Rais Kagame Kamteua Mtanzania kuwa waziri

Pamoja na kwamba ni ya muda mrefu, mtu akishaukana uraia wake hawezi kuitwa "mtanzania" tena. Huyo ni mnyarwanda mwenye asili ya Tanzania.
 
Mwacheni mzee wa watu asaidie kuijenga Rwanda, sisi wasomi wetu na maprofesa wetu tunawatumia vibaya kama misukule, angalia tulivyomharibu propesa ripumb
 
Kiinteligensia waweza kuta alikuwa mnyarwanda then akapandikizwa Tz kwa kazi maalumu na alipoikamilisha akachukuliwa kinamna namna. Na sisi tulivyo maji vichwani tunajisifu pasi na kuangalia kwa jicho la tatu.

Nahisi vyuo vyetu vikuu vina mapandikizi mengi sana ya nje.


Hatushtuki



Usingizi wa pono
 
mimi uzuli nishawahi kuishi kagera ukweli ni kwamba asilimia 50 ya wakazi wa muleba na bukoba wengi asili yao ni rwanda ila wakiwa hapa mjini wanajiita wahaya ,

ila sisi wataalamu huwa tunawatambua kwa kuangalia sura, macho na pua tukishawaona hapa mjini tunawajua wametokea wapi licha wakiwa hapa town wakijiita wahaya
 
17008707821_4d25809c36_k-750x375.jpg

RAIS Paul Kagame wa Rwanda amemteua Mtanzania, Profesa Silas Rwakabamba kuwa Waziri wa Miundombinu wa nchi hiyo katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Jumatatu iliyopita.
silas.jpg
Profesa Silas Rwakabamba.

Kabla ya uteuzi huo, Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda. Ni mmoja wa mawaziri wanaoingiza sura mpya katika Baraza la Rais Kagame ambalo amelifanyia mabadiliko kwa kuunda wizara nyingine mpya.

Sura nyingine mpya katika Baraza hilo ambalo liliapishwa juzi Ikulu ya Rwanda ni pamoja na Seraphine Mukantabana (Wakimbizi na Menejimenti ya Maafa) na Oda Gasinzigwa (Ofisi ya Waziri Mkuu- Familia na Jinsia).

Akizungumza kwa simu na mwandishi wetu jana, mdogo wa Profesa Rwakabamba, Timothy Rwamushaija anayeishi Dar es Salaam, alisema ndugu yake alizaliwa katika Kijiji cha Bushagara, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.

Alisema Profesa Rwakabamba alikuwa Mtanzania aliyeamua kuchukua uraia wa Rwanda na wote baba yao ni Mzee Titus Rwamushaija… “Huyu ni kaka yangu wa tumbo moja na kwa kweli tumefurahi sana kwa mafanikio yake sisi kama wanafamilia.”

Naibu Makamu Mkuu – Taaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Profesa Makenya Maboko alisema Profesa Rwakabamba alifanya kazi katika chuo hicho na aliondoka akiwa Mkuu wa Kitivo cha Uhandisi.

“Aliondoka wakati Kagame alipoingia madarakani na alikwenda kuongoza Taasisi ya Teknolojia ya Kigali (KIST) kabla ya kwenda katika Chuo Kikuu cha Kigali,” alisema Profesa Maboko.

Msomi huyo alikwenda Rwanda mwaka 1997, baada ya kuombwa na Rais Kagame ambaye alikwenda UDSM kuwaomba baadhi ya wahadhiri kwenda Kigali kufungua chuo kikuu katika taifa lake baada ya kumalizika vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1994.

Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa kwanza wa KIST na kukifanya kuwa miongoni mwa vyuo bora barani Afrika kwa masuala ya teknolojia jambo lililomfurahisha Rais Kagame.

Baada ya mafanikio hayo, Rais Kagame alimteua kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda, Butare ambako pia alijizolea sifa baada ya kusimamia vyema ujenzi wa mabweni kwa wingi na kiongozi huyo alimtunukia uