Rais Magufuli ukimaliza vyote usisahau kuwatumbua green guards wanatisha mno

Chura

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
1,345
2,296
Katika nchi ambazo haziheshimu demokrasia wala utawala wa sheria, wapinzani ni fungu la kukosa. Huweza kupigwa na polisi au vikundi vya vijana wa vyama tawala na wasiwe na mahali pa kushtaki.

Hivyo ndivyo inatokea Burundi, ambako chama tawala cha CNDD-FDD kina tawi la vijana liitwalo imbonerakure linalopiga wapinzani na hawashitakiwi kokote.

Nchini Botswana kimewahi kuwapo kikundi cha Boy Brigades; Malawi ya enzi za Bakili Muluzi, chama chake cha UDF kilikuwa na Young Pioneers wakati DPP ya Bingu wa Mutharika ilianzisha Young Democrats sawa na Zanu-PF ya Zimbabwe yenye Green Bombers au Green Guards wa Tanzania.

Vikundi hivyo, ni matawi ya vyama tawala, vitalu vya kulea viongozi wa baadaye na kueneza siasa. Majukumu yasiyo ya wazi ya vikundi hivyo ni kuendesha vitisho, kuwazingira na kupiga na kuwavuruga wapinzani; wanasiasa, viongozi wa dini, wanaharakati na waandishi wa habari wanaopinga serikali, huku vikikingiwa kifua na Serikali sidhani kama vitaendelea kuwa na nafasi katika serikali yenye mwenyekiti mcha MUNGU na mwenye kuogopa dhambi.

Wapinzani katika nchi zinazoendelea watalalamika, watalia na huenda wakakimbilia polisi wengine ndo kabisa wakaamua na kupanda ndege kwenda kushitaki the hague ila mwisho wa siku inakua ni ushuzi wa futari ambao siku zote haukarahishi daku yani hakuna ufuatiliaji.

Kwa kuwa vikundi hivyo, hupewa nguvu na vyama tawala, hutekeleza uhalifu huo kwa uwazi bila kuzuiwa wala kukamatwa na Jeshi la Polisi.

Kwa mfano, wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Marekani na Jumuiya ya Kimataifa wametoa wito tawi la imbonerakure livunjwe lakini wahusika wameziba masikio kwa pamba.Matamko ya Jaji Mutungi, aliyeteuliwa Agosti 2013 kushika wadhifa huo ulioachwa na John Tendwa, mara zote huwa yanavilenga vyama vya siasa vya CUF, ambacho inadaiwa kina kikundi cha Blue Guards na Chadema yenye Red Brigade.

Hata hivyo, kikundi cha ulinzi na usalama chenye madhara makubwa mpaka sasa katika jamii na ambacho Jaji Mutungi hakizungumzii kabisa ni Green Guards kilicho chini ya chama tawala CCM.

Wapinzani wamelalamikia Green Guards kwamba wanateka na wanatesa, lakini mamlaka nchini, Jeshi la Polisi na Msajili wa Vyama vya Siasa hawalaani wala kufanya juhudi zozote wahusika wakamatwe na kushitakiwa. Green Guards wametajwa kuhusika katika matukio mengi ovu katika chaguzi mbalimbali za viongozi nchini.

Moja ya matukio mabaya kutokea kipindi cha 2015 ambacho Jaji Mutungi akiwa msajili ni kutekwa, kupigwa na kudhalilishwa kwa mbunge wa viti maalum, Rose Kamili (Chadema) katika uchaguzi mdogo Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa Aprili mwaka juzi. kwa masikitiko alisema mama huyo “Wamenipiga, wamenidhalilisha vya kutosha,” alisema mbunge huyo huku akitokwa na machozi. “Walipanua miguu yangu na kunikanyaga sehemu za siri". Kama angekuwa mwanamume sijui angekuwa katika hali gani?” alihoji. Kamili alisema vitendo hivyo vilifanywa na walinzi wa CCM, wanaojulikana kwa jina la Green Guards na alifanyiwa unyama huo ndani ya ofisi ya chama hicho Mkoa wa Iringa na vilishuhudiwa na Mwenyekiti wa CCM wa Iringa, Jesca Msambatavangu. Mbali ya kupigwa aliporwa Sh350,000, Pauni 500 za Uingereza na simu mbili. Msambatavangu alikiri chama hicho kumshikilia Kamili. Lakini Polisi walipoarifiwa, walifika na kumweka ndani mbunge huyo kwa madai alikuwa anatoa rushwa, suala la kupigwa halikuwa ajenda.

Mbunge huyo aliachiwa kwa dhamana. Hadi leo hakuna mwanaCCM yeyote wala kijana wa Green Guards aliyekamatwa.

