Rais Magufuli anzisha Taasisi ya Maadili ya Umma

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
MH RAIS NAOMBA UANZISHE TAASISI AU MAMLAKA YA KULINDA NA KUTETEA MAADILI NA UZALENDO KWA TAIFA.
Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mtare John Pombe Magufuli awali ya yote sina hofu toka siku ile Dodoma ulipochaguliwa nilijua mawazo yangu juu ya Taifa langu na masahibu iliyopita sasa yanapata tiba na ujio wa maendeleo kwa Watanzania wote kwa kwenda mbele.Kura yangu dhidi yako ilikua thabiti kutoka moyoni mwangu na mpaka sasa naamini utafanya mengi kwa faida ya vizazi vya sasa na kuandaa mambo mazuri ambayo yatakuja kuwa faida kwa vizazi vijavyo

Hoja yangu ni kuwa Mh Rais wakati unasambaratisha [Dismantle] lile li MFUMO FISADI NA RUSHWA ebu chonde chonde Mh Rais ebu anza kutengeneza Taasisi ambayo kazi yake kubwa itakuwa ni kulinda , kutetea na kuratibu Maadili na Uzalendo wa Umma [Taifa] .[TAASISI YA MAADILI YA UMMA (TAIFA) -KIFUPI – TMT]

Kwanini nasema hili, Taifa linajua kuna TUME YA MAADILI YA VIONGOZI ambayo Kiongozi wake ni Judge Kaganda, lakini kama Taifa hakuna japo Tume Maalumu ambayo wigo wake unalinda maadili ya Taifa kwa ujumla wake kwenye umma, yani tume ambayo ni jicho kwenye umma kwa ajili ya kulinda maadili na Uzalendo wa Taifa.

Taasisi au Mamlaka ya Maadili ya Viongozi inafahamika majukumu yake ni kuona Viongozi wanatii vipi na kushiriki vipi kuwa wasimamizi wa maadili ya Taifa.Lakini wakati huo wale wanao wasimamia hawana Maadili wala chombo cha kusimamia [monitor] maadili yao. Hebu kwa mfano kama swala la kawaida…ebu chukulia mfumo wa shule ya msingi au Sekondali unavyoendeshwa mbali na Shule kuwa na Mwalimu wa Maadili [Sura iwe Kiongozi Wa Umma] Shule ina Kamati za Maadili [Uongozi Simamizi wa Maadili] lakini pia kuna Viongozi wa Wanafunzi nidhamu [Ugatuzi wa Maadili kwenda kwa Wanafunzi] lakini kuna Sheria na Taaratibu kama taasisi simamizi ambayo Mwanafunzi au Mwalimu anapokosea basi kama ni Mwalimu ataperekwa kwenye vikao husika kwa ajili ya kuwajibishwa .Lakini kama ni Mwanafunzi yeye anapokosea basi Shule ujikusanya kama Jamii [School Assembling] kisha uongozi wa Shule utoa tamko na kama kuna adhabu utamkwa mbele ya hadhara husika kuonyesha jinsi gani kama Taasisi nidhamu na utii wa sheria za Shule zinapaswa kuzingatiwa.

Mfano Mwanafunzi kutoku simama na kumsalimia Mwalimu si kosa la moja kwa moja kisheria ya kumfukuzisha Mwanafunzi Shule papo kwa papo lakini ni kigezo tosha cha kuupa uongozi wa nidhamu shuleni kumuadhibu au kumwadabisha Mwanafunzi husika kama kipimo cha utovu wa nidhamu kwenye shule [Kwa Taifa Tungesema Kukiuka Maadili]. Lakini mwendelezo wa Mwanafunzi mwadhibiwa kukutwa na aina fulani fulani tena ya matendo ya kutokusalimia Walimu wake mara kwa mara basi uperekea kufikiwa uamuzi wa kumfukuza Shule kwa utovu wa nidhamu.

KWANINI TAASISI YA MAADILI YA TAIFA.
Kuanzishwa kwa Mamlaka ama Taasisi hii Serikali itapata jicho la kuona maadui wa Taifa kupitia uaribifu wa Maadili ya Umma na Ukiukaji wa Uzalendo kwa Taifa [Hii yaweza kuwa Wizi wa Mali Asili, Tabia na mienendo ya Jamii, Makuzi na Malezi ya Watoto, Maisha ya Vijana na Wazee Kitaifa, Kuangalia Tabia mbaya ambazo zinaweza kushamili kama Uzembe, Wizi, Ulevi, Imani Potofu [Hapa Ujio wa Dini zenye Mwerekeo usio Mwema Kwa Taifa], Uchoyo, Ufisadi, Uzembe, Uzururaji etc. Wakati huo huo kuwa sehemu ya chombo chennye kuhamasisha [Promote] haiba nzuri kwa Taifa, mambo Mazuri ya kuenziwa Kitaifa na kuhakikisha Sheria za kulinda maadili na Uzalendo wa Taifa zinaunndwa na Taasisi hii kuwa ni Bureau ambayo ina uwezo wa kufungua mashitaka dhidi ya raia ama mgeni yoyote ambaye atakuwa amevunja maadili na Uzalendo wa Taifa letu.

