Rais Magufuli, kuwapunguzia mshahara walio juu ili uwaongezee wa chini ni sawa, lakini...

Rais yuko sahihi labda namna alivyoeleza kuna watu walikuwa wanaongeza mshahara kwa kusingizia hali ngumu mfano tumeouona kwa wabunge lakini nini matokeo yake kulikuwa na mfumiko mkubwa wa bei kwani mwenye nyumba alipandisha kodi, mfanyabiashara alipandisha bei za vyakula kila huduma ilipanda bei lakini akianza kupunguza hiyo mishahara mikubwa wale wanaopata mishahara hiyo wataanza kuwafikiria watu wanaopata mishahara midogo walikuwa wanaishije maana sasa hvi watu bila aibu wamekuwa wakijipandishia gharama za huduma bila kuangalia mwananchi wa kawaida kipato chake kikoje .
Lakini pia rais atapunguza malalmiko toka sekta nyingine ambazo zimekuwa zikidai zimedidimizwa
Sasa tutaona kasi ya Msechu kujenga nyumba zinazoangalia tabaka la kati na juu atamuuzia nani
 
40M KWA MWEZI? HILI NI JIPU MH. MAGUFULI LITUMBUE MAPEMA SANA. MI NAKOMAA NA PHYSICS FORM FIVE NA SIX KUWAFUNDISHA WAJE KUWA WATAALAMU WA KULISAIDIA HILI TAIFA LAKINI NAAMBULIA 500000 TU. USAWA UKO WAPI WANDUGU?
Kazi ya CEO wa NHC si ilitangazwa ktk magazeti? Mbona hukuapply upate 40m unabaki kufundisha physics wanfunzi wako wanakuja kukupita mshahara?
 
Nimemsikia Leo Rais wetu alipokuwa mwanza kuwa atawapunguzia mshahara watumishi wa umma walio na mshahara mikubwa.

Rais ametoa mfano kuwa kuna watumishi wanalipwa mil 40 kwa mwezi, jambo lililo onekana kumkera. Hata Mimi limenikera kwani ni unyonyaji.

Hofu YANGU NI kuwa kwakuwa umewatangazia, watajipanga kwa kukopa hadi mwisho wa kukopesheka, ili ukiwapunguzia wanaleta muongozo wa Hazina wa 1/3 ibaki kama sehemu ya mshahara. Japo sina hakika kama hii ni KWA watumishi wote au ni KWA walimu tu.

Tambua Rais wangu hawa watu wamesoma, ndio wanao tuibia KWA kutumia vema ELIMU zao NA kalamu.

Huo ni mtazamo wangu unge kaa kimya ili suala hili ulifanye kama ambushing yaani shitukizo, hapo wasingekuwa NA muda wa kujipanga.
Robin hood of now days, safi sana sio jambo baya kupunguza gap iliyopo maana hali ilivyo ina katisha tamaa mtu anapokea 40 ml. monthly wewe unaondoka na laki 3 halafu kwa ubinadamu wetu bado akifikwa na msiba uka mchangie.
 
kwani JPM ndiyo Lowasa? au aliwahi kuahidi wapi atafanyia kazi ahadi za Lowasa.
Sasa nini kinamuwasha kuzungumzia mishahara ya watu kuwa mikubwa ili hali wa kwake nao ni mkubwa ila ameuficha???

NONSENSE mwambieni atoe kwanza KIBANZI CHAKE ndio azungumzie boriti zetu!
 
Kazi ya CEO wa NHC si ilitangazwa ktk magazeti? Mbona hukuapply upate 40m unabaki kufundisha physics wanfunzi wako wanakuja kukupita mshahara?
Hizo nafasi hutangazwa ili kuwaridhisha wenye uelewa mdogo kama wewe.

In reality watu huandaliwa mapema na kutangaza ni uzugaji tu.
 
Hiyo haiwezekan taratibu za utumishi wa umma hazisemi hivo hta muundo wa utumishi haupo hivo,haiwezekan mim nipo TGTS I(2800000/=) kwa mwezi unipunguzie mpka TGTS D(730000/=) kwa mwezi.
Magufuli hafati taratibu mkuu yeye anataka kuweka sawa mambo tuu..
 
Mshahara wa mtu ni swala la kikatiba na kisheria na bahati nzuri lina kinga nzuri sana kisheria. Sitegemei Rais avunje sheria.
Swala la mishahara mikubwa lina chimbuko lake ila limewekwa kama watu wanajilipa. Sivyo. Hakuna mtu anayejipangia maslahi yake. Mtu hupewa na mamlaka ya juu yake.
Pia wapo watu wametafutwa kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kujaza mapengo ya kiutaalam na uzoefu uliokuwa unahitajika. Huko walikotolewa walikuwa na mishahara yao mikubwa. Ili wakubali kuja ilibidi makubaliano maalum yafanyike. Watu hawa walioshawishiwa wakaacha kazi zao huko kuwaachisha bila muafaka ni kukaribisha kesi kwenye mahakama ndani na nje ya nchi.
Ukishampa mtu mkataba ni haki na huwezi kuivunja kwa jazba. Mtalipa watu bila kazi. Uangalifu unahitajika.
Baki hapo hapo bwana magu yupo above the law behind the scene...
 
Mshahara wa raisi mtu mmoja ukipunguzwa we itakusaidia nn, kuwen na akili unapo post, jamaa ana lengo kwa watumishi wa chini na ndio wengi na wanaofanya kazi ngumu kuwaongezea mshahara ni jambo jema,sio kila kitu kupinga tu,toeni mawazo mema keki ya nchi inufaishe kila mmoja sio wachache
 
Kwa hili namuunga mkono kabisa utakuta mtu anapokea m1 kazi anayofanya ndogo tu muda mwingi yupo inst,fb,whatsap oficin lakini mwingine analipwa laki 3 muda wote kutembea tu na kufanya kazi ngumu, hapo kweli kuna hakiii?jpm vivaaa ukifanya hilo watumishi wa chini tutakuombea udumu kuifanyia nchi yetu memaa
 
Mshahara wa raisi mtu mmoja ukipunguzwa we itakusaidia nn, kuwen na akili unapo post, jamaa ana lengo kwa watumishi wa chini na ndio wengi na wanaofanya kazi ngumu kuwaongezea mshahara ni jambo jema,sio kila kitu kupinga tu,toeni mawazo mema keki ya nchi inufaishe kila mmoja sio wachache
tulia hivyo hivyo ikuingie vizuri
kwani JPM ndiyo Lowasa? au aliwahi kuahidi wapi atafanyia kazi ahadi za Lowasa.
 
Kwani unaujua mshahara wa Rais ni shs. ngapi? Rais kuamua kupunguza mishahara mikubwa tayari keshaonyesha uzalendo na kutetea wanyonge. Ni aibu, dhuluma na wizi mtupu kwenye nchi yenye walalahoi wanaoshindia mlo mmoja kwa cku kama viboko, mfanyakazi wa serikali anapokea mshahara wa 40m kwa mwezi. Yaani anapata milioni na zaidi kwa siku! Waliopanga hiyo mishahara hawana uzalendo kabisa, ni majipu ya aina yake!


Magufuli anapokea millioni 400 kwa mwezi!! Yaani analamba zaidi ya milioni 10 kwa siku. Sasa kama huu si UFISADI ni nini?
 
MAGUFULI ANASHAURIWA NA NANI ??? KWENYE HILI KAKOSEA SANA ........

MIMI NADHANI AFANYE TOO AUDITING KUONDOA WATU AMBAO WANALIPWA KWA MIKATABA MINONO LAKINI HAKUNA KAZI WANAYOFANYA ...LAKINI KWA KWELI KUNA WATU AMBAO WANASTAHILI KABISA MALIPO MAKUBWA....NA HATA UKIWAONDOA UNAWEZA KUJIKUTA UNAJIUMIZA
 
Sawa ipo kisheria ila kwa manufaa ya wote hizi sheria kandamizi, unyonyaji na upendeleo Zifumuliwe haraka. Mhasibu wa halmashauri, wizara ana tofauti gani na Wa Sumatra au TPA? Makusanyo ya taifa wote tugawane sawa. Nyerere said" Haiwezekani wengine kuishi kama hayawani wakati wengine wanajifaidisha na pesa ya serikali.""
 
Nyerere alifanya hivyo lakini matokeo yake yalikuwa mabaya. Yeye aliweka mshahara wa juu kabisa kuwa ni wake wa Shs 5000. Mwaka 1973 aliweka kodi ya ajabu kabisa. Marginal rate ya mshahara wa 20 000 Iilikuwa 95%....

Nadhani Magufuri alikuwa na maana ya wale akina Msechu and the like ambao wanajilipa 40M+ kila mwezi. Anataka awashushe ''warudi duniani''. Nina uhakika kama watakuwa na jeuri ya kukataa mshahara wa M15 kwa mwezi, kuna nyomi yenye uwezo sawa na wao itakuwa tayari kuwareplace kwa kasi ya ajabu.
 
wakuongezea waongezewe ila asimpunguzie mtu ataleta mvutano. anasema hatakuwepo mtu wa kulipwa zaidi ya mil 15, labda aanze na mawaziri na makatibu wake then afuate wabunge ila asiguse misharaha ya wetu wenye taaluma zao

Taaluma ya kukopa benk na kujenga magorofa mbona kila mtu anaweza,mtanyooka tu everyday is not friday
 
Back
Top Bottom