Kwa upande mwingine ni Afadhali kulipia karo kuliko hii bure inayotangazwa. Unajua shule ya msingi ni bure, lakini hiyo michango ni zaidi ya karo na ni kero kweli kweli. Sekondari ada inayofutwa ni 20,000/= lakini pia kulikuwa na michango ya karo; na hivi sasa Ikiondolewa hiyo basi ujue michango itaongezeka. Waulize hata BRN wanalijuwa hilo maana ni moja ya mikakati yao.Serikali jana imetangaza elimu bure kuanzia primary hadi sekondary na kwa shule za private bei elekezi kutolewa! Pia baada ya maabara nguvu kuelekezwa nyumba za walimu! Elimu ya msingi miaka 10.
Hilo ni jambo jema kabisa nakubali, lakini je kwanini limekuja wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu? Je, ilisubiri uchaguzi tu? Kama si kampeni ya CCM ni nini?
Ukitaka kujua yaliyojiri jana soma magazeti ya leo : Majira, Mtanzania....n.k