Rais Omar al-Bashir wa Sudan alazimishwa na Jeshi kutoka Madarakani. Inadaiwa kajiuzulu, Uwanja wa Ndege wafungwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Vyanzo vya habari vinasema Majeshi ya Sudan yachukua udhibiti wa nchi huku Rais Omar al-Bashir akilazimishwa kujiuzulu kwa lazima na kutoka nje ya Ofisi ya Ikulu. Jeshi limepeleka karibu na jumba la rais na Khartoum(Ikulu) na wamezingira tayari huku Maafisa wakuu wa nchi wakiwa wamekamatwa. Hali hii inakuja katikati ya maandamano dhidi ya Rais Omar al-Bashir ambayo yamechukua miezi kadhaa sasa. Tayari uwanja wa ndege wa Khartoum, Sudan Umedhibitiwa na Jeshi.

Vyanzo vya Jeshi vinasema jeshi kama taasisi limeamua kuchukua udhibiti wa Sudan.

TIPS FROM SUDAN

=> Military taking control of country

=> President Omar al-Bashir forced out of power, reports that he resigned

=> Military deploys around presidential palace and Khartoum

=> Senior officials being arrested

=> Comes amid months of protests against President Omar al-Bashir

=> Airport shutdown in Khartoum, Sudan.

=> Sudan's President removed from power

=> Army sources say the military, as an institution, is set to take control of Sudan.



=======

Waziri wa Ulinzi wa Sudan Awad Mohamed Ahmed Auf ametangaza kuwa kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir ameondolewa madarakani na anashikiliwa mahala penye usalama.

Akizungumza kupitia Televisheni ya Taifa ya Sudan waziri huyo amesema kutokana na hali hiyo ametangaza hali ya dharura ya miaka mitatu na amri ya kutotoka nje wakati wa usiku kwa muda wa mwezi mmoja.

Amesema kwamba baraza la mpito linaundwa na litabaki madarakani kwa miaka miwili.

Baraza la mpito

Akilihutubia taifa kupitia televisheni ya taifa Auf alisema baraza la mpito litakuwa na jukumu la kutayarisha uchaguzi utakaofanyika wakati muda wa mpito ukimalizika.

Hata hivyo, wanaharakati waloitisha maandamano ya miezi minne mfululizo dhidi ya Rais Bashir wamepinga taarifa ya waziri wa ulinzi ya kutangaza muda wa mpito.

Wanaharakati hao wa chama cha wafanyakazi ambao ni wanataaluma mbalimbali wameitisha maandamano siku ya Jumamosi na kuwataka waandamanaji warejee tena kukaa nje ya makao makuu ya jeshi hilo wakishinikiza kuundwa kwa serikali ya kiraia.

Awali viongozi wao walisema watakubali tu serikali ya kiraia ambayo itajumuisha viongozi wa upinzani.

Taarifa za kujiuzulu Bashir

Taarifa zaidi zinaeleza Rais al-Bashir amejiuzulu, kufuatia shinikizo la jeshi la nchi hiyo baada ya miezi minne ya maandamano yakipinga utawala wake uliodumu kwa miaka 30.

Chanzo cha habari katika jeshi la Sudan kimeifahamisha VOA kuwa Rais huyo alikuwa kizuizini nyumbani wakati viongozi wa jeshi na viongozi wa siasa Alhamisi asubuhi wakizungumzia utaratibu wa serikali ya mpito.

Kufungwa kwa uwanja wa ndege

Ripoti zinaeleza vyombo vya dola vimefunga uwanja wa ndege mkuu na kuwakamata maafisa na viongozi wa jeshi ambao ni watiifu kwa al-Bashir.

Wakati huohuo Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa vikosi vya Sudan vimefanya upekuzi katika makao makuu ya harakati za Kiislam za Bashir, ambacho kinaendesha chama chake cha National Congress Party.

Hata hivyo msemaji wa chama hakujibu ombi la VOA kutoa maoni yake.

Waandamanaji Sudan wapiga serikali ya muda

Waandamanaji washeherekea

Waandamanaji wamekuwa wakisheherekea nje ya makao makuu ya jeshi mjini Khartoum.

Wanaharakati waloitisha maandamano ya miezi minne hivi sasa dhidi ya Rais Bashir wamepinga taarifa ya waziri wa ulinzi ya kutangaza muda wa mpito.

Kuondolewa madarakani kwa al-Bashir ni baada ya maandamano yaliyoanza kufuatia ongezeko la bei ya mkate, na baadaye bei ghali ya mafuta, na hapo tena upungufu wa chakula na ukosefu wa pesa za kigeni, waandamanaji wakilijitokeza mitaani na kumtaka aondoke madarakani kwa usimamizi mbovu wa uchumi.

Jinsi mapinduzi yalivyoanza

Wakati maandamano yalipoanza, hapo Disema 19, 2018, Bashir, alisema waandamanaji walikuwa vibaraka wa mataifa ya magharibi na kwamba maandamano yao yalikuwa sawa na vilio vya vyura, akisisitiza kwamba mabadiliko nchini Sudan, yangeweza tu kutekelezwa kwa njia ya kidemokrasia.

