Rais Magufuli: Kama umesoma 'private school' atakayekupa mkopo ni kichaa

its non sense,

mtaji wa maskini ni nguvu zake au akili zake kichwani. Kama huna nguvu na akili kumkichwa ni za kupima na kijiko basi tukuombee mungu tu.
 
we need competence and not sympathy.
kila mwanafunzi bila kujali kasoma wapi, lazima apimwe na wezake na aonekane kuwa na uwezo wa kudeliver.
sio huruma.
 
Hivi ni kweli kama sababu ya kupewa mikopo
au kutopewa ni uwezo wa mzazi ndio unaoangaliwa,
tukichunguza vyuo vikuu vyote humu nchini na nje yanchi,
ni kweli hakuna watoto wa wenye vyeo serikalini
wanaopata mikopo?
Na je kama tutaamua sote tupeleke watoto wetu shule
za serikali rais atatuhakikishia kwamba watoto wetu
wakifika chuo kikuu watapata mikopo?

Mimi nadhani hekima itumike zaidi ,kwamba wale wenye
uwezo wajitahidi kuhudumia familia zao
ili kutoa nafasi serikali ihudumie zaidi jamii duni
ambayo wengi wanaangukia kwenye fungu hili.
 
Baada ya kuzuia watoto wa matajiri kusomeshwa Chuo Kikuu na Serikali yetu ambapo ni jambo jema, hatua ya pili iwe kwenye ajira hasa Serikalini na Mashirika ya Umma kwamba kipaumbele na upendeleo wa makusudi vitolewe kwa aliyesoma Shule za Kata mpaka Chuo Kikuu, kama akikosekana alipitia Shule za Kata mwenye ujuzi unaotakiwa ndiyo waangaliwe waliosome Shule binafsi, ...
Je serikali inaweza kugharamia Elimu ya watoto wote kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu?
Watu wana mawazo ya kurudi back square one (Ujamaa uliomshinda Nyerere). Kazi ipo!
 
Si azifute kabisa shule za private,Magufuli asione hawa watoto wanaosoma private schools kwamba wazazi wao wana kipato kikubwa la hasha, wengine wanasomesha kwa kudunduliza mno,wanakosa mahitaji mengine kwa ajili ya kuwalipia watoto wao ada,lakini kuna factor ya hali ya maisha kubadilika,mzazi anakuwa na unafuu wa maisha muda fulani lakini kuna wakati mambo yanagoma na hapo mtoto anatakiwa kudahiliwa kujiunga Chuo Kikuu,hiyo pesa ataitoa wapi? Magufuli anatakiwa kuyatafakali hayo aliyoyasema maana hata hao anaowapa mikopo ni kwa pesa ya walipa kodi wa Tanzania ama wenye watoto walioko vyuo vikuu au wasio na watoto.
 
Baada ya kuzuia watoto wa matajiri kusomeshwa Chuo Kikuu na Serikali yetu ambapo ni jambo jema, hatua ya pili iwe kwenye ajira hasa Serikalini na Mashirika ya Umma kwamba kipaumbe, ...
yani hao wenye elimu zinazoeleweka kama havard na oxford hawafai eeh??
 
Soma nilichoandika kama ukipenda, nimesema kama wote wana vigezo sawa basi wa Shule za Kata apewe upendeleo maalumu!
sidhani kama kuna kitu kama hicho.
kipimo cha vigezo sawa ni nini mkuu.
vyeti, au matokeo ya usahili.
pia unachoshauri unataka kiwekwe kwenye SOP za uajiri au wapendelee kiujanjaujanja bila kuwepo na maandishi ya kuwaback up.
 
Hivi jamani tuwe wakweli tu. Umesoma Marian au Canossa au FEZA hadi form 6. Unashindwaje kulipa ada ya chuo ambayo mara zote kwenye Vyuo vingi iko chini ukilingqnisha na Secondary School za Private?
Kuna wengine mazingira yao yamebadilika-kwa mfano aliyemsomesha amestaafu na mafao yake ni duni, wengine walikuwa wanasaidiwa na ndugu ambao sasa hawana tena ule uwezo.
Pili ni wazi issue siyo ada ya chuo tu, kuna fedha za kujikimu, malazi, nauli, michango ya moja kwa moja na mingine, etc hizi ukiongeza kwenye ada usishangae cha private aliesoma kikawa kidogo. Wengine wanapata watoto zaidi wanaohitaji elimu hivyo uwezo wa kuhudumia wote unapungua na kuleta hitaji la mkopo. Lakini pia kwa makato ya sasa kama mzazi ana uwezo atamliapia mtoto wake kupunguza maumivu huko mbeleni. Si dhani kama wanao omba kwa ajili ya kuomba tu wako wengi kiasi hicho.
 
Oh basi sawa mkuu ila ye amesema pale me. Sjaona makosa....
Kama upo shortsighted pia si rahisi kuona makosa. Suala la elimu sio la kucheza nalo. Tulidhani tunaelekea kwenye elimu bure had vyuo vikuu. Ila kwa mtazamo huu. Tutasubiri sana
 
Lazima atambue ya kwamba Hela hizo zinazopatikana kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa vyuo ni kodi za wananchi,sasa yeye anataka kujiamulia tu Hvi kuna watu wanashindwa kumshauri rais......naona Hata Bunge linashindwa kuingilia kati Suala hilo!