Tukio la pili kutokea Jaji Mutungi akiwa madarakani ni la kupigwa hadharani mgombea urais, Dk Mussa Kalokola kwa madai aliingilia mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya mgombea mwingine mjini Tanga. Licha ya picha za video za tukio hilo kusambazwa mitandaoni zikiwaonyesha vijana hao wa Green Guards wakimpa mkong’oto mgombea huyo, ambaye inaelekea hakuwa kipenzi chao, na japo lilifanyika peupe, mbele ya viongozi wa CCM mkoani Tanga na mbele ya polisi waliopangwa kulinda usalama, mpaka leo hakuna kijana aliyekamatwa kwa mahojiano.

Haikuwa bahati mbaya Polisi kutoshughulikia matukio hayo, bali ni mazingira maalumu yaliyojengwa kulinda mikakati ovu ya Green Guards. Machi 2013, watu wasiojulikana walitengeneza picha ya video(haya ni madai kutoka CHADEMA kuwa video hiyo ilitengenezwa kuna uwezekano pia ikawa ni ya kweli) wakaiweka kwenye mtandao kuonyesha Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare alikuwa anapanga njama za kudhuru watu, alikamatwa siku ya tatu tangu picha iwekwe, lakini picha halisi zinazoonyesha Dk Kalokola akigalagazwa na Green Guards si ushahidi kwa polisi.

Oktoba 2011 katika uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga, yalitokea matukio mawili ya kutisha. Mosi, ni kuuawa kwa mfuasi wa Chadema, Mbwana Masudi, mkazi wa Dar es Salaam; na pili, kumwagiwa tindikali kada wa CCM aitwaye Mussa Tesha. Mpaka leo Polisi hawakujishughulisha na kifo cha mfuasi wa Chadema isipokuwa walihangaika kuchunguza na hatimaye kuwakamata vijana watano wa Chadema iliowashtaki kwa masuala ya ugaidi.

Jumamosi Novemba 14, 2015.Tukio lingine lililogusa hisia na laana nyingi ni lile la kifo aliyekua mwenyekiti wa Chadema mkoani Geita Ndugu Alphonce Mawazo ambaye aliuwawa kikatili kwa kupigwa mapanga na vijana wanaosadikiwa kuwa ni green guards jambo ambalo polisi walilikanusha.

Machi 31, 2012 usiku wa kuamkia uchaguzi wa marudio katika kata 27 nchini, wabunge wawili wa Chadema; Salvatory Machemli wa Ukerewe na Highness Kiwia wa Ilemela mkoani Mwanza walipigwa na Green Guards tena mbele ya polisi.

Kati yao Kiwia aliumizwa vibaya kichwani, lakini mpaka leo hakuna aliyekamatwa licha ya mtuhumiwa (jina limehifadhiwa) kujeruhiwa, kwa bahati mbaya, na wenzake na hivyo pia kulazwa Hospitali ya Bugando.

Siku hiyo, ndiyo mwenyekiti wa Chadema kata ya Usa-River, wilayani Arumeru mkoani Arusha, Msafiri Mbwambo (32) aliuawa kwa kuchinjwa kama kuku, katika tukio linalohusiana na uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki na Joshua Nasari wa Chadema alishinda.

Zabron Yussuf
, mmoja wa makada wa Chadema waliokwenda kupambana na waliokuwa wamemteka Mbwambo ili wamwokoe, alimwagiwa tindikali. Watuhumiwa wa matukio hayo, wanaodaiwa kuwa ni Green Guards hawajakamatwa.

Ieleweke hakukuwa na namna ya kuzungumzia rekodi hatarishi za green guards bila kuhusisha na Chama Tawala na matukio yote yanayofanyika aidha kwa tuhuma au uhalisia yanayoendeshwa na Green guards mengi ni katika kipindi cha uchaguzi na kwa sababu hiyo moja kwa moja maswahibu yamekua yakiwapata wapinzani wa karibu wa CCM kwa mwaka husika tangu kuasisiwa kwa kikundi hiki.

Hatari nazoziona mosi ni usalama wa chama husika na wanachama wake Vijana wanalipwa na makada wenye pesa kwa maana hiyo ni kwamba kuna Kipindi flani baadhi ya vijana wa Green guards wataanza kutumika kwa masilahi ya vigogo hao wa Chama sio kwa maslahi ya Chama bali kwa maslahi yao binafsi kama kupunguza ushindani kwa ujumla usalama wa wana CCM wenyewe ni dhahiri utakuwa mashakani .

Pili ni usalama wa Taifa leo CCM ipo madarakani ina uwezo wa kulipa vijana hao je pindi itakaposhindwa kuwalipa vijana hawa wenye mafunzo ya kijeshi na taaluma ya ngumi(martial arts) kuna hatari kubwa wazee wa mapangoni Amboni wakaongezeka hivyo kuiweka rehani amani ya nchi myetu iliyotukuka
Leo tunawalipa tunawaita walinzi siku tukishindwa kuwalipa tutashindwa kuwaita magaidi???
 
Back
Top Bottom