Rais Magufuli atembelea Hospitali kuu ya Taifa Muhimbili, Amjulia hali Mufti Mkuu Tanzania

mwaka huu magu ataisoma namba. na wizara ya elimu wanamsubiri. watoto wengi wanakaa chini. pia kuna upungufu mkubwa sana wa walimu wa shule za misingi hasa vijijini....
 
Mungu yu pamoja nae atamjwezeshe kuyashinda yote. Penye NIA pana NJIA.

Watanzania tuyaone haya mambo ni yetu wote, sio kumrushia tu lawama na kumkatisha tamaa Mhe. Rais utadhani hao wanaoteseka na kukaa chini sio watanzania wenzetu. Tujaribu kuweka uzalendo mbele.

Queen Esther

mwaka huu magu ataisoma namba. na wizara ya elimu wanamsubiri. watoto wengi wanakaa chini. pia kuna upungufu mkubwa sana wa walimu wa shule za misingi hasa vijijini....
 
Sasa Mimi ndio huwa sielewi, hapa mambo ya u-kada na u-chama yametoka wapi???

Hivi haya matumizi mabaya ya fedha Mhe. Rais anayoyafanya pamoja na timu Yake bado hujayaona??? Mbona wengine wanalalamika kuwa anabana sana??

Queen Esther

Tatizo la Muhimbili sio inaongozwa na nani. Tatizo ni ipo chini ya mfumo wa uongozi wa nchi gani! Bila kujenga mfumo wa uwajibikaji na kuondoa matumizi mabaya ya fedha hali haitabadilika. Mfumo wa utawala wa nchi yetu unatakiwa ufumuliwe na ujengwa upya... ndipo pa kuanzia. Halafu haya mambo ya u-chama, u-kada haya ni mabaya sana.
 
Nyani Ngabu Vipi tena?? Soma between lines. Ndio maana hizi kazi huwa zinafanyiwa interviews na sina maana mradi una MBA basi uwe CEO Wa Muhimbili.

Naomba mpendwa unielewe.

Queen Esther

Huh?

Wanahitajika watu wenye MBA au wanahitajika watu wenye weledi na uwezo wa kuongoza?

Au ukishakuwa na hizi herufi mbele ya jina lako basi moja kwa moja unapata weledi na uwezo wa kuongoza?
 
Si walisema wamepeleka vitanda vya kutosha na picha zilipigwa mpaka vitanda vingine wanalalia manesi? ? Au yalikua maigizo zile posho za wabunge za kufanyia uzinduzi wa bunge
 
Mungu yu pamoja nae atamjwezeshe kuyashinda yote. Penye NIA pana NJIA.

Watanzania tuyaone haya mambo ni yetu wote, sio kumrushia tu lawama na kumkatisha tamaa Mhe. Rais utadhani hao wanaoteseka na kukaa chini sio watanzania wenzetu. Tujaribu kuweka uzalendo mbele.

Queen Esther
sawa tumuombee. lakini changamoto alizonazo ni kubwa mno sio kwenye kilimo, elimu nk.
 
Kwanza Sijapenda kauli ya kusema Mhe. Atumie akili, kweni unadhani anatumia nini?? Ina maana na washauri wote alionao hawatumii akili???

Pili kuna pesa zinakusanywa Muhimbili kila siku. Umewahi kujiuliza kwa siku wanapata shs ngapi na zinawezaje kutumika???

Kuna haja kila Gari linaloingia Muhimbili liachangie angalau shs 200 ili zitumike kuboresha wodi za wazazi na watoto.

Queen Esther

Katika hali ya kushangaza kwa mara nyingine tena amekuta wodi ya kina mama wanalala chini na hata wengine katika vitanda wanalala watano watano.

Asitpotumia akili Rais Pombe atafukuza watu kila siku na mwisho atajikuta anaajiri mazombi.Muhimbili sio ndogo isipokuwa ni mipango mibovu ya serikali katika huduma za afya.Muhimbili ni hospital ya rufaa lakini ukienda leo utakuta mtu ana busha au jibu anatokea mbagala anaenda muhimbili.Dar ina hospital kubwa tatu za serikali Amana,Temeke na Mwananyamala,ukikaa getini kwenye hospitali hizi kwa siku moja gari la wagonjwa hupeleka wagonjwa muhimbili mara kadhaa ukiuliza utaambiwa ni rufaa.Mgonjwa toka Amana ,Temeke au mwananyamala hupokewa na kutibiwa na madaktari cheo sawa na walio Amana,Temeke,na mwananyamala,je tutaendelea kusema muhimbili ndogo? je Hospitali ya taifa ni ya kutibu majipu? Mr pombe akae vizuri na mwantumu na naibu wake kwani hawana mpaka sasa mtazamo wa kutatua matatizo mengi yanayoikabili wizara ya afya.Mr pombe aiulize wizara inafanya nini sio kufukuza fukuza wataalam na kuwapaka matope kwenye jamii.
Unapokuta mtaalam wa afya analipwa pesa ambayo haiwezi hata kukidhi mahitaji muhimu kwa kada yake unategemea nini?.
Angalia bajeti ya afya ya 2015,unategemea nini?
Angalia manunuzi wizara ya afya,unategemea nini?
Angalia agakhan watu wanavyolipia ulinganishe na wanavyolipia muhimbili,Amana,Temeke unategemea nini?kumbuka huyo anaelipia agakhan ni gharama za serikali.
 
Nyani Ngabu Vipi tena?? Soma between lines. Ndio maana hizi kazi huwa zinafanyiwa interviews na sina maana mradi una MBA basi uwe CEO Wa Muhimbili.

Naomba mpendwa unielewe.

Queen Esther

Ok, sawa. Huku qualify ulichoandika lakini nimekuelewa.

Ila, umeweka msisitizo kwenye MBA kana kwamba ni lazima uwe na hizo herufi mbele ya jina lako ndo uweze kuwa CEO.
 
Zile zilikuwa ni general wodi.

Queen Esther

Si walisema wamepeleka vitanda vya kutosha na picha zilipigwa mpaka vitanda vingine wanalalia manesi? ? Au yalikua maigizo zile posho za wabunge za kufanyia uzinduzi wa bunge
 
Naibu waziri si ndo alionekana anafunga geti eti kudhibiti wanaochelewa kazini? Kumbe semina elekezi ni muhimu
 
mnashangaza sana baadhi ya wachangiaji....tohu....eti lazima uwe na MBA....!...nakupa homework ya kusoma kwanza health delivery system ya nchi yetu ndio uje na MBA zako hapa
 
DUUUU!! My dear, you are very right. Ila Hiyo ni kazi ya Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Wakurugenzi husika. Hiyo siyo kazi ya Rais kabisa.

Queen Esther

Si dhani kama hii si kazi ya rais bali nafikiri ni kazi ya Mh.rais na creaw nzima katika upande wa afya kuweka mikakati ya kusaidia hii sekta. Nafikiri tatizo la cabinet ya Mh. Rais ni kutoelewa muelekeo /maono ya Mh.Magu..yaani wapi anataka kutupeleka na ndio maana unaona Waziri wa afya pamoja msaidizi wake wanakimbizana na Ndugu Mwaka, mara wamefunga mageti mara hiki mara kile maana hawafahamu nini la kufanya.Na hakuna kiongozi anayekuja na mbinu mpya au mawazo mapya ili kuondokana na hadha ya mrundikano wa wagonjwa.

