuchumi kila mmoja wetu? Rais Samia kaonyesha usikivu unyenyekevu uungwana na upendo kwa kila mmoja wetu, Sasa kwanini tusimkumbatie Mama na Rais huyu muungwana mwenye kumfuta machozi na kumfariji kila mwenye kububujikwa na machozi?

Tunamtaka Nani mwingine Kama siyo Rais mama Samia ? Hamuoni furaha upendo na Tabasamu lililotamalaki hapa nchini? Nani kaumizwa na Rais Samia kwa maneno au matendo? Rais wetu mpendwa mama Samia Ni kiongozi wa haki mpenda Haki mtenda haki kutokana na ucha Mungu wake na kujawa na hofu ya Mwenyezi MUNGU katika kifua chake.

Ni kiongozi wa aina yake ambaye kila mtu anatamani aendelee kuwepo madarakani,Nikiongozi aliyeleta matumaini kwa watanzania, Nikiongozi aliyeinua Imani na upendo kwa watanzania juu ya utanzania wao, Ni Rais na kiongozi aliyewafanya watanzania wajisikie fahari kuzaliwa Tanzania kuitwa watanzania na kuongozwa na Rais Samia.

Hakika Rais huyu mwenye ushawishi zaidi Barani Afrika na ambaye anachukuliwa Kama mtetezi na sauti ya Afrika na waafrika ameacha gumzo kubwa Sana Barani Afrika na Dunia nzima kwa ujumla na kuitetemesha Dunia na siasa za kimataifa na kuacha SoMo na funzo kwa viongozi wote wa Afrika, Kama Afrika nzima ingeungana na kuwa nchi moja naamini Rais Samia angechaguliwa na kupita kwa kishindooo kikuu.

Hongera Sana Rais Samia kwa Kuendelea kuiweka Tanzania katika kilele Cha mafanikio na mfano wa kuigwa Barani Afrika,umeliheshimisha Taifa letu, umewaheshimisha watanzania na kuwafanya wakubalike mahali popote waendako na kunyenyekewa na kusikilizwa kwa uzito mkubwa Sana. Rais Samia Ndio chaguo letu watanzania na tuna Imani naye na tupo tayari kuongozwaa Naye kwa kipindi na muhula mwingine Tena ili Taifa letu liendelee kuwa Tulivu na lenye amani na mafanikio kwa kila secta na nyanja.Ni Samia Hadi 2030 ni mama muhula wa pili Tena.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Naona sasa ushauri wangu kwamba mwisho uwe unaweka namba za simu umeufanyia kazi.

Ngoja chawa wa mama wapite hapa unaweza kuambulia chochote,kaa tu karibu na simu yako.
 
Mama hataki chawa, anataka akosolewe constructively
Kwani wewe Nani kakuzuia kukosoa Kama unaona Pana pakukosoa. Mimi naziona juhudi kubwa za mh Rais katika kuwatumikia watanzania na kuwainua kiuchumi, naziona juhudi za mh Rais katika kupambana na changamoto mbalimbali na kuzipatia majibu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom