Shigganza
Senior Member
- May 24, 2018
- 160
- 412
Leo tarehe 26 Mei 2019, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuli amekutana na kufanya Mazungumzo na Rais wa Afrika kusini, mhe. Cyril Ramaphosa Ikulu jijini Preteria. Katika Mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine amempongeza kwa kuapishwa kuwa Rais wa awamu ya tano wa Afrika kusini na amemhakikishia kuwa Tanzania itadumisha uhusiano na ushirikiano wa kindugu na kihistoria ulioasisiwa na Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere na Hayati Nelson Mandela kupitia vyama vya ANC na CCM.
Kadhalika mhe Rais alibainisha kuwa anatarajia kukua kwa uhusiano wa Tanzania na Afrika kusini utakua katika masuala ya kiuchumi pamoja Kiswahili. Kabla ya Mazungumzo hayo Wazir wa Mambo ya Nje Palamagamba Kabudi alimkabidhi mhe. Ramaphosa zawadi ya vitabu vya kusoma na kufundishia Lugha ya Kiswahili kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM)
Kwa upande wake Rais wa Afrika kusini alimshukuru Rais Magufuli kwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwake na kufuatia uamuzi wa Afrika kusini kuanza kufundisha Lugha ya Kiswahili, Nchi yake itachukua walimu wa Kiswahili kutoka Tanzania ili watumike kufundisha katika shule za Msingi na Sekondari.
Nampongeza sana mhe. Rais wa ushawishi wake alioufanya ili kurejesha fursa ya Watanzania kupata ajira za kufundisha Lugha ya Kiswahili Nchini Afrika kusini ambayo wakenya walitaka kuijuchukua ambapo hivi karibuni iliripotiwa wakenya kadhaa kuajiriwa Nchini Afrika kusini kufundisha Kiswahili, licha ya ukweli kwamba linapokuja suala la umahiri wa Lugha kitaaluma watanzania tupo vizuri ikilinganishwa na majirani zetu hao kwa kuwa Lugha hiyo ni ya pili kwa Watanzania wengi na inatumika kufundishia kwa elimu ya Msingi, na ni somo mojawapo kwa ngazi ya kidato cha Sita na vyuo vikuu.
Rai yangu ni kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Wizara ya kazi, Ajira na Maendeleo ya vijana, ziandae utaratibu mzuri utakaowezesha kupatikana kwa walimu wenye sifa nzuri na watakapo kwenda huko wahakikishe wanafanya kazi kwa bidii, maarifa na ubunifu ili kujenga imani kubwa kwa Afrika Kusini dhidi ya walimu kutoka Tanzania, wasipofanya hivyo tusishangae, Nchi hiyo ikachukua uamuzi wa kujaribu walimu kutoka Mataifa mengine ambao wanaweza kujituma zaidi ya wa kwetu na hivyo kuchukua fursa hiyo.
Mabalozi wetu mlioko katika mataifa ya Nje wekeni kipaumbele cha kwanza kwenye Diplomasia ya uchumi, kila hafla ya kuapishwa kwa balozi Rais amekuwa anasisitiza mabalozi wetu kusaka fursa za kiuchumi zilizopo nje kwa taifa letu lakini nashawishika kuamini baadhi yao bado wamepiga usingizi wa pono, msaidieni Rais ili Watanzania wengi tunufaike na taifa kwa ujumla.