Rais Magufuli: Utawala wangu sitaki kulimbikizia watu vyeo. Mbunge hawezi kuwa RC au DC

Ni kweli kabisa. Hii falsafa ihamishiwe mpaka kwenye chama. Haiwezekekani mtu anakuwa anakuwa mbunge halafu hapohapo yeye ni Mwenyekiti wa CCM )(W). Au mtu anakuwa Msemaji wa Chama halafu yeye ni Mbunge. Na hilo nalo tulione hadi kwenye ngazi ya Mwenyekiti wa CCM (Taifa), haiwezekani mtu awe yeye Rais halafu ahodhi uenyekiti wa Chama!
je rais kuwa mwenyekiti mtahoji?
 
hao w
Vipi wanajeshi aliowateua kuwa Wakuu wa mikoa,wilaya Ma RAS?
Hao wanafanya kazi hizo walizoteuliwa nazo tu, watarudi Jeshini pale tu uteuzi wao huko utakapobadilishwa!!! Ni tofauti wabunge waliokuwa wakiteuliwa kuwa RCs/DCs walkuwa wanafanya vyote kwa wakati mmoja
 
Rais wa Tanzania John Magufuli ametangaza kuwa katika utawala wake hatateua mbunge kuwa mkuu wa Mkoa au Wilaya. Amesema lengo ni kuboresha utendaji kazi na uwajibikaji, kwamba "Haiwezekani katika watanzania mil. 50 tukose watu hadi turundie watu vyeo.

Tunataka tuchape kazi kwa ufanisi na ufanisi hauwezi kuja kwa kumrundikia mtu vyeo".

HAYO NDIO MANENO YA MAGUFULI RAIS WETU.
Kampa mtu za USO hapa!
 
Vipi wanajeshi aliowateua kuwa Wakuu wa mikoa,wilaya Ma RAS?
Bora hao kwa sababu wanakuwa wameacha utumishi wao wa kwanza kuliko hawa mawaziri wanaokula pesa za uwaziri na ubunge kwa pamoja, achilia mbali wale wanaokula na za kamati za bunge kama wenyeviti. Yaani mbunge anaweza kuwa DC/RC halafu hapo hapo ni waziri mwandamizi halafu pia ni mkuu wa mkoa, achilia mbali cheo anachoweza kukipata kwenye chama chake! Hii ipo Tanzania pekee ambapo wasomi wenye shahada za uzamivu wanalia kwamba hawana ajira huku form four au six anahodhi vyeo vyote hivyo.
 
Mbona kuna baadhi ni wabunge then ni mawaziri!? ingekuwa fair wabunge waachwe wawakilishe wananchi ili wajitenge na wasiwe sehemu ya serikali...
Wakati mwingine kukaa kimya kama huna la kusema si mbaya mkuu. Katiba inasema waziri atachaguliwa ama kuteuliwa kutoka ktk wabunge waliochaguliwa ama kuteuliwa na Rais. Haihitaji degree kujua hili ama kama unaona ukikosa kucomment utaonekana hujui.
 
Ni kweli kabisa. Hii falsafa ihamishiwe mpaka kwenye chama. Haiwezekekani mtu anakuwa anakuwa mbunge halafu hapohapo yeye ni Mwenyekiti wa CCM )(W). Au mtu anakuwa Msemaji wa Chama halafu yeye ni Mbunge. Na hilo nalo tulione hadi kwenye ngazi ya Mwenyekiti wa CCM (Taifa), haiwezekani mtu awe yeye Rais halafu ahodhi uenyekiti wa Chama!
Yaani umeona kwa ccm tu?mbowe mwenyekiti wa maisha,mbunge,KuB
 
Kuna katuni moja ya Msanii GADO wa DW iliniudhi!!
Eti MPJ ni Mtuhumu, Mwendesha mashtaka, Hakimu, Bwana JELA na eti huenda akawa msoma misa siku ya mazishi!
 
Back
Top Bottom