Rais Magufuli atishia kuteua Mkuu wa Magereza kutoka JWTZ

Najaribu kufikiria hapa, je JWTZ kwa ushirikiano na JKT wakishindwa kukamilisha ujenzi huo na Mh. Rais akatembelea mradi huo, je atatoa tamko kama hili?

Je nini itakuwa muitikio wa Jeshi kwa kauli hizo?
Wewe! Wameshasema jeshi halishindwi!
 
MAGEREZA NAO, HIVI KUNA HAJA GANI YA KULALISHA WAFUNGWA SAA KUMI WAKATI WANAWEZA KUWAPANGIA SHIFT WAKAPIGA MZIGO MASAA 24,WASINGEKUA WANALIA MAMBO YA MAJENGO WALA CHAKULA!
Hujui ulisemalo, hiyo bajeti ya mafuta, cement, n.k utawapa wewe?!
Hata mafuta ya kupeleka wafungwa mahakamani hawana,
Uniform hawana, zimechakaa balaa, viatu hawana
Serikali imepeleka bajeti kubwa sana JWTZ na TISS kwa kuwa inaogopa kupinduliwa.
Polisi rushwa inawabeba balaa.
Zimamoto ndio taabani kabisa.
Kama Magereza wangewezeshwa wangefanya makubwa.
Nenda gereza la Songwe, Ngwala, Karanga na kadhalika uone kazi zao.
Hakuna uzalishaji bila kuwezeshwa.
Kuhusu hayo majengo sio wao waliopewa hiyo kazi, kazi walikabidhiwa TBA, Magufuli anatafuta tu namna ya kumtumbua huyu Kamishna mkuu wa Magereza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Magufuli amesema hayo baada kutembelea ujenzi wa Nyumba za askari magereza Ukonga na ule wa Magomeni kota.

Miradi yote miwili imesimama bila sababu za kueleweka ukumbukwe ujenzi wa nyumba za Askari Magereza unasimamiwa na Magereza wenyewe na Mradi wa Magomeni kota unasimamiwa na TBA

Hata hivyo Rais amewanyang'anya Magereza mradi huo na kuwakabidhi JWT waumalizie

Nb: humu JF kuna uzi unaongelea miradi ya serikali ya Magufuli iliyokwama sababu ya ukosefu wa fedha na hiyo miradi imetajwa humo naona ndio uliomwamsha Mzee toka Magogoni na kufuatilia utekelezwaji wake.

Huu ni mwendelezo wa madudu tu,
Ishu ya kikokotoo cha mafao,boss wa SSRA,akatolewa kafara,wakati Yeye ni mtekelezaji tu wa mambo yaliyoamuliwa na Baraza la mawaziri.
Ishu ya korosho,ni madudu matupu,mpaka Leo,ni mishuzi tu,inawatoka.
Sasa ishu ya TBA,mzee baba,anahasira,mambo hayaendi,sasa anatafuta "punching bag" ili angalau asikike,maana ile kauri mbiu"hapa kazi tu"haisikiki tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
General makakala anafaa sana kuwa mkuu wa magereza, huyu mkuu ni mbunifu na ameenda shule, kwa sasa ni balozi wetu nchini zimbabwe.
 
Udhaifu wa Magereza ni udhaifu wa Serikal sio wa Magereza yenyewe

Mh. Rais Mara kwa Mara amekuwa alikisifu Jeshi la Wananchi (JWTZ) kwa ubora wa Kazi Na Nidhamu yao lakin lazima tujue hayo Ni Matokeo ya uwekezaji Mkubwa Sana uliofanyika JWTZ especially wakati wa Utawala wa Mwanajeshi wa Zamani Jakaya Mrisho Kikwete

Rais Magufuli wakati akiwa Bagamoyo akishuhudia mazoezi ya Kwenye Maji ya JWTZ aliwahi kujikuta anasema Jk Kwenye Majeshi kafanya wonderful job ambayo ndio leo inawafanya wawe bora

Moja ya udhaifu Mkubwa wa Jk ilikuwa kulipendelea mno Tena Mno JWTZ kiasi kwamba uwekezaji uliofanyika JWTZ Ni zaid ya 80 ya Uwekezaji uliofanyika Kwenye Majeshi yote Kama utajumlisha uwekezaji Kwenye Majeshi yote kuanzia Rasilimali watu, Elimu, Nyenzo Za Kazi n.k

Magereza Na Zimamoto walisahauliwa Sana wakabaki Nyuma

Udhaifu wa Magereza hauwezi kuondolewa kwa kuleta Kamishna Jenerali toka JWTZ

Tuwawezeshe kabla ya kuwasimanga
Nasikia wanataka magereza kuzalisha mazao ambayo watauza nje ya nchi,hapo hapo magereza hawana magari ya kubebea mazao na Kila kitu kinachohusiana na usafiri,je hilo litawezekana?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujui ulisemalo, hiyo bajeti ya mafuta, cement, n.k utawapa wewe?!
Hata mafuta ya kupeleka wafungwa mahakamani hawana,
Uniform hawana, zimechakaa balaa, viatu hawana
Serikali imepeleka bajeti kubwa sana JWTZ na TISS kwa kuwa inaogopa kupinduliwa.
Polisi rushwa inawabeba balaa.
Zimamoto ndio taabani kabisa.
Kama Magereza wangewezeshwa wangefanya makubwa.
Nenda gereza la Songwe, Ngwala, Karanga na kadhalika uone kazi zao.
Hakuna uzalishaji bila kuwezeshwa.
Kuhusu hayo majengo sio wao waliopewa hiyo kazi, kazi walikabidhiwa TBA, Magufuli anatafuta tu namna ya kumtumbua huyu Kamishna mkuu wa Magereza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu wa magereza si kamchagua juzi tu?anataka mwangushia jumba bovu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, Rais kasema hazina walitoa 10 billions kwa TBA ili nyumba ziishe.. Toka 2017 mpaka Leo hazijaisha.. Ndo mana jeshi linapewa tenda kwa hela zilizopo kwenye budget ya 10 billion...


Amiri jeshi mkuu kasema kama Kuna ubadhirifu umetokea kwenye hizo 10 billions basi wahusika watalimia Meno.
Hivii walitakiwa kufanya hiyo kazi kwa vyanzo vyao vya mapato au kuwezeshwa na hazina?

JWTZ watapewa fungu la hiyo kazi au watajitegemea?

TBA alikuwa kawekewa pesa kwenye akaunti akawa anaiangalia tu badala ya kuifanyia kazi,au aliibadhirifu?

Hivi nani vile juzi kaongea juu ya hali ilivyo magerezani kwa ujumla wake?

Naomba jeshi litusaidie tumalizie na zile zetu za wazee wa Magomeni Mapipa,tafadhali.

Tunaunga mkono nia njema na juhudi za serekali yetu ya leo kukabiliana na changamoto za watu wa chini.



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom