Rais Magufuli amjibu Kikwete kiaina

Amesema ataendelea kusema kwa maendeleo yanayofanyika katika miaka hii minne kulinganisha na miaka zaidi ya hamsini tangu uhuru!

Maendeleo ya ununuzi wa ndege, ujenzi wa zahanati, barabara, elimu bure nk!
Huyu jamaa anaona ndege ni dili sana ee?
Nyau kabisa
 
Huu upuuzi anaosema magufuli kwamba toka uhuru hakikufanyika chochote ndo siasa za ccm siku hizi au una maanisha nini mkuu hapa? Kwamba hiyo PhD yake aliipatia chini ya mti na alijipa mwenyewe kwa kuwa hapakuwa na madarasa ,lecture theater wala walimu na wahadhiri wa kumfundisha kwa kuwa hapakuwa na mtu wa kujenga wala wa kusomesha watanzania.Huyu mtu ukimfuatilia sana unaweza ukahisi tunaongozwa na mteja wa milembe hospital
Hiyo PhD haifanyii kazi ni urembo, na uko sahihi kapewa tu na yeye anatoa fadhila kwa kumpa ulaji aliyempa.
 
Amesema ataendelea kusema kwa maendeleo yanayofanyika katika miaka hii minne kulinganisha na miaka zaidi ya hamsini tangu uhuru!

Maendeleo ya ununuzi wa ndege, ujenzi wa zahanati, barabara, elimu bure nk!
Angekuwepo nyerere angeshamuuwa uyu ibilic
 
Huyu dhaifu uchukue Mkuu? Mlimkosea sana JK naona mnammiss kiani my best president maana alinilipia school fees na nilikuwa nikigoma hana shida ananisikiliza.Live longer JK
I wish 2020 JK achukue fomu, ni kama TZ inamuhitaji tena
 
Mwambie nyerere alinunua ndege 12...
Wengine walienda nazo JFK wakazamia mpaka sasa hawajarudi. Kumbuka wakati wa mwalimu ndege zilienda Heathrow . JFK na kwingine kwingi. Sasa ndege zinaenda wapi zaidi ya SA na kukamatwa? Huko Mumbai zimeenda mara ngapi? Watu tulikuwa tunaenda Lusaka, Lubumbashi na kwingine kwa ATC wakati wa Mwalimu.
 
Tutaanza kwenda Mpanda soon.
 
Amesema ataendelea kusema kwa maendeleo yanayofanyika katika miaka hii minne kulinganisha na miaka zaidi ya hamsini tangu uhuru!

Maendeleo ya ununuzi wa ndege, ujenzi wa zahanati, barabara, elimu bure nk!

Aliwahi kusema amemteua waziri wa uvuvi kichaa kama yeye, sasa huoni maneno mengi anayozungumza kuna element ya ukichaa!!!!
 
Haaahaaa...wanahaha watapataje ulaji waliokuwa wanagombania.
JPM ndo dawa yetu
Majuto ni mjukuu,unajua wasingemkata Lowassa huyu Magufuli hata tano bora asingefika. Watu wa Lowassa walinuna wakakataa kumpigia Membe na wakampigia Magufuli kwa hasira ili wamkomeshe JK.Sasa wanaishia kwenda kuomba misamaha ikulu (Nape),mwingine kakimbia nchi. JK yeye anapiga vijembe. Haisaidii maana JPM tayari ni Rais. Na Rais wa Tanzania ana madaraka yote kama King Suleiman.
 
Taarifa zisizo rasmi jk anaundiwa zengwe ndani ya ccm na kundi la jpm ili aunganishwe Na kina membe. Wakubwa wanasema kusema msingi Wa ccm ni Uhuru Wa majadiliano ndani ya vikao nje ya hapo chama kitapata matatizo kunamlenga jpm na uongozi wake ndani ya chama kuelekea 2020
 
Hahaaaaa 😁nani amekimbia nchi!! Kila zama na kitabu chake maisha ni kama pedal za baiskeli, moja ikiwa juu nyingine taka isitake lazima iwe chini ili mwendo upatikane😆
 
Taarifa zisizo rasmi jk anaundiwa zengwe ndani ya ccm na kundi la jpm ili aunganishwe Na kina membe. Wakubwa wanasema kusema msingi Wa ccm ni Uhuru Wa majadiliano ndani ya vikao nje ya hapo chama kitapata matatizo kunamlenga jpm na uongozi wake ndani ya chama kuelekea 2020
Sio kwamba anaundiwa zengwe. JK ni team Membe kutoka unyayoni mpaka kisogoni. Unaweza vipi kumtenganisha Membe na JK?Kabla JK hajawa Rais uliwahi kumsikia Membe wewe kwenye siasa za Tanzania ? JK alipukuwa Rais ndo alimpa Membe unaibu waziri baadae uwaziri kamili. Hata walipomkata Lowassa waliamini Membe atashinda. Ila Mungu siyo Masanja,akashinda mwingine kabisa.
 
Duh hivi JPM seriously anaamini kabisa kwamba ndani ya miaka yake minne kaleta maendeleo kuliko miaka 50 ya uhuru?
Kwa watoto waliozaliwa ndani ya miaka yake hii minne labda wanaweza kumwelewa.
Anasahau pia deni la Taifa kwa miaka yake hii minne karibu linazidi deni la miaka 10 ya Kikwete. Na hapo anadai tunatumia pesa zetu za ndani kwenye miradi mikubwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom