Rais Kikwete: Kuna mgombea nimemtakia 'kila la heri' kwenye SMS

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,055
Katika mazungumzo yake, Mheshimiwa rais ametahadharisha endapo kuna mgombea yeyote wa urais atajitokeza na kusema kwamba yeye (JK) amemchagua, basi ieleweke kuwa hiyo haikuwa dhamira yake.

JK ameyasema hayo kufuatia kupokea ujumbe kutoka kwenye simu ya mkononi ulioomba 'baraka' zake kwenye nafasi hiyo inayowaniwa kwa sasa, ambao aliujibu kwa mkato 'Good-luck'.

"Mgombea mmoja alinitumia message akasema aumenisaidia sana kufika hapa naweza kushika hata hiyo nafasi yako, nipe baraka zako.. nikamwambia ‘goodluck‘ sasa sijui ataitumia hiyo goodluck yangu kusema mzee amenichagua mie!" J.K Kikwete.

Bashiri: Uonavyo wewe unahisi mgombea gani ndio atakuwa amemtumia meseji JK?

Hisani: TimesFM
 
Tuna shida kubwa nchini huyu jamaa anazungumzia personal sms na mgombea mmoja

uswahili ukzidi inakua balaa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Na kuandika jina lake kwenye kingo za madaraja mikoa yote tz
Siasa za kitoto sana, kanikumbusha kuchora kuta za shule kipindi cha uchaguzi wa serikali ya wanafunzi.

nimekuwa najiuliza ikiwa ataukosa urais je atawatuma tena walioenda kuandika wakafute maana madaraja mengi sana yameandikwa kuwa ye ndo rais mtarajiwa
 
Huyu JK nae anatakiwa apatikane kwenye kitabu cha Maajabu duniani! Yule Mhasibu sijui wa KCMC alomtumia SMS, msela hakujibu, jamaa wa watu kakamatwa na kasimaishwa kazi!!

Je huyu alie mjibu yuko juu ya binadamu wengine au?

Na hiyo simu yake ni ya kuwasiliana na akina nani? ( Orodha tafadhali, wengine tusije swekwa Lupango buree!).
 
Na hilo liwe fundisho kwa wanaojikomba kwa watu, eti umenisaidia sana kufika hapa so what......huyo uliyemtumia sms kakunanga hadharani,watu wanajipendekeza mpk kero.
 
Je na mimi nikitangaza nia, kuchukua fomu, na kutuma sms ya huruma nitaambiwa good luck? Waswahili wa Pemba wanajuana kwa vilemba.
 
Back
Top Bottom