Rais kumteua na kumuapisha Jaji Mkuu ni "Kuitia Mfukoni Mahakama"

ntemintale

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
952
1,872
Haifai na haipendezi Rais kumteua na kumuapisha Jaji Mkuu.

Jaji Mkuu alipaswa kuomba nafasi hiyo na chombo kama kamati ya majaji inampitisha na kumwapisha ili kulinda Uhuru wa Mahakama.

Kwa mtindo wetu huu Mahakama haiko huru kabisa. Yaani mhimili wa Mahakama uko ndani ya Dola/Rais.
 
Uko sahihi, hadi pale wabunge hasa wa CCM watakapozinduka kwenye usingizi wa pono ndio mambo ya aibu kama haya yatakaporekebishwa
 
Haifai na haipendezi Rais kumteua na kumuapisha Jaji Mkuu.

Jaji Mkuu alipaswa kuomba nafasi hiyo na chombo kama kamati ya majaji inampitisha na kumwapisha ili kulinda Uhuru wa Mahakama.

Kwa mtindo wetu huu Mahakama haiko huru kabisa. Yaani mhimili wa Mahakama uko ndani ya Dola/Rais.
Kiongozi, Je unafahamu Mchakato wa kumpata Jaji Mkuu ukoje? Labda kama tatizo lako ni raisi kumwapisha jaji mkuu tu, lakini kuteuliwa kwa jaji mkuu ni mlolongo ambao ukiambiwa utashangaa.
 
Je akimkataa huyo waliomleta kutokana na mchakato inakuwaje na nani anafahamu? Je akiamua "kuwashughulikia" hao wanamchakato kwa ku - challenge matakwa yake inakuwaje? Bado naamini Rais anamteua jaji anaemtaka yeye, uhuru sijui wa mchakato wala mlomlongo Tanzania haupo.
 
Akimkataa aliyeletewa mchakato unaanza upya! Matakwa yake hayaanzi, bali mchakato ndio unaanza.
 
Haifai na haipendezi Rais kumteua na kumuapisha Jaji Mkuu.

Jaji Mkuu alipaswa kuomba nafasi hiyo na chombo kama kamati ya majaji inampitisha na kumwapisha ili kulinda Uhuru wa Mahakama.

Kwa mtindo wetu huu Mahakama haiko huru kabisa. Yaani mhimili wa Mahakama uko ndani ya Dola/Rais.
Labda tu jaji mkuu mwenyewe aamue kujipendekeza lakini baada ya kuteuliwa huyo rais hana lolote la kumfanya!

Yupo huru kabisa kisheria!
 
MKUU UMEONGEA POINT

HATA HVYO, JAJI MKUU AKIAPISHWA, RAIS HANA MAMLAKA NAYE TENA.. UKIONA ANAVURUNDA NI UZEMBE WAKE TU.
 
Kila kiongozi hufanya kazi kwa kiapo. Hivyo kwa kiapo cha jaji mkuu automatically atawajibika kwa rais, hivyo hawezi kuwa huru.
 
Akimkataa aliyeletewa mchakato unaanza upya! Matakwa yake hayaanzi, bali mchakato ndio unaanza.
Huo mchakato hauko wazi na ndio maana hakuna anayeujua. Lakini kwa maneno yake mwenyewe Rais alisikika akijinadi kutumia muda mwingi kumteua Jaji Mkuu. Sasa huo mchakato uko wapi hapo wakati yeye ndiye kajisifia?
 
Mchakato uko wazi sana kwa wanaohusika na mchakato wenyewe. Mchakato huu ni siri kuu (top secret) na hautakiwi ufahamike kwa mtu mwingine zaidi ya wahusika tu. Raisi alitumia mda mwingi kumteua jaji mku kwa sababu nae alihitaji mda kujihakikishia. angekataa angeletewa mtu mwingine.
 
Kama Rais ndiye mwenye final say, basi yeye ndiye anayeteua. Na hicho ndicho tusichokitaka
 
Back
Top Bottom