hugochavez
JF-Expert Member
- Mar 1, 2013
- 1,907
- 1,009
Kwa kipindi kifupi alichokaa madarakani Rais Magufuli ameonyesha uwezo mkubwa sana wa kujenga miundombinu ya Uchumi wa Nchi, ameweza kujenga na kuimarisha mifumo ya utendaji kazi na ameweza kuisimamia ipasavyo. Rais magufuli ameibuka kuwa kinara wa ujengaji uchumi na maendeleo kwa watu wake katika Nchi zinazoendelea kwa maana ya Afrika, Asia na mashariki ya kati.
Moja ya mambo makubwa aliyofanikiwa kuyajenga hadi sasa ni kujenga reli ya kisasa inayotumia umeme itakayosafiri kwa mwendokasi wa kilometa 900 kwa masaa matatu. yaani mtu ataweza kutoka mwanza saa moja asbh na saa tatu asbh atakuwa amefika Dar tofauti na sasa ambapo safari hiyo inachukua masaa 18 hadi 20.
Jambo lingine kubwa ni kufanikiwa kujenga mtandao wa barabara na madaraja yanayounganisha Nchi kuwa moja kutoka kila kona yaani ukitoka Mtwara unafika arusha bila kukanyaga vumbi, ukitoka mwanza unaenda mbeya, hadi songea bila kukanyaga vumbi nk.
Afrika inahitaji Magufuli watano tu kuifikia Nchi ya ahadi.
pichani chini RAIS MAGUFULI AKIKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA DARAJA LA KUPITA BAHARINI KUTOKA COCO HADI AGA KHAN JIJINI DAR ES SALAAM