Rais Magufuli: Mimi ni Rais kweli kweli, jiwe. Sitishwi wala sitishiki; azindua kiwanda cha Alizeti mkoani Singida

Kwa wanaoangalia ZIARA ya MHESHIMIWA RAIS mkoani singida tumemsikia WAZIRI MWIGULI akifunguka ukweli juu kilicho jificha kwa sasa ndani ya nchii yetu juu hizi vugu vugu kwa sasa zinazochagizwa na WAPINZANI WASIOITAKIA MEMA NCHI YETU mfano UTEKAJI,MAUAJI.....maandamano yanayoandaliwa hapo 26/04/2018...kasema ni ukweli usiopingika haya mambo ya kutisha kabsa yanatokea kwa sasa baada ya WAPINZANI wa NCHI HII kukosa hoja za kisiasa juu ya serikali iliyopo madarakani na matokeao yake wanatafuta njia mbadala ya kuchafua picha ya SERIKALI YETU mfano kuitisha maandamano yasiyoruhusiwa KISHERIA na wao kutumia mwanya huo kufanya mauaji na mwisho wa siku kuihusisha serikali iliyo madarakani...
Propaganda hizi ebu acheni jamani!!. Yaani tuna TIS pili hata miili inayookotwa hatujasikia status ya kinachofanyiwa kazi. Tatu itakuwa big failure kwa TIS pamoja na jeshi LA police linalojinasibu kwa umahiri kwenye kulinda usalama wa raia kwamba matukio kama haya wameshindwa kukamata hata mbwa aliesababisha mauaji hayo yote. We will never step ahead kama mpo kwa ajili ya kuficha ukweli wa serikali inayoyafanya kwa wananchi. Alafu mnasimama majukwaani na kujinasibu kuilinda amani ya nchi!! Kwendraaaaaa wasindaki nyie.
 
mpuuzi tu huyo....

anatafutiwa kosa, nafasi ya uwaziri imemshinda... soon utaona barua toka magogoni yenye saini ya kijazi kwamba bwana mkubwa amemtumbua.
Kati ya mawaziri waliofeli na ambao kwa vyovyote watapumulia the Hague ni huyu Mwigulu Nchemba ana madoa mengi sana na sijajua kwanini bado wanaendelea kumwachia wizara kama hii!!, labda kwa sababu ni moja kati ya watu walio na uwezo wa kuishi katika hali ya unafiki.
 
Kama hatishiki kelele za nini majukwaani. Atulie dawa iingie vizuri
Huyu kiumbe kuna mahali kuna kasoro si bure
Mange anawayambisha kweli kweli....
 
Mara kazi ngumu,mara mniombee,mara nilisukumiziwa,mara mini JIWE.Mara dereva wa Lori
IMG_20180311_075154.jpg
 
Wakuu, kwajinsi ninavyo ona mienendo na kauli za Rais akiwa Jukwaani, napata shida kumwelewa.

Leo kasema hatishiki, mara kamfokea jamaa mmoja alie kuwa na bango akamwambia akamwonyeshe baba ake.

Nina wasiwasi huko mbeleni Rais atatoa tusi kubwa hadharani.

Naomba wanasaikolojia wamsaidie.
 
waeleweshe, hata kikwete alizindua miradi ya mkapa, na kwa taarifa tu magufuli akikaa miaka 10 atakuwa amazindua na kuanzisha miradi mikubwa kuliko raisi yoyote tanzania
Sijui unaishi wapi ndugu. Huoni biashara zinafungwa wew unashabikia u zuzu
 
ulimsindikiza kuchukua form? kugombea ? alishasema hapangiwi.....

kumbuka nadhan ilikuwa kule bandarini alisema sometimes anakuwaga na stress kwa hiyo tumsamehe kwa kauli zake......

doooh choo cha kike hiki.
 



Rais Magufuli leo hii anazindua kiwanda cha mafuta ya Alizeti mkoani Singida Mount Meru Millers baada ya kutoka mkoani Geita akiwa anazindua miradi mikubwa ya barabara.

Waziri wa viwanda na biashara Mh Charles Mwijage:Singida ina viwanda 543 lakini kiwanda kikubwa ni kimoja tu.

Wabunge wa Singida: Watahakikisha wanamlinda kwa nguvu zao zote Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na hata kuku hawataandamana na chochoko zote zile ndani na nje ya CCM zitadhibitiwa.

=====

Rais Magufuli: Amesema kuwa Waagizaji wa mafuta ghafi kutoka nje wamekuwa wakifanya ushawishi kwa wabunge ili kupunguziwa kodi au kutokulipa kabisa

Kutokana na mchezo huo aliouita kuwa mchafu ameziagiza mamlaka husika kutoka kodi kubwa kwa mafuta ghafi yanayoagizwa

Rais Dkt. Pombe Magufuli amesema uwepo wake madarakani ni kutaka kuwatoa watanzania katika shida mbalimbali walizokuwa nazo na kuwapelekea eneo ambalo watakula raha ili siku atakapokuja kufa basi hata Mungu ampe nafasi ya kuwaongoza Malaika mbinguni.

