Rais Magufuli afanya mazungumzo na Bilionea Dangote

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
776
1,330
b2aa3093-25ca-423e-9bc0-04ad326c2fe1.jpg




Rais Magufuli leo Desemba 10 amekutana na kufanya mazungumzo na mmiliki wa Kiwanda cha Dangote Mtwara, Bilionea namba moja Afrika, Alhaji Aliko Dangote.

Rais Magufuli baada ya kufanya mazungumzo na Dangote amesema hapakuwa na tatizo bali watu tu waliotaka kujinufaisha kupitia mradi huo kiujanjaujanja.

Rais amemtaka Dangote kununua gesi moja kwa moja toka TPDC ambacho ni chombo cha serikali badala ya kutumia watu wengine.

Amemhakikishia Dangote serikali itaendeleza mazingira mazuri kwa Wawekezaji ili kutimiza lengo la Tanzania ya Viwanda.
===========================

UPDATE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.

Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini katika kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya Viwanda.

Rais Magufuli amesema kuhusu kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara hapakuwa na tatizo lolote ila kulikuwa na watu ambao walitaka kujinufaisha binafsi kupitia mradi huo kwa kufanya biashara za ujanja kitu ambacho serikali yake haikiruhusu.

Amemtaka Dangote kununua gesi moja kwa moja kutoka TPDC ambacho ni chombo cha serikali badala ya kutumia watu ambao wamekuwa na nia ya kutengeneza faida tu.

''Iwapo unataka maelezo yoyote ama lolote linalokukwamisha uwasiliane na viongozi wa serikali badala ya kuwasiliana na watu ambao wako kwa ajili ya kufanya biashara ya ujanja ujanja kwa lengo la kupiga dili '' amesema Rais Magufuli.

Dokta Magufuli amesema Dangote ametaka eneo dogo ambalo angelitumia kusafirishia saruji yake wakajitokeza watu ambao wametaka kumuuzia kwa shilingi bilioni 43 kitu ambacho hakina uhalisia wowote bali ni watu ambao wanataka kutengeneza faida kitu ambacho hakiwezekani.

Kwa upande wake mmiliki wa Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amefunga kiwanda kwa sababu amekatazwa kuagiza makaa ya mawe toka nje ya Tanzania kitu ambacho amesema hakiingii akilini kwa sababu makaa ya mawe ya Tanzania ni rahisi na yana ubora kuliko kuagiza nje.

Katika kuthibitisha hilo, tayari Mfanyabiashara huyo ameingiza malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake. Ameongeza kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana nchini.

Alhaji Dangote amemuhakikishia Rais magufuli kuwa ataendelea kufanya kazi na Serikali ya Tanzania na kamwe hana nia yoyote ya kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari bali ana mpango wa kuangalia fursa nyingine zaidi za uwekezaji hapa nchini kutokana na uwepo wa sera nzuri za uwekezaji chini ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Katika hatua nyingine Rais Dkt. John Pombe Magufuli amuapisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Olonyokie Ole-Sendeka anayechukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Wengine walioapishwa na Rais Magufuli ni Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye anakuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo (Kilimo), Dkt. Maria Sasabo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Bibi Grace Alfred Martin kuwa Balozi (Mkuu wa Itifaki).

Jaffar Haniu,
Naibu Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU.
Dar es Salaam.

10 Desemba, 2016.
 
Tofauti zipi? Hizi posti za kuwahi bila details ni shiiida sana humu jf .
 
duh ! mi sijaelewa kabisa , sawa na ile thread ya 'siku hizi watu wanapenda kula jicho' , yaani sikuambulia kitu !
 
Kuna baadhi ya watu wanakesha wakimuomba shetani ahakikishe kuwa Serikali ya awamu ya tano haifanikiwi.

Kuna wengine mpaka wamejivika ujinga kuhakikisha tu wawepo kwenye maombi kwa shetani.

Mbaya zaidi, njozi zao kila mara zinatupiliwa mbali pale ukweli unapojipambanua.

Ni hatari kuishi katika matumaini hewa huku yakiendelea kujazwa ujinga na baadhi ya wanasiasa.

Ukweli huwa haupuuzwi na hakuna mbadala wa ukweli.

Dangote case is closed.

Tunasubiri tena bidhaa nyingine ya uongo kuingia mitaani kwa sababu inavyojidhihirisha kwa sasa Tanzania kuna tekinologia mpya ya kuzalisha uwongo.

Ninatumaini kabla bidhaa nyingine ya uwongo haijaingia mitaani, watengenezaji watakuwa wamejifunza sababu ya kutonunuliwa au kuoza haraka bidhaa zao za uwongo.
 
Back
Top Bottom