Al-Bashir alichukua madaraka mwaka 1989 kutokana na mapinduzi yaliyofanywa na chama cha Kiislamu na mara moja kutangaza hali ya dharura kote nchini katika juhudi za kukandamiza upinzani.

Mapinduzi Sudan : Bado waandamanaji hawajaridhika, wanataka serikali ya kiraia

Imetayarishwa na Mwandishi Abdushakur Aboud, Washington, DC.

Mfahamu Omar al-Bashir, kiongozi aliyetawala kwa mkono wa chuma Sudani

Rais wa Sudani aliyepinduliwa na jeshi Alhamisi wiki hii, Omar al Bashir alizaliwa mwaka 1944 katika familia ya wakulima kaskazini mwa Sudan, ambayo pia ni sehemu ya ukoo wa ufalme wa Misri.


Alijiunga na jeshi la Misri akiwa kijana mdogo na kupanda ngazi ya uongozi wa jeshi hilo, katika vita dhidi ya Israel mwaka 1973.

Aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka mnamo mwaka 1989 na alichukua madaraka wakati Sudan ilikuwa ikikabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Kaskazini na Kusini kabla haijagawanyika (Sudani na Sudani Kusini).

Lengo lake lilikuwa la kuunganisha Sudan, lakini kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu kujitenga kwa Sudan Kusini ilifikiwa kama sehemu ya mkataba wa amani, na hivyo ndoto yake kuzima. Hata hivyo licha ya kutofikia ndoto yake ya kuunganisha Sudan alipongezwa kwa kukubali bila upinzani wowote eneo la Kusini kuwa taifa huru na hivyo kuitwa Sudani Kusini.

Japo alikubali kujitenga kwa Sudani Kusini, aliendelea kulitazama kwa jicho la ajabu jimbo la Darfur - ambalo lilikumbwa na machafuko kuanzia mwaka 2003.

Omar al-Bashiri alishtumiwa na jamii ya kimataifa kuuunga mkono wanamgambo wa kundi la Janjaweed linalotuhumiwa kwa kutekeleza uhalifu wa kivita dhidi ya jamii ya Waafrika weusi katika eneo hilo.

Tuhuma zinazomkabili Omar al-Bashiri

Mauaji ya kimbari



Kuwaua watu wa jamii ya Fur, Masalit na Zaghawa



Kuwasababishia mafadhaiko makubwa ya kimwili na kiakili



Kuwaweka katika hali ngumu kwa kuwaharibia makaazi yao


Uhalifu dhidi ya binadamu

Mauaji



Kumpoteza mtu



Kuwahamisha watu kwa nguvu



Ubakaji



Mateso


Uhalifu wa kivita

Kushambulia raia katika jimbo la Darfur



Kuiba mali katika miji na vijiji


Omar al Bashir kwa sasa anazuiliwa na jeshi, washirika wake wa karibu wanaendelea kutafutwa
 
jeshi la Sudan limemtoa madarakani Rais wa Sudan,Omary Al Bashir mda si mrefu uliopita,waziri wa ulinzi na baadhi ya maofisawa kisiasa wamewekwa chini ya ulinzi,huku ikulu ya sudan ikizungukwa na magari ya kijeshi mapema asubuhi hii
 
wenzetu wameweza
Screenshot_2019-04-11-08-53-29.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Omar al-Bashir is the 7th President of
Sudan. He led a military coup to
overthrow Prime Minister Sadiq al-Mahd
in 1989. Since then he has been elected
3 times as President in elections that
have been under scrutiny for electoral
fraud. He is now losing power to a
military coup.
 
Vyanzo vya habari vinasema Majeshi ya Sudan yachukua udhibiti wa nchi huku Rais Omar al-Bashir akilazimishwa kujiuzulu kwa lazima na kutoka nje ya Ofisi ya Ikulu. Jeshi limepeleka karibu na jumba la rais na Khartoum(Ikulu) na wamezingira tayari huku Maafisa wakuu wa nchi wakiwa wamekamatwa. Hali hii inakuja katikati ya maandamano dhidi ya Rais Omar al-Bashir ambayo yamechukua miezi kadhaa sasa. Tayari uwanja wa ndege wa Khartoum, Sudan Umedhibitiwa na Jeshi.

Vyanzo vya Jeshi vinasema jeshi kama taasisi limeamua kuchukua udhibiti wa Sudan.

TIPS FROM SUDAN

=> Military taking control of country

=> President Omar al-Bashir forced out of power, reports that he resigned

=> Military deploys around presidential palace and Khartoum

=> Senior officials being arrested

=> Comes amid months of protests against President Omar al-Bashir

=> Airport shutdown in Khartoum, Sudan.

=> Sudan's President removed from power

=> Army sources say the military, as an institution, is set to take control of Sudan.
Shida kubwa hata wakimwondoa anaekuja ni dictator tena
 
Back
Top Bottom