Fisherscom
JF-Expert Member
- Mar 13, 2008
- 1,763
- 764
ni kweli hatahutubia, tezi dume limembana.. na jioni ya leo ataelekea Marekani kwa uchunguzi zaidi
We mutu hatari sana....teh teh
ni kweli hatahutubia, tezi dume limembana.. na jioni ya leo ataelekea Marekani kwa uchunguzi zaidi
Mbona hueleweki mkuu..??
Mkuu wa kaya anahutubia taifa jumatatu au?????
Watanzania mmemtukana sana mzee wenu ila j3 anaenda kuwapa zawadi ya x-mas na mwaka mpya anaenda kuwaacha watu wote midomo wazi, idara zote za usalama wametoka watu very faithful pamoja na wazee kuminambili wamejifungia mahali wanatengeneza sura mpya yakitaifa. Singasinga atajuta kutafuna fedha za wa Tz. Serikali imeomba msaada toka idara za nchi washirika zenye nguvu kwenda rudisha fedha za watanzania. Huu ndio mwisho wa ufisadi, mambo yote ni siri tena siri kubwa watu wameapa kiapo chakuto kutoa siri. No phn no anya connection only ikulu cable used. Hao walio toka nakuwautubia wa Tz kwamba niwasafi wanaenda kufa kisiasa maana uwenda asubuh ya j3 itakuwa mwisho wa kuwa mawaziri na hawatotakiwa kuongea chochote ktk media! Stay tune Tz
nasikia kuna baadhi ya mitandao inakwenda kula ban ni kweli?
nyerere ndo alikuwa hafai ndo maana wlikosakosa kumpindua safari tatu
Ni kweli. Nimemsikia Salva akiongea na Clouds muda mfupi uliopita.
Mkuu , japo kiduchu, kuwa aliahidi kuliongelea swala la escrow ndani ya wiki.
Wiki isha katika na mike ziko kimya, kulikoni?
hahaha,kuna watu wanangojea kwa hamu kweli hii sijui mkutano
Rais Kikwete ameahirisha kulihutubia bunge na 'Wazee wa Dar'; ambapo sasa ataongea nao Jumatatu wiki ijayo(Disemba 22, 2014),Ikulu imethibitisha kuwa na kusema muda utatangazwa.
Rais kikwete leo alitarajiwa kulihutubia taifa kupitia wazee wa mkoa wa Dar es salaam katika mkutano wake ambao ulikuwa ufanyike katika ukumbi wa Hotel ya Blue Pearl,ubungo jijini Dar es salaam.
Katika mkutano wake huo Rais Kikwete alitazamia kuzungumzia mustakabali wa nchini sambamba na kuweka wazi juu ya sakata la utekelezaji wa maazimio nane likiwamo la bunge la kuwawajibisha viongozi waliotajwa katika sakata la uchotwaji wa fedha bilioni 360 katika akaunti ya Tegeta Escrow Pamoja na mambo mengine.
Katika maazimio nane ya bunge yaliyopendekezwa yalitaka viongozi waliotajwa katika ripoti hiyo kwa tuhuma za uchotwaji wa fedha kuchukuliwa hatua za kinidhamu na hata wanapo bainika kufilisiwa mali zao na kushitakiwa katika viombo husika kwa kuonekana kulihujumu taifa katika sakata hilo la uchotwaji wa fedha akaunti ya Escrow.
Rais pia alipanga kuzungumzia juu ya Sekta ya Elimu pamoja na agizo lake la ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari nchini,Upigaji kura za maoni kuhusu katiba Mpya utakao fanyika Aprili 30 pamoja na daftari la wapiga kura.
Hata hivyo Katika Hotuba hiyo Rais aliazimia kuelezea uchaguzi wa serikali za Mitaa ulivyo fanyika ambao ulionekana kukumba na dosari kadhaa katika vituo vya kupigia kura katika sehemu mbali mbali za nchi ulipo kuwa ukifanyika uchaguzi huo ambao uliweza kugharimu maisha ya watu kwa kupoteza maisha.
Daaah.. Ninakumbuka ile stori ya Mwalimu kuhusu yule raia wa kigiriki aliekuwa anatangaza kwamba serikali yote ya Tanzania ameiweka mfukoni mwake..
JK ataingia kwenye rekodi ya raisi dhaifu kuliko wote Afrika asipochukua hatua zozote kwa sababu hii ya watu kwenda mahakamani..
Ni vizuri ukatumia lugha ya staha kufikisha ujumbe lugha kama hizo unazotumia si nzuri kwa mwendo huo tutakuwa tunajenga taifa la watu wasiyokuwa na adabu kuheshimiana miongoni mwa jamii yetu kutapotea na hiyo inaweza pelekea machafuko nchini kwetu kila kukicha
Kubwa lijalo, haya yote cha mtoto.Serious and potentialy dangerous undercurrents encountered!!!!
Sasa nchi inaongozwa kwa matukio-what's next!
Huyu ni zaidi ya dhaifu....ni dhaifuest...goigoi ambaye hawezi mshinda mbio farasi.