Ova

CCM wanamuogopa huyu dikteta kumshauri na nafikiri hashauriki huyu. Uamuzi huu utawaumiza hata wao CCM kwa kuwa na wao wanao watoto wanaosoma private schools tena wengi. Lakn dawa ni kuikomoa CCM kwenye uchaguzi wa 2020. Mkuu wa kaya anafanya kama kwamba hizo pesa anazitoa mfukoni mwake. Tutaisoma namba sote aliye CCM na asiye CCM.
 
Sijajua kama Mhe analifikiria hili jambo sawa sawa. Kwani Wapo watu tunaishi nao wameshatumbukia kwenye umaskini kwa kusomesha watoto wao private, nia ya wazazi hawa haikuwa mbaya lakini sasa uchumi wao imeyumba ukisema hauwapi mkopo sababu tu walisoma private unawanyima haki hao watoto. Suala hili liangaliwe upya.

Wazee wa busara walio CCM jitokezeni kumshauri huyu jamaa anaipelekea nchi pabaya. Naamini ndani ya CCM kuna watu vichwa vzr, wenye mwono na fikra huru na wanaokubalika pande zote kwa wapinzani na kwa CCM. Sasa jitokezeni wazee nyinyi mumshauri huyu jamaa, nchi anaiplekea pabaya. Naamini hata nyinyi wa CCM mnao watoto mnawasomesha kwenye private schools, basi tumieni busara zenu kumshauri huyu jamaa kwani pesa hazitoki mfukoni mwake, sote tunalipa kodi.
 
Mwambieni sisi tunakomaa tu, tunawasomesha private school na university tutalipia tu, kumchukia mwenye nacho haikufanyi wewe kuwa na ahueni kimaisha huo ni upuuzi tu

Hatujali tena.... Namsomesha mwanangu private na akifika chuo anakwenda soma kwa pesa yangu c kwa mikopo yenu ya pasua kichwaaa... We fAnya utakavyo

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app

Wakuu wangu mko sawa kwa kujiangalia hali zenu, utata unakuja kwa wale ambao walipitia private schools na hali za kifadha za wazazi/ walezi/wadhamini zimebadilika. Hawa ndiyo wanao umia zaidi kwa kukosa mikopo. Ni watanzania wenzetu inabidi tuwatetee wasikose elimu kwa kuwa tu wakati fulani walisomea private.
 
Kwenye issue ya baadhi ya vyuo vya private kutolewa macho sana nakuunga mkono..kuna vyuo vimezuiliwa kudahili kisa kukosa sifa,lakini kwa uchunguzi wangu mdogo tu,nimeona kama ni isssue ya kubana wasipate mkopo..vyuo vingi bongo,standard haitofautiani sana,japo mapungufu yapo,ila sio ya kumsababishia kijana asipate elimu,inayoweza kuja kulisaidia taifa baadae..

Nafikri utaratibu huu wa watoto wengi walioosoma Private schools kukoseshwa mikopo haujaanza leo wala jana. ulikuwepo na labda haukuwa rasmi. Mwanangu mwk jana hakupewa mkopo hata senti moja na amepata div 2. Badala yake mimi na mama yake tumekopa kutoka kwa ukoo wetu ili mtoto asome. Alhamdulillah yko chuo lakni baada ya shida kubwa sana. Sasa kauli ya mkuu wa kaya aliyoitoa juzi SUA labda ni ku- formalize uamuzi huo thakili na usiozingatia utu na haki ya watanzania.
 
Aliye Ccm asiye Ccm lazima # ataisoma tu kwa maamuzi haya

Ova
 
Huu ni ubaguzi wa kiwango cha juu kabisa, sikutegemea kusikia kutoka kwa mkuu wa nchi.
Mimi nilitegemea, na wala sishangai...hivi kweli hutegemei kusikia kauli kama hizi toka kwa Magu? Upo hapa hapa duniani!!
 
Wakuu wangu mko sawa kwa kujiangalia hali zenu, utata unakuja kwa wale ambao walipitia private schools na hali za kifadha za wazazi/ walezi/wadhamini zimebadilika. Hawa ndiyo wanao umia zaidi kwa kukosa mikopo. Ni watanzania wenzetu inabidi tuwatetee wasikose elimu kwa kuwa tu wakati fulani walisomea private.

Kwa mfano kama mimi nimestaafishwa mwaka huu na mafao sijapata. Sasa nitapata wapi pesa za kumsomeshea mwanangu mwengine nikikosa mkopo ambao ni haki ya mwanangu apatiwe kwa vile ni mtanzania na wazee wake tumeliipa kodi. Maamuzi mengine ya kijinga sana, mtu anaamka na frustration zake na anaamua bila ya kufanya rational choices, matokeo yke maamuzi anayoyafanya yanaamiza wengi.
 
Back
Top Bottom