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza na wananchi wa mkoa wa Singida muda mchache kabla ya kukizindua kiwanda cha mafuta ya Alizeti Mount Meru Millers kilichojengwa mkoani humo.

"Nataka niwahakikishie watanzania kuwa mna Rais kweli kweli, jiwe kweli kweli. Sitishwi wala sitishiki mimi jukumu langu ni kwaajili ya watanzania, nikuhakikisha nawavusha watanzania kutoka mahali kwenye shida na kwenda mahali kwenye raha. Ninajua hiyo ndio itakuwa sadaka yangu kwa watanzania ili kusudi hata siku moja nikienda huko mbinguni Mungu atakaponihitaji, akanichague kutokana na mimi nilikuwa kiongozi mzuri hivyo unaweza hata kuongoza Malaika polepole kwasababu ninajua kuna maisha baada ya maisha ya hapa duniani", amesema Dkt. Magufuli.

Pamoja na hayo, Dkt. Magufuli ameendelea kwa kusema "ndio maana nawaomba sana viongozi wa dini, masheikh na wale watu mbalimbali katika imani zao tuitangulize Tanzania kwanza, tusitumike".

Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Maguli amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujikomboa na kujiongezea kipato cha maisha.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa hakuna maandamano yatakayofanyika, hakuna ruhusa ya kuandamana wala sehemu ya kufanyia maandamano

Hata ikitokea watu waandamana chumbani kunguka kitanda, ikitokea mmoja akaumia basi aliyewaita atawajibika

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amesema amemuagiza na kumuelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kuwakamata watu wote ambao wamepanga njama za kutaka kuwauwa watanzania katika maandamano ambayo wameyapanga kuyafanya

Mwigulu ametoa hiyo wakati alipokuwa akitoa salamu zake kwa Rais Dkt. Magufuli aliyopo Mkoani Singida katika ziara yake ya kikazi ambapo leo hii (Machi 11, 2018) amezindua kiwanda cha Alizeti Mkoani humo na kusema kinachotafutwa katika maandamano hayo ni namna ya watu wanatakanywa tawanywa ili kusudi waje kulalamika kuwa serikali ndio imeuwa watu wake.

"Njama hiyo tumeiona na mimi nimemuelekeza IGP Sirro kwamba hata kupanga njama ya kuua ni kosa, wachukue hatua kwa wale watu wanaopanga mipango ya aina hiyo na kuchafua taswira ya nchi yetu ama kwa mipango yao au ya wale wanaowatuma. Watu wanataka mikusanyiko ili wafyatue na kuuwa watu ili kuchafua taswira ya nchi yetu na tunayo mifano wa maeneo waliwahi kufanya jambo la aina hiyo na hatua zitachukuliwa", amesema Mwigulu.

Pamoja na hayo, Mwigulu ameendelea kwa kusema "Mhe. Rais ndio maana unaona vinyago vinyago vingi hivi kama hivi juzi alitokea kijana mdogo amesema ametekwa, eti ametekwa na akapata muda wa kutafuta pafyumu na nguo za kubadilishia kule atakapokuwa ametekwa. Unatowa wapi muda wa kujiandaa ?, watu wanatafuta njia za kuchafua taswira ya nchi yetu, na jambo hili Mhe. Rais kama ambavyo ulishatoa maelekezo, si jambo ambalo tutacheza nalo wala mjadala, hakuna sababu ya maandamano wala hakuna sehemu ya kuandamania na hakuna ruhusa ya kuandamana".

Aidha, Waziri Mwigulu amesema endapo ikatokea hata watu wakaandamana ndani ya nyumba zao bado sheria itachukua mkondo wake dhidi ya watu hao.

"Ikitokea hata watu wakaandamana ndani ya nyumba wakazunguka kitanda na akatokea mtu akaumia, yule aliyeitisha waandamane pale atakuwa nala kuajibika kwasababu watu wanafanya mzaha na maisha na dira ya nchi yetu ambapo Rais umejitoa muhanga kwa ajili ya kutengeneza urithi wa watoto wa Tanzania", amesisitiza Mwigulu.

Kwa upande mwingine, Waziri Mwigulu amesema yeyote atakayethubutu kutaka kuharibu taifa la Tanzania kwa kufanya vitendo vya uovu hawatoweza kumuacha salama.




This yelling fest shows he is weak to the core!

"The loudest one is the weakest in the room"-Frank Lucas (Denzel Washington)-The American Gangstar!
 
Back
Top Bottom