Rais kawekeza pakubwa, na bado anaendelea kuwekeza

Kalamu

JF-Expert Member
Nov 26, 2006
7,683
8,864
Rais Samia Suluhu Hasan, kamwe hawezi kujilaumu kwa kutofanya jitihada, tokea mwanzo wa utawala wake kuona umuhimu wa kushawishi makundi mbalimbali katika jamii kuungana naye katika juhudi zake za kusaka ngwe yake mwenyewe ya utawala hapo ifikapo 2025.

Mwanzo kabisa, katika makundi aliyoyawekea nguvu kuyavuta kwake ni kundi la wasanii, kundi ambalo hakuachana nalo hadi sasa. Juhudi hizo zilihusisha makundi mengine, kama ya tekohama; makundi ya michezo mbalimbali, na hata utawala wa kijadi wa machifu na kubahatika kuwa mkuu wa kundi hilo.

Baadhi ya juhudi hizo hazikuonyesha mafanikio yaliyotazamiwa, kama yale ya kuinasa CHADEMA na viongozi wake katika kokolo zito chini ya kilichojulikana kama "Maridhiano." Kuna baadhi ya makundi, licha ya kuunga juhudi zake za awali, kama lile lililobatizwa kwa jina la 'Sukumagang', kundi hili baadae lilijikuta kwenye hatihati na kuangukia pembeni kwa muda.

Sasa baada ya kuona mambo hayaendi vizuri ilivyotegemewa, karudi nyuma na kujaribu kulikusanya kundi hili kwenye kona yake. Ni mapema kusema kama juhudi zake za karibuni za kulisogeza kundi hili karibu naye zitakuwa na matokeo mazuri au la, kutokana na misuguano iliyotokea kati ya kundi hilo, na jingine linalojitambulisha kwa 'Uchawa'.

Juhudi za hivi karibuni, ni kujaribu kulikusanya kundi la kidini, chini ya inayojulikana kama TEC. Hili ni kundi linalojitambua sana, kwa hiyo ni vigumu kutabiri kama juhudi zake hizi zitafanikiwa kuwasahaulisha mambo mazito aliyojaribu kuyafanya yaliyoonekana kutokuwa kinyume kabisa na maslahi ya nchi anayoiongoza.

Amejitahidi kadri alivyoweza kwa njia zake mbalimbali kujionyesha kwamba ni msikivu, na kuruhusu maoni ya kundi hili kutazamwa. Bila shaka hatua hii inategemewa kuzaa matunda kwake kwa kundi hili kuwa upande wake katika juhudi za kupiga kampeni na kuungwa mkono kutoka upande huo.

Kwa hiyo Rais kajitahidi kwa upande wake, na bila shaka anayo matumaini makubwa ya ushindi hapo 2025 iwapo atapata ushirikiano wa makundi yote haya, bila kujali mengine yote yaliyofanyika katika awamu aliyoirithi yeye.

Je, haya makundi mbalimbali yanayotazamiwa kuunga juhudi zake, yatasahau yote yaliyopita katika utawala wake wa kipindi hiki cha miaka minne na kuganga yafuatayo?
 
Siasa za Dunia zinabadilika kwa kasi sana

Kwa mfano ndugu Paul Makonda kupewa Usimamizi wa Itikadi ya Chama hapo CCM itatoka awamu ya 4 na kurejea ya 5 hivyo Wananchi wataikumbatia tena na kuachana na Upinzani
 
Back
Top Bottom