Rais Kikwete kuzindua ujenzi wa reli mpya ya kisasa

Akili zao ndio zimeishia hapo kwa kutuita wapumbavu na malofa kwa sasa wanatamka chochote wanachojisikia wakijua tutawaamini kumbe sivyo na tunawaambia hatudanganyiki kura ni kwa UKAWA na Lowasa
 
Labda kama walipata teknolojia ya kupaisha bundi au ungo, akili ile ile iliyoua ATCL haiwezi kuifufua
 
Asante NEC kwa kuniandikisha jina langu kwenye kitabu cha kupigia kura.
Mubarikiwe sana
 
JK angekuwa suti, ningeitundika Makumbusho ya Hayati Mwl. JK Nyerere.
 
Hivi kinachoendelea na Kenya Airways atujajifunza chochote kuhusu hii biashara ya ndege kubwa.

ATCL waangaike na route ambazo watanzania wengi wanatumia kuvamia masoko ya mbali na ndege kubwa hiyo ngoma awaiwezi kabisa bila ya ushirikiano na kama wakisema washushe landing fees za Tanzania na hii mikakati ya kutanua viwanja vya ndege wasahau if you have any idea how large airlines operate their businesses to make profits (utakuja kukuta route ya mwaka mzima inawekwa kwa sababu ya miezi minne tu ya mwaka, miezi mingine 8 ndege inastruggle even to break even).

Na hayo ni mashirika yenye videge vya mid-size airline inayokusanya abiria kila kona ya europe kwanza kabla ya kuwajaza kuja afrika kwenye jumbo jet moja. I dont see how you can compete na mtaji mdogo, bora wabakie na videge vyenye vi-route vya EA na SA afrika huko kwengine ni un-chattered territory tu na risk ni kubwa zaidi.
 
Lowasa ana kz moja tu Kuitoa ccm madaraka ni hatakiwi hata kutoa ahadi mengine titapanga nchi ikishakuwa mikono ni mwetu .
 
Baada ya miaka 10 ya Kikwete tumeishia kuachia majiwe ya msingi tu..!!
 
Watuambie ni lini yale mabehewa feki wataychukua ili waturudishie pesa zetu.
 
Ni upuuzi mtupu,wameshindwa miaka 54 wataweza ndani ya miaka 5? Mnakumbuka shuka asubuhi imeshafika?
 
Mmeshindwa yafuatayo kwa uchache, mtaweza kujenga hiyo reli? Acheni kutunywesha sumu

Hadithi ya kujenga flyover mwaka wa kumi sasa
Kipande cha barabara kigogo jangwani mwaka wa sita sasa
Tabata dampo kigogo (km 2) mwaka wa tatu sasa
Mbezi kinyerezi (km 13) mwaka wa tano sasa
Kituo cha mabasi ubungo zimebaki story tu.

Mtaweza hizo thousands of Kms za reli?

Maendeleo ni mchakato...haiwezekani ukaanza na kila kitu lazima kuwe na kitu na sehemu ya kuanzia.
Ujenzi wa barabara na miundombinu mingine huenda ikatekelezeka kwa uharaka zaidi kipindi hiki kwa kua mchakato wake ulianza zamani na unaendelea.
Wakiingia wengine na vipaumbele vyao tunaweza kusimama wakti wanatafakari waanzeje kutekeleza ilani zao.
Kitu kizuri ni kwamba upinzani unaendelea kuimarika na kupata uzoefu, wasichoke kujifunza na kuwa marafiki wa serikali ili kupata uzoefu wa mambo mazuri na pindi wakati ukifika wachukue nchi na kuendeleza mipango mizuri kwa taifa letu.
Kenya tunayoina kama mfano wa anguko la chama tawala na mambo yanawaendea vizuri, wanayotofauti kidogo na sisi.
Ilikusanya wazoefu serikalini na kuwaweka upande wao. Sisi viongozi wa kisiasa waliowahi kuhudumu serikalini ni wachache sana na wengi wao hawana ''maadili''.
Wengine mtasema hata Nyerere aliongoza hakuwa na uzoefu wa kuwa kiongozi wa nchi lakini utakubaliana na mimi kuwa tulikaa mwaka mmoja kabla ya kuwa jamhuri na kipindi chote pamoja na kuwa na uhuru lakin Uingereza ndio walikuwa wanawapa uzoefu.
 
Tukisema hiki chama na serikali yake vimechoka wengi hawaelewi.

Baada ya Lowassa kuahidi kwenye kampeni zake kujenga reli ya kati kwa Standard Gauge alitoka bwana Six na kudai ujenzi utaanza karibuni na utazinduliwa na Kikwete na kumsema Lowassa kuwa anadandia hoja asizozielewa.

Zikiwa zimebaki siku 16 Tufanye uchaguzi naomba mwenye taarifa za uzinduzi wa Reli hii atuwekee hapa ili tujue uwongo na ukweli uko wapi.
 
tukisema tutaje msururu wa ahadi ambazo ccm hawajawai kuzitimiza either kwa kiburi chao tu au mazoea yao nahisi tunaweza kujaza server ya JF
 
tukisema tutaje msururu wa ahadi ambazo ccm hawajawai kuzitimiza either kwa kiburi chao tu au mazoea yao nahisi tunaweza kujaza server ya JF

Alitamka maneno makali sana dhidi ya Lowassa tena akijiamini kabisa na habari ikapewa uzito wa juu.
 
Mnaongelea yule jamaa anayevuja jasho sana, yule ni mchumia tumbo kama alivyo Kigwangalla.
 
tukisema hiki chama na serikali yake vimechoka wengi hawaelewi.

Baada ya lowassa kuahidi kwenye kampeni zake kujenga reli ya kati kwa standard gauge alitoka bwana six na kudai ujenzi utaanza karibuni na utazinduliwa na kikwete na kumsema lowassa kuwa anadandia hoja asizozielewa.

Zikiwa zimebaki siku 16 tufanye uchaguzi naomba mwenye taarifa za uzinduzi wa reli hii atuwekee hapa ili tujue uwongo na ukweli uko wapi.
sitta alkuwa anaongea uongo na kwa kupotosha makusudi makusudi kutokana na hasira za kukatwa
 
Back
Top Bottom