Hapo juu umeongelea swala la akina mama wasio na matatizo kujimfungulia katika hospitali za Wilaya ni wazo zuri ambalo nilitegemea kuona hawa mawaziri wanalifanyia kazi, au kuna wakunga wa jadi au wakunga (manesi)waliostaafu ambao wangependa kuendelea na kutoa huduma ya kuzalisha,hawa watu wanaweza kupewa ujuzi zaidi hii kwa wakunga wa jadi, vifaa vya kuzalisha na wakawa wanazalisha wajawazito wasio na matatizo na mwisho wa mwezi serikali inawalipa kutokana na idadi ya akina mama waliojifungulia hapo..(of course watapewa elimu, kuandaa sehemu safi za kujifungulia, kupewa vifaa vya kuzalisha na nk)

Kwa kufanya hii utapunguza tatizo la akina mama kulala chini, hivyo kuwa na huduma bora kwa akina mama mjamzito, akina mama kuchagua ni wapi wanaona panafaa kujifungulia, kupunguza vifo vingi vya watoto na akina mama hasa wakati wa kujifungua maana unakuta nesi wako wawili ambao wanahitaji kuhudumia akina mama watatu au zaidi kwa wakati mmoja, madk kuwa na muda wa kutosha wa kuhudumia watoto waliozaliwa na matatizo/akina mama waliojifungua na matatizo na nk.
 
Vitanda vinauzwa nini?
Vile vitanda mlivyokua mnavishabikia hadi mkawamnalaza paka wezi vitandani vingine manesi wakawa wanalala mkashabikia kuwa muhimbili mambo super,
Mbuni mnaoficha vichwa chini ya mchanga tunawafurumusha mjue tumewaona mnavyojidanganya kujificha vichwa hili hali miili yenu na makalio yanaonekana with naked eyes.
 
UNA UHAKIKA WAZIRI HAIJUI ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI NA HAJUI NINI CHA KUTEKELEZA??? HIYO NI DHARAU KWA WAZIRI NA TIMU YAKE!!

Queen Esther

Si dhani kama hii si kazi ya rais bali nafikiri ni kazi ya Mh.rais na creaw nzima katika upande wa afya kuweka mikakati ya kusaidia hii sekta. Nafikiri tatizo la cabinet ya Mh. Rais ni kutoelewa muelekeo /maono ya Mh.Magu..yaani wapi anataka kutupeleka na ndio maana unaona Waziri wa afya pamoja msaidizi wake wanakimbizana na Ndugu Mwaka, mara wamefunga mageti mara hiki mara kile maana hawafahamu nini la kufanya.Na hakuna kiongozi anayekuja na mbinu mpya au mawazo mapya ili kuondokana na hadha ya mrundikano wa wagonjwa.

Hapo juu umeongelea swala la akina mama wasio na matatizo kujimfungulia katika hospitali za Wilaya ni wazo zuri ambalo nilitegemea kuona hawa mawaziri wanalifanyia kazi, au kuna wakunga wa jadi au wakunga (manesi)waliostaafu ambao wangependa kuendelea na kutoa huduma ya kuzalisha,hawa watu wanaweza kupewa ujuzi zaidi hii kwa wakunga wa jadi, vifaa vya kuzalisha na wakawa wanazalisha wajawazito wasio na matatizo na mwisho wa mwezi serikali inawalipa kutokana na idadi ya akina mama waliojifungulia hapo..(of course watapewa elimu, kuandaa sehemu safi za kujifungulia, kupewa vifaa vya kuzalisha na nk)

Kwa kufanya hii utapunguza tatizo la akina mama kulala chini, hivyo kuwa na huduma bora kwa akina mama mjamzito, akina mama kuchagua ni wapi wanaona panafaa kujifungulia, kupunguza vifo vingi vya watoto na akina mama hasa wakati wa kujifungua maana kunakuts nesi wako wawili ambao wanahitsji kuhudumia akina mama watatu au zaidi kwa wakati mmoja, madk kuwa na muda wa kutosha wa kuhudumia watoto waliozaliwa na matatizo/akina mama waliojifungua na matatizo na nk.
 
Back
Top Bottom