Rais Mstaafu Kikwete ashiriki Kikao cha Kamati ya Uandishi wa Bunge la Katiba ya Libya

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,961
2,138
Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika utatuzi wa mgogoro wa Libya ameshiriki Mkutano wa Kamati ya Uandishi ya Baraza Maalum la Uandishi wa Katiba ya Libya (Constitution Drafting Assembly) unaoendelea mjini Salalah, Oman. Mkutano huo uliohudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdallah na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler.

Katika Mkutano huo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameelezea dhamira ya Umoja wa Afrika kuona kuwa mgogoro wa Libya unapatiwa suluhisho la kudumu.

Amewakumbusha wajumbe wa mkutano huo kuwa jawabu la matatizo ya Libya ya hali ya usalama na changamoto zake liko mikononi mwao. Amewakumbusha dhamana kubwa iliyo juu yao na matarajio ya wananchi wa Libya kwa wajumbe hao kupawapatia Katiba ambayo itatoa majawabu kwa changamoto za Libya na kulinda haki na usawa kwa makundi yote.

Rais Mstaafu Kikwete pia amepongeza jitihada za Umoja wa Mataifa chini ya Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler za kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro wa Libya kupitia Mkataba wa Amani wa Libya (Libya Political Agreement) uliotiwa saini tarehe 17 Desemba, 2015 huko Shkirat, Morocco.

Amehimiza wadau wa pande zote za siasa nchini Libya kutekeleza makubaliano hayo ikiwemo kuundwa kwa serikali na kusimikwa kwa serikali hiyo yalipo makao makuu ya nchi hiyo mjini Tripoli mapema iwezekanavyo.

Mwakilishi huyo wa Umoja wa Afrika amewahakikishia wajumbe hao utayari wa Umoja wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Falme za Kiarabu (Arab League) na wadau wengine wote kusaidia jitihada za wananchi wa Libya kurejesha hali ya usalama, amani na utulivu nchini Libya.
c1aeb488-3276-4b0c-8936-7f9b29cad240.jpg

Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika utatuzi wa mgogoro wa Libya akiongea katika Mkutano wa Kamati ya Uandishi ya Baraza Maalum la Uandishi wa Katiba ya Libya (Constitution Drafting Assembly) unaoendelea mjini Salalah, Oman. Pamoja naye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdallah na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler.
b912f56d-7410-48b4-bfd6-b8df2d06d0dc.jpg

Picha ya pamoja ya Mkutano wa Kamati ya Uandishi ya Baraza Maalum la Uandishi wa Katiba ya Libya (Constitution Drafting Assembly) unaoendelea mjini Salalah, Oman.

Chanzo: Michuzi
 
Heee, mwakubwa hayo tena jamani, kashindwa nyumbani kwake kusimamia na kutengeneza katiba mpya na nzuri, sasa eti kwenda kuisaidia Libya kutengeneza katiba mpya, mama yangu weee, kushnei!!
 
Wako busy kusuluhisha wenzao wakati kwao hata kufanya attempt tu wa naona shida!!
 
Atakuwa alipanda emirates, mzee wa msoga kwa kupenda kupanda ndege hakuna anayemfikia teh teh teh teh
 
Heee, mwakubwa hayo tena jamani, kashindwa nyumbani kwake kusimamia na kutengeneza katiba mpya na nzuri, sasa eti kwenda kuisaidia Libya kutengeneza katiba mpya, mama yangu weee, kushnei!!
Hizi sanaa
 
Kuna mtu kaweka Uzi humu kuwa wafrica tumelaaniwa naanza kukubaliana nae. Mfano mwingine Ni mseven na mkapa kusimamia demokrasia Burundi wakati wao Ni madikteta kwenye nchi zao
 
Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika utatuzi wa mgogoro wa Libya ameshiriki Mkutano wa Kamati ya Uandishi ya Baraza Maalum la Uandishi wa Katiba ya Libya (Constitution Drafting Assembly) unaoendelea mjini Salalah, Oman. Mkutano huo uliohudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdallah na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler.

Katika Mkutano huo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameelezea dhamira ya Umoja wa Afrika kuona kuwa mgogoro wa Libya unapatiwa suluhisho la kudumu.

Amewakumbusha wajumbe wa mkutano huo kuwa jawabu la matatizo ya Libya ya hali ya usalama na changamoto zake liko mikononi mwao. Amewakumbusha dhamana kubwa iliyo juu yao na matarajio ya wananchi wa Libya kwa wajumbe hao kupawapatia Katiba ambayo itatoa majawabu kwa changamoto za Libya na kulinda haki na usawa kwa makundi yote.