Nimevutika kuliona jambo hili kwa jicho la tatu kupitia uamuzi wa Mh Rais JPM kuamua kupambana na Rushwa na Mafisadi kama alivyo toa ahadi wakatika akinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi.Kulikua na malalamiko sana dhidi ya Ufisadi na Rushwa Nchini kabla ya Mh JPM kuingia Madarakani, Ufisadi na Rushwa ulikuwa wimbo wimbo mkubwa sana wa Taifa. Wananchi walikua wanalalamika sana kwa maneno makali, kiasi kuwa kuna watu walibeza Utaifa wao na kujinasibu dhidi ya Mataifa mengine.

Wenye akili waliliona ilo, hatimae Rais mwenye uwezo [GUTS] za kupambana na kilio cha UFISADI NA RUSHWA akachaguliwa na kushika ofisi kuu.La ajabu alipoanza mapambano wale wale waliokuwa wanawaaminisha Wananchi yani umma dhidi ya udhaifu wa Serikali katika kupambaa na Ufisadi na Rushwa wakarudi kuwaaminisha umma tena kuwa yanafanyika maonezi dhid ya wale wote wanao ondekana kuguswa na Serikali kuwa wamechagia ama hasara au mapungiufu ya utekerezaji wa maagizo na shughuri za Serikali Nchini.Baadhi ya Umma kupitia majukwa huru ya Mitandaoni [Socialnetwork] kumeibuka Watanzania wenye kutoa maneno ya hovyo naya kukera kuhusu mustakabali wa Taifa na kutumia uhuru wa majukwaa hayo ya kijamii kuvuluga maadili na Uzalendo kwa Taifa na kuaminisha uvunjifu wa maadili halisi ya Kitanzania yenye kuhitaji staha katika mijadala na mazungumzo mbalimbali iwe ni katika ngazi ya mtu na mtu, familia, kundi, au jamii kwa ujumla wake.

Kwa mwelekeo huo kama Taifa tunahitaji kuwa na msimamizi ambae ana wajibu wa kuona iwe ni vyombo vya habari, taasisi, mtu mmoja mmoja, kikundi cha watu, au kampuni ina wajibika kulinda maadili na Uzalendo wa Taifa na kuwa mstari wa mbele kuakikisha misingi mikuu ya Maadili yetu una imarika toka ngazi ya Familia yani Kaya mpaka ngazi ya Taifa. Sasa hivi ujio wa tekinolojia ya mawasiliano kumelifanya Taifa kuwa Kaya ndani ya Kijiji kimoja yani Dunia.Hivyo taalifa na mawasiliao yanafanyika kwa kasi kubwa sana na hivyo hivyo katika uvunjifu wa Maadili ya Taifa kasi yake ufanywa kwa kasi kubwa sana kupitia mawasiliano.na usambaaji wa taarifa za uharibifu wa Maadili ama kuhujumu Uzalendo wa Taifa [Patriotism] navyo utawanyika kwa kasi sana.

Tunaitaji jicho la Kijamii ambalo ni mfumo wa Kitaasisi au Mamlaka ambao kila mwanajamii atakua anauona kwa jicho la wazi na kuviacha vyombo vya ndani vya kiusalama na Ulinzi kuwa na wigo wa kusimamia mambo ya Ulinzi na Usalama wa Taifa letu katika utaratibu wake ule ule wa mipaka kwa raia wa Kawaida.Kwa kuwa na Taasisi kama tunvyoona TAKUKURU [PCCB] ama MAMLAKA YA BANDARI basi kuwe na Mamlaka ya MAADILI KWA TAIFA. Mamlaka hii itakuwa ni jicho la wazi la Umma kwa Umma juu ya Uzalendo na Maadili ya Taifa bila kujali itikadi bali kuangalia zaidi mustakabali wa Mtanzania katika kuheshimu Mila na Jadi, Desturi, Utamaduni, Nidhamu, Wadilifu, Uzalendo na Heshima ya Taifa lake kokote kule aendako iwe ni ndani ama nje ya Taifa lake. Ni eneo hili tiba yoyote ya jicho la Ukabila ama Dini litaonwa mapema na kuwa na mamlaka au taasisi yenye jicho la kisheria kuwa na uwezo wa kulikabili tatizo kisheria hadharani kwa faida ya Umma na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Taasisi hii itatumika kuwa mhamasishaji [Campaigner or Promoter] na Mtetezi [Advocate] wa maswala ya msingi kuhusu maadili ya Taifa na umuhimu wa Mtanzania kuwa Mlinzi wa Taifa lake zima.


