Rais kapotoshwa na wasaidizi wake utenguzi wa Kairuki?

Hata JK aliwahi kumfuta kazi mwajiriwa wa Wizara ya Elimu kwa taarifa za informers bila kufanya uchunguzi...

Mkuki kwa nguruwe...

Chuma kala chuma

Na huyo jamaa alikuja akashinda kesi dhidi ya serikali. Kilichofuata baada ya hapo mkwere akaapa kutokufukuza watu kazi kinyaparanyapara ambayo ilikuwa extreme nyingine kwani kuanzia hapo watu ndio wakafisadi kwa kwenda mbele. Kwa nafasi ya urais extremes zote mbili hazifai-extreme ya jk na extreme ya magufuli pia.
 
Swali jepesi.

Huyu mama aliyetumbuliwa wana undugu na Mh Waziri wa Utumishi/Utawala Bora?
Au huyu ni mtu na wifi yake? Mbona majina yanafanana, wanashare kama mtu na dada au majina tu? Mwenye uelewa atujuze. Au ni majina tu kama ambavyo jina Juma, Ally, yanakua na watu wengi?!
 
Hivi inaingia AKILINI kuanza kazi mpya (3 years) na kuacha uliyonayo bila makubaliano ya mshahara na benefits zingine?
Nchii hii imejaa sisi wendawazimu!...hivi serikalini unaweza kuajiliwa huku "serikali na wewe mkiwa katika mjqdala wa makubaliano?"

Ni utaratibu upi jamani watanzania wenzangu unaajiliwa, unapiga kazi wakato bado humjakubaliana malipo ya kazi? Mbona kama sielewi?

Eti walimu/mahakimu mnapomaliza masomo mnaajiliwa na serikali wakati bado mnadebate juu ya salary? Hivi kweli hii ni serkali au kilikuwa kikundi cha watakachokiwe kinakuwa?
 
kuna uwezekano mkubwa JPM kapewa full story na ndiyo maana taarifa ikasema kama anahitaji kazi nyingine atapewa.
 
kuna uwezekano mkubwa JPM kapewa full story na ndiyo maana taarifa ikasema kama anahitaji kazi nyingine atapewa.
Kupangiwa kazi nyingine kwa mshahara upi anaoutaka yeye wa serikali hii ya JPM?!
 
Msuituchanganye watanzania na story za kupika kama South Africa kuna mshahara mkubwa arudi tu uko akafanye kazi haiwezekani mkuu wa taasisi ya wizara flani awe na mshahara mkubwa kuliko waziri
Si alimuomba Jk arudi arudi tu sasa magufuli ateue mwingine akimkosa aniteue mimi tu kazi itAenda vizuri tu kwani lazima awe yeye,
Usiongee kwa husia hao wakurugenzi ni wataalamu, waziri hachaguliwi kwa kuzingatia Taaluma aliyosomea na kazi ya Waziri ni kusimamia sera ya wizara,Hakuna jambo jipya katika hili NHC iko chini ya wizara ya Ardhi na MD anakula zaidi ya 30M,Tanesco iko chini ya Nishati na Madini na MD anakula zaidi ya 20M,TRA,BOT ziko chini ya Fedha n Mipango wakuu wake wanakula ndefu, TPDC wako chini ya Nishati na madini na MD wake anakula hela ndefu, sasa unaposema haiwezekani mkuu wa Taasisi kulipwa zaidi ya waziri unatumia reference za nchi gani?
Hizi Taasisi au Mashirika mengi yanazalisha au kutengeneza faida, usifananishe na wanasiasa/wawakilishi wa wananchi.
 
Wahaya kwa sifa na hili pia alikuwa anajisifia kuwa hawezi kupewa kamshahara ka mil 5 kwanza amaeolewa na super bilionea sasa JPM kasema ukatumikie ndoa yako yeye anataka wazalendo wanaochukua hata hako kadogo, na bora katumbuliwa tu TAASIS ya uwekezaji ndo imeuza nchi hii
 
Nchii hii imejaa sisi wendawazimu!...hivi serikalini unaweza kuajiliwa huku "serikali na wewe mkiwa katika mjqdala wa makubaliano?"

Ni utaratibu upi jamani watanzania wenzangu unaajiliwa, unapiga kazi wakato bado humjakubaliana malipo ya kazi? Mbona kama sielewi?

Eti walimu/mahakimu mnapomaliza masomo mnaajiliwa na serikali wakati bado mnadebate juu ya salary? Hivi kweli hii ni serkali au kilikuwa kikundi cha watakachokiwe kinakuwa?

