galindas
JF-Expert Member
- Mar 3, 2013
- 978
- 1,304
Umesema vizuri mkuu. Kama vyama vyote vingechachamaa kudai haki za wanachama wao serikali ingesikiliza tu. Tukumbuke umoja wetu ndio nguvu yetu. Watumishi wote nchi hii wakigoma serikali haitakuwa na namna zaidi ya kulipa stahiki zao.Afadhali yao hao waalimu walau viongozi wao wanajinasibu kuwatetea. Viongozi wa vyama vingine hawasikiki kabisa utafikiri hawapokei makato ya wanachama. Nina wasiwasi sana na mienendo ya hivi vyama vya wafanyakazi, wanachama mwishowe wataona hakuna haja ya kuchangia chama kisichoweza kuwatetea. Haiwezekani wafanyakazi wanakatwa madeni ya mikopo ya HESLB kinyume na kiwango walichoafikiana napia zaidi ya kiwango cha makato halafu hivyo vyama havikemei wala kuwatetea.
Sent from my TECNO P5 using JamiiForums mobile app