Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,820
- 4,573
Rais Samia ameteua na kufanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala na Kaimu Kamishna (TANAPA).
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemhamisha kituo cha kazi Sixtus Raphael Mapunda kutoka Wilaya ya Sumbawanga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke akichukua nafasi ya Mobhare Holmes Matinyi ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari - Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.
Rais Samia pia amemhamisha kituo cha kazi Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Kenan Laban Kihongosi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba Mkoani Songwe akichukua nafasi ya Fakii Raphael Lulandala ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM.
Amemteua pia Elibariki Bajuta, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora akichukua nafasi ya Kihongosi ambaye amehamishiwa Momba.
Amemteua Nyakia Ally Chirukile kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga ambapo akichukua nafasi ya Sixtus Raphael Mapunda aliyehamishiwa Wilaya ya Temeke, kabla ya uteuzi huu Ndugu Nyakia alikuwa Katibu Tawala wa Ngorongoro.