Wanasema aliruhusiwa kuendelea na kazi na kujilipa posho kufidia mshahara ambao ndio alikuwa anajitahidi kupatana. Posho zikawa tamu, sasa miaka inakwenda mara Magu huyu... ndo hivo tena limekuwa jipu....
 
Story za vijiweni hizi. Ni company gani ilikuwa inamlipa hizo pesa? As far as I know ..not even the UN could pay her that amount (in a location where she was working). Kama ni private company muitaje hapa muache longo longo. Kama ni SADC au another regional organization huo mshahara haufiki.

Tatizo la watanzania wengi tunapenda ujanja ujanja. Hizi ni story za kuunga unga. Na hata mimi namuunga mkono Magufuli. Utafanyaje kazi kama hutaki mshahara wa mwajiri wako? kwa lugha nyingine kulikuwa hakuna uhusiano wowote wa mwajiri na mwajiriwa. So it was very good Magufuli got rid of her. Kwanza alichelewa.

Ushauri kwa watanzania wenzangu: Serikalini hakuna utajiri. Sijui hii mentality ya kuwa tajiri/kupata mishahara mikubwa tukiingia serikalini tunaitoa wapi. Nowhere in the world mshahara wa serikali unaweza kukufanya tajiri. Kama umeamua au unataka kuwa tajiri baki huko huko kwenye private sector. serikalini ni utumishi wa umma. Siyo sehemu ya kutengeneza pesa. Ndo maana Magufuli anafukuza watu kila siku kwa sababu tumepoteza uelekeo kwa kudhani serikalini ndo kuna hela. That is wrong and should be discouraged.
Narudia tu nilisha andika kitambo kwamba mawaziri,wakurugenzi,wabunge na post zote selikalini mishahara iwe midogo tu isizidi hiyo mil 5 na allowances zipunguzwe kabisa na magari yawe 4x4 double cabin au landcruiser 2 ili ile tamaa ya kutaka hivi vyeo ifutike watu wanauwana kwa kugombania hivi vyeo that means kuna maslahi na ufisadi mkubwa
 
Habari wanaJF,

Kufuatia kuteguliwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC), Bi. Juliet Kairuki taarifa za ndani zinasema bibie huyu kaonewa kwa sababu zilizoainishwa katika nukuzi ya taarifa hapa chini.

"Huyu Julieth ni mke wa Dr.Kairuki Mkurugenzi wa Mikocheni Hospital. Kabla ya kuja Tanzania alikua anafanya kazi South Afrika akilipwa mshahara wa USD 15,000. JK ndiye aliyemkuta SA akamuomba arudi nchini kuja kusaidia pale TIC baada ya Ole Naiko kustaafu. Kabla hajaja wakaset T&C kuwa her salary wont go bellow 18M Tzs.

Ikumbukwe SA alikua akilipwa 15K USD equals to 35M Tzs. Kwahiyo kukubali kulipwa 18M ni kukubali kusucrifice 17M kitu ambacho si rahisi kwa watu wengi. Lakini she did that for the sake of her country. But alipofika nchini TIC wakamwambia hawana scale ya 18M, wakataka kumlipa 5M. Huyu mama akakataa. She cant be that cheap kutoka mshahara wa 35M kule SA hadi 5M? Akamwomba JK arudi SA kuendelea na kazi yake, lakini JK akaagiza TIC wafanye salary review ili kuweza kuaccomodate madai yake. Kipindi chote hicho alikua hapokei mshahara b'se alikua hajafikia concesus na serikali. Sasa kabla TIC hawajakamilisha salary review ndio JPM akawa ametake power. Akawa anadiscourage mishahara mikubwa kwa wakuu wa mashirika ya umma.

TIC wakaogopa kuendelea na review ya Kairuki. Katika ufuatiliaji JPM akaambiwa kuna Mkurugenzi hajapokea mshahara tangu 2013. Lakini informers wake they didnt nail the whole story. Wao wakamwambia tu amekataa mshahara aliopangiwa anataka mkubwa zaidi na marupurupu makubwa. JPM akahamaki na kutengua uteuzi without knowing the truth. Hapa JPM kafanya kosa lakini simlaumu yeye, nalaumu informers wake. Basing on the facts provided huyu mama kaonewa sana and worse enough JPM hakumuita kumsikiliza. He just made decision basing from his informers.

This is typical injustice b'se principles of natural justice were abandoned. Ni bora JK angemruhusu arudi SA kuendelea na kazi yake"

Karibuni wadau.
Kwani wewe ndie mwajiri wake?wewe na raisi nani anajua zaidi?kama alikuwa hachukui mshahara kwani alikuwa anafanya kazi bure kwa mahaba yapi,ukiona mkono mmoja unaingia mfuko wa kulia jua na mkono mwingine unaingia mkono wa kushoto,badala ya kushobokea hapa ndugu jua kuna wengine wanajua yote ,kwanza alikuwa hapati mshahara huo wa USD$15,000 huko SA,pia alikuwa anakwamisha kujadiliwa huo mshahara wake huku akichukua posho ya 25 milioni kila mwezi,sasa kwa hiyo posho kuna haja gani ya mshahara,halafu eti ndio alikuwa anafanya kazi bure,nani kasema kuna kufanya kazi bure ,hata Red Cross hawafanyi kazi bure siku hizi.Ukiona hivyo jua kuna kitu nyuma ya pazia,eti bure nani kasema kunabure siku hizi
 
Hajakosea hata chembe, chukua mfano huu; 'umemkamata mtanzania akiiba mayai supermarket, hebu jaribu kumpa nafasi aongee uone nini kitatokea...
Kama ulicho kiandika ni kweli,jpm kakosea
Sijasema huyo mama ni mwizi note that!
 
Ayaaa hebu subili kidogo nifanye makakulesheni kabisa
posho = 25,000,000 x 12 x 3 = 900,000,000/=
Mother katusua si mchezo ngoja akapumzike kwa raha zake
 
Nchii hii imejaa sisi wendawazimu!...hivi serikalini unaweza kuajiliwa huku "serikali na wewe mkiwa katika mjqdala wa makubaliano?"

Ni utaratibu upi jamani watanzania wenzangu unaajiliwa, unapiga kazi wakato bado humjakubaliana malipo ya kazi? Mbona kama sielewi?

Eti walimu/mahakimu mnapomaliza masomo mnaajiliwa na serikali wakati bado mnadebate juu ya salary? Hivi kweli hii ni serkali au kilikuwa kikundi cha watakachokiwe kinakuwa?

Ni jambo ambalo haliwezekani, labda aliyesema hilo ana "divert" kutenguliwa kwake na kutoa sababu zingine.
 
Kama kawaida yangu huwa nakuwa faster kuwafundisha MAJUHA jinsi ya kujenga HOJA na si kutuletea UPUUZI humu. Hivi kwa akili ya kawaida tu na ambayo hata haihitaji uwe na Elimu kubwa kivile inawezekana Mtu akafanya Kazi mahala halafu asichukue Mshahara wake? Na ndiyo nampenda mno na namwombea kila siku US Republican Presidential Hopeful Donald Trump apite na apambanishwe na Mama Clinton Uchaguzi Mkuu ujao wa Marekani November ili awe Rais wa Marekani na ATUKOMESHE sisi WAAFRIKA tulio na UVIVU wa kufikiri na tuliokalia UTEGEMEZI tu tushike adabu!

Mkuu tupo kwenye meli moja namtaka hata Trump achukue tu huko US ili atukomeshe waafrika tunapenda kuimba imba utendaji zero.! JPM alipokwenda kwa Kagame alienda kimkakati moja wapo ni kupata ni vipi Rwanda is the best country in EA?? PK alimpa hivi asichekecheke na watu usoni na ndivyo JPM anavyofanya.. Huyu mama alimaliiza first degree hapo mlimani na master ndo alichukulia South na kazi akapata huko..sasa mtu mwenye akili timamu umwambie eti aache 35m aje bongo ale 5m kwa ajili ya uzalendo atakuona ww ni hamnazo atii..huyo alikua jipu, jamani mengine siri za ndani ngoja tuweke akiba za maneno!
 
Awamu ya 5 hatutaki kusikia " Rais kapotoshwa" apotoshwe na nani? Kwanini akubali kupotoshwa? Kupotoshwa ni kosa la kiuwajibikaji kama alivyoajibishwa Kilango kwa kupotoshwa.
Tunahitaji dakika ngapi za kufikiri jambo fulani kama ni sahihi au sio sahihi? Uzalendo gani ukufanye uanze kazi bila mkataba na bila malipo? siku, miezi, miaka!!!! Tunajua kama kufanya kazi pasipo mkataba au makubaliano ni kosa? Tunajua hata kufanya kazi pasipo malipo ni kosa?
 
Kuhusu kuishi bila mshahara miaka mitatu kwa mtu kama mke wa marehemu dr Kairuki si ajabu hata kidogo!Ile hospitali pale mikocheni,na chuo kikuu cha Kairuki vinaingiza zaidi ya Milioni 15 kwa siku!sasa huyu mtu atahitaji mshahara wa nini?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Sasa malalamiko ya nini si aende sasa akatumbue hizo za wagonjwa wa kairuki mpaka wagonjwa mnawafanya dili, kama huu moto upo kweli kwa mungu kuna watu wakuyeyushwa kabisa
 
Back
Top Bottom