Leo hii Mashrika kumi na Saba [17] ya ulinzi na Usalama wa Marekani yanalalamika uchaguzi wao mkuu uliingiliwa na Urusi kwa kutumia mfumo wa mtandao [Cyber]. Tukienda mbele na kuludi nyuma kumbe mtu wa muhimu pia katika kulilinda Taifa lake ni Mwananchi pia. Waswahili pia usema ‘’Mjenga Nchi ni Mwananchi na Mvunja Nchi ni Mwananchi huyo huyo’’.Hivyo kwa kuwa na Taaisis hiyo itakuwa na dhamiara kuu moja KULINDA NA KUTETEA MAADILI NA KUSHIRIKI KUJENGA UZALENDO WA MTANZANIA KWA TAIFA LAKE. Kazi hii ikiwekwa kwenye sura ya Mamlaka itasaidia sana sana kulejesha Mtanzania mwenye maadili katika maadili yake. Tanzania ilikua na kansa ya Rushwa na Ufisadi sasa Matibabu ya Ugongwa huo yameeanza kuonekaa na yanaendelea …Ugonjwa mwigine baada ya Rushwa na Ufisadi na Maadili ya Umma na Viongozi. Tayari Viongozi wana chombo lakini Umma haua chombo lasmi.


CHOMOBO HIKI KITAKUWA MHAMASISHAJI MAADILI TOKA NGAZI YA KAYA HADI TAIFA
Si ajabu kuwakuta Watanzania Mitaani wanamshabikia Kijana aliyeiba na kufanikkisha maisha yake kwa dhuruma , udanganyifu, ghiriba, utapeli, wizi, kukaba watu nk , lakini wanajamii ugeuka kuwaita wa aina hiyo ni wajanja na kuwa wana uwezo na kwa ushenzi huo ugeuzwa na wanajamii kuwa ni wakupigiwa mfano kama werevu wa kimaisha. Hivyo hivyo imekwenda mpaka kwa kizazi kipya [New generation] inayoingia kwenye sekta ya Umma na Binafsi kama Waajiliwa. Uingia wakiwa na mtazamo [Mindset] ya kuwa Wanaitaji Mafanikio ya haraka kwa kudanganya, kuiba Mali ya Umma au ya Kampuni husika ili wafanikiwe kimaisha kumilki Mali [Materialism] kama Nyumba, Magari, Accounts na vitu mbalimbali ambavyo jamii imevikumbatia kama moja ya ishara za mafanikio katika jamii na kumpa mtu heshima ya kuheshimika kama mtu muhimu katika jamii.

Leo hii familia nyingi za Kitanzania mweye fedha ndiye mtu anaheshimika kuanzia ngazi ya familia yani kaya hadi Taifa,haijarishi fesha hizo au mali hizo kazipataje bali wanachoagalia ni fedha aliyo nayo.Kwa kuacha Taifa kujinasibisha kwa sura hiyo kuna siku umma utakuja kuamini kwa Maharamia, Waalifu Sugu nna Watu wengine mbalimbali ambao wamepata fedha kwa njia haramu zisizo na haki. ‘’HAKI UINUA TAIFA NA BATILI UANGUSHA TAIFA’’ tutumie uwepo wa Taasisi hiyo kusimamia haki ya umma kujisimamia kimaaadili dhi ya Taifa toka ngazi ya familia mpaka Taifa.

Si ajabu kumkuta Mtanzania anasema maneno yasiyo na Staha kama Mtausi juu ya Taifa lake ..hapa sizungumziii kumtukana kiongozi nazungumzia mtu kulitukana Taifa lake katika namna ya kujieleza kukwazika na jambo fulai ufikia hatua ya kulitusi Taifa lake kwa maneno machafu na hata wengine udiliki kuwatukana viongozi wa wakuu wa Kitaifa kama ishara ya kujinufaisha wao binafsi ama Taasisi au mtu wa ziada katika jambo husika.Tunaitaji mwangalizi [Watchdog] wa kisheria mwenye ruksa ya kimamlaka kwenda mbali [Extra Miles] kuona mapungufu na kuyaziba na kupata mapya ya kuyaongezea nguvu yakaimalike kwa umma.
 
Back
Top Bottom