Rais Mstaafu Kikwete pia amepongeza jitihada za Umoja wa Mataifa chini ya Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler za kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro wa Libya kupitia Mkataba wa Amani wa Libya (Libya Political Agreement) uliotiwa saini tarehe 17 Desemba, 2015 huko Shkirat, Morocco.

Amehimiza wadau wa pande zote za siasa nchini Libya kutekeleza makubaliano hayo ikiwemo kuundwa kwa serikali na kusimikwa kwa serikali hiyo yalipo makao makuu ya nchi hiyo mjini Tripoli mapema iwezekanavyo.

Mwakilishi huyo wa Umoja wa Afrika amewahakikishia wajumbe hao utayari wa Umoja wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Falme za Kiarabu (Arab League) na wadau wengine wote kusaidia jitihada za wananchi wa Libya kurejesha hali ya usalama, amani na utulivu nchini Libya.
View attachment 331188
Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika utatuzi wa mgogoro wa Libya akiongea katika Mkutano wa Kamati ya Uandishi ya Baraza Maalum la Uandishi wa Katiba ya Libya (Constitution Drafting Assembly) unaoendelea mjini Salalah, Oman. Pamoja naye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdallah na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler.
View attachment 331187
Picha ya pamoja ya Mkutano wa Kamati ya Uandishi ya Baraza Maalum la Uandishi wa Katiba ya Libya (Constitution Drafting Assembly) unaoendelea mjini Salalah, Oman.

Chanzo: Michuzi
Dah Natamani kama wangekuja kutupa support kuandika pia Katiba ya Warioba ambayo imeshindikana.
 
...naona kapata platform ya kuonyesha at least anashiriki kwenye maongezi ya amani ya Libya....maana nlikuwa najiuliza ni wapi anaweza kuonekana angalau anashiriki shida za Libya....haswa ukizingatia kuwa kule Libya sasa moto unawaka kati ya makundi ya kivita ya ISIL, alqaeda..na mengine tele....wote wakipigania nafasi ya kutafuna keki ya Libya iliyoachwa na mtemi Gaddafi......
 
Haiwezekani kuusuluhisha ule mgogoro kwa sababu Boeing na Lockeheed Martin wameshaanza kuigombania tenda ya kutengeneza ndege zitakazotumika katika uvamizi wa Libya.

Hizo ndege watatumia jeshi la anga la nchi gani. US?
 
Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika utatuzi wa mgogoro wa Libya ameshiriki Mkutano wa Kamati ya Uandishi ya Baraza Maalum la Uandishi wa Katiba ya Libya (Constitution Drafting Assembly) unaoendelea mjini Salalah, Oman. Mkutano huo uliohudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdallah na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler.

Katika Mkutano huo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameelezea dhamira ya Umoja wa Afrika kuona kuwa mgogoro wa Libya unapatiwa suluhisho la kudumu.

Amewakumbusha wajumbe wa mkutano huo kuwa jawabu la matatizo ya Libya ya hali ya usalama na changamoto zake liko mikononi mwao. Amewakumbusha dhamana kubwa iliyo juu yao na matarajio ya wananchi wa Libya kwa wajumbe hao kupawapatia Katiba ambayo itatoa majawabu kwa changamoto za Libya na kulinda haki na usawa kwa makundi yote.

Rais Mstaafu Kikwete pia amepongeza jitihada za Umoja wa Mataifa chini ya Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler za kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro wa Libya kupitia Mkataba wa Amani wa Libya (Libya Political Agreement) uliotiwa saini tarehe 17 Desemba, 2015 huko Shkirat, Morocco.

Amehimiza wadau wa pande zote za siasa nchini Libya kutekeleza makubaliano hayo ikiwemo kuundwa kwa serikali na kusimikwa kwa serikali hiyo yalipo makao makuu ya nchi hiyo mjini Tripoli mapema iwezekanavyo.

Mwakilishi huyo wa Umoja wa Afrika amewahakikishia wajumbe hao utayari wa Umoja wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Falme za Kiarabu (Arab League) na wadau wengine wote kusaidia jitihada za wananchi wa Libya kurejesha hali ya usalama, amani na utulivu nchini Libya.
View attachment 331188
Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika utatuzi wa mgogoro wa Libya akiongea katika Mkutano wa Kamati ya Uandishi ya Baraza Maalum la Uandishi wa Katiba ya Libya (Constitution Drafting Assembly) unaoendelea mjini Salalah, Oman. Pamoja naye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdallah na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler.
View attachment 331187
Picha ya pamoja ya Mkutano wa Kamati ya Uandishi ya Baraza Maalum la Uandishi wa Katiba ya Libya (Constitution Drafting Assembly) unaoendelea mjini Salalah, Oman.

Chanzo: Michuzi

JK wampuuze kwani uzoefu alionao kwenye kuandaa katiba ni figisufigisu na kuchakachua; hana lolote!
 
Back
Top Bottom