Rais Magufuli aamuru Ney wa Mitego aachiwe huru na wimbo wake upigwe vituo vyote redio na TV

Raisi magufuli ameuruhusu wimbo wa ney wa mitego wa wapo amesema uendelee kupigwa tu kwani hata yeye ameupenda, kasema auboreshe kwa kuongeza vionjo kama, wapo wauza unga, wapo wala rushwa, wapo wakwepa kodi ña wapo pia wahujumu uchumi ña mengine mabaya pía.
Nukuu kutoka kwa muheshimiwa Prof mwakyembe
 
Mh Rais janja sana I see. Ameona njia rahisi ya kuwapumbaza watu wasiendelee kumfuatafuata Bashite wake, ni kuhamishia movie kwa WAPO ili Bashite asahaulike vichwani mwa watu aendelee kula bata kama kawaida. Hahahahahahahaha!!
 
Kibaya zaidi kuna wanasheria wanajiita nguli walijitokeza kumtetea...kumbe magu keshagundua hilo na kufanya yake...ha ha ha I like my president.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Ney wa Mitego aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi hilo.

Waziri Mwakyembe ameishauri pia BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo huo, na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.

Akiongea na Wandishi wa Habari muda huu mjini Dodoma, Dk. Mwakyembe amesema hata Rais Magufuli amefurahishwa na wimbo huo wa WAPO, na kumshauri Msanii huyo kama inawezekana aendelee kutaja watu wengine kama vile Wakwepa Kodi, Wauza Unga, Wabwia Unga, Wezi pamoja na watu wengine wasio na maadili mema katika jamii.



Nyimbo yenyewe ndio hii



MAONI YA MLETA UZI
Watanzania tumtumie Vizuri huyu Rais kkwa kweli hatakuja kutokea nani alifikiria hili.

BASATA wafunike nyuso zao kwa viganja vya mikono yao kama wale manyani wa Adili na nduguze
 
Hii inathibitisha ombwe la utawala bora na abuse of power iliyotamalaki - amepanda mbegu (bangi) na sasa anaona matokeo yake (ameona anaanza kuvuna bangi). yeye ni alfa na omega! Polisi, mawaziri, wakurugenzi, makatibu wakuu, nk. wanafanya maamuzi (mara nyingi mabaya) wakifikiri wanamfurahisha alfa na omega! Hata uzuiaji wa press conference ya Nape na nguvu kubwa iliyotumika ilikuwa ni bangi hiyo hiyo! Kama ameanza kutambua kosa hili, basi anastahili pongezi.
Sawa, mwenzio kuna kitu sijakielewa

Polisi wamemkamata

Basata nao wametoa maamuzi ya kuifungia ile nyimbo kwa haina maadili

Inamaana hawa watu wawili hapo juu hawakuwasiliana na mkuu wao?

Kwa maamuzi ya mkuu wa kaya yanamaqnisha wamekurupuka,

Yaani mpaka nadata, wacha niishie hapo
 
Back
Top Bottom