Alikua mkimbizi tu. Karudi kwao!
RAIS Paul Kagame wa Rwanda amemteua Mtanzania, Profesa Silas Rwakabamba kuwa Waziri wa Miundombinu wa nchi hiyo katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Jumatatu iliyopita.
Kabla ya uteuzi huo, Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda. Ni mmoja wa mawaziri wanaoingiza sura mpya katika Baraza la Rais Kagame ambalo amelifanyia mabadiliko kwa kuunda wizara nyingine mpya.
Sura nyingine mpya katika Baraza hilo ambalo liliapishwa juzi Ikulu ya Rwanda ni pamoja na Seraphine Mukantabana (Wakimbizi na Menejimenti ya Maafa) na Oda Gasinzigwa (Ofisi ya Waziri Mkuu- Familia na Jinsia).
Akizungumza kwa simu na mwandishi wetu jana, mdogo wa Profesa Rwakabamba, Timothy Rwamushaija anayeishi Dar es Salaam, alisema ndugu yake alizaliwa katika Kijiji cha Bushagara, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.
Alisema Profesa Rwakabamba alikuwa Mtanzania aliyeamua kuchukua uraia wa Rwanda na wote baba yao ni Mzee Titus Rwamushaija... Huyu ni kaka yangu wa tumbo moja na kwa kweli tumefurahi sana kwa mafanikio yake sisi kama wanafamilia.
Naibu Makamu Mkuu - Taaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Profesa Makenya Maboko alisema Profesa Rwakabamba alifanya kazi katika chuo hicho na aliondoka akiwa Mkuu wa Kitivo cha Uhandisi.
Aliondoka wakati Kagame alipoingia madarakani na alikwenda kuongoza Taasisi ya Teknolojia ya Kigali (KIST) kabla ya kwenda katika Chuo Kikuu cha Kigali, alisema Profesa Maboko.
Msomi huyo alikwenda Rwanda mwaka 1997, baada ya kuombwa na Rais Kagame ambaye alikwenda UDSM kuwaomba baadhi ya wahadhiri kwenda Kigali kufungua chuo kikuu katika taifa lake baada ya kumalizika vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1994.
Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa kwanza wa KIST na kukifanya kuwa miongoni mwa vyuo bora barani Afrika kwa masuala ya teknolojia jambo lililomfurahisha Rais Kagame.
Baada ya mafanikio hayo, Rais Kagame alimteua kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda, Butare ambako pia alijizolea sifa baada ya kusimamia vyema ujenzi wa mabweni kwa wingi na kiongozi huyo alimtunukia uraia wa nchi hiyo kama zawadi.
Hata hivyo, Profesa Rwakabamba atakuwa amelazimika kuukana uraia wa Tanzania kwa kuwa katiba ya nchi hairuhusu uraia wa nchi mbili.
Profesa Rwakabamba alipata elimu ya msingi huko Muleba na akajiunga na Shule ya Sekondari ya Ihungo.
Baada ya hapo, alijiunga na Chuo Kikuu cha Leeds, Uingereza na kupata Shahada ya Uhandisi mwaka 1971 na 1975 alipata Shahada ya Uzamivu katika fani hiyohiyo.
--------
Hapa JF, kuliwahi kuwa na mjadala juu ya mwanazuoni huyu hapa ---> https://www.jamiiforums.com/celebri...nia-mwanzilishi-wa-kigali-institute-kist.html
Wapo ndio!
Ndugu zangu msidanganyike, huyo Prof. Silas Rwakabamba, ni Mtanzania na wala hatuhitaji kujiuliza kama ni Mtusi au nini, maana kwa wabantu na hasa ukifuatilia historia za migration za wananchi wetu, na hasa wa mipakani, utakuta Ancestral origin ni moja. Hivyo si ajabu Mchaga kufanana na Mkikuyu, Mha kufanana na Mrundi na mengine, maana walipodecent kuja huku walikaa maeneo yanayofanana. Maeneo ya Bukoba wana koo za Kitemi mathalani, koo hizi za akina Kasusura, Ruhinda, Rumanyika and so forth, wana origin inayofanana, na hawa hawa akina Bahinda ndio pia wako Rwanda, Burundi na Uganda, but that does not make them Baganda, Barundi or Banyarwanda. Ni vema kuelewa hiyo misingi ya Historia ili kuwaza vema. Hata majina yana aina fulani ya kufanana. Watoro, Wachiga na Wanyankole toka Uganda wanazungumuza sawia na Wahaya na Wanyambo, toka Tanzania, lakini hii haiwafanyi kutokuwa Waganda au Watanzania. Litafakari hilo.ni mtusi aliesoma hapa tanzania.
Mbona sura yake full mnyarwanda? Nileteeni huyo mdogo wake nimhoji
Mbona sura yake full mnyarwanda? Nileteeni huyo mdogo wake nimhoji