Rais kwanini hajamteua mwenyekiti wa TSC? Ni mwaka Sasa tangu aliyekuwa mwenyekiti amalize muda wake

Mangowe

Member
Jul 10, 2023
12
16
Mpaka Sasa Rais hajateua mwenyekiti wa TSC tangu mwaka jana mwezi wa saba 2023 hakuna Aliyethibitishwa kazini kutokana na ukosefu wa mwenyekiti.

Mashauri ya kinidhamu ngazi ya wilaya yamekuwa Mengi mno maana hayawezi tatuliwa maana hakuna kamati iliyoundwa kutokana na itifaki, hata kupandishwa vyeo na madaraja Bado ni Sintofahamu maana haijulikani ni lini Rais ataamua kumchagua mwenyekiti.

Tunampenda Rais na tunashauri asiwe mbali na kundi hili la watumishi (wamepitia wakati mgumu Sana awamu ya Tano sio vyema wakaendelea kupoteza tumaini kwa serikali hii ya awamu ya sita)

Uhamisho wa vituo vya kazi pia ni siasa, mfumo haueleweki na wizara husika haisemi Nini wafanye watumishi sintofahamu ni nyingi mno. Kwanini mamlaka zisiwe huru na Kusema ukweli kwa wananchi?
 
Epuka kutumia vifupisho kama TSC sio kila mtu anaelewa TSC ni nini jamaa
 
Back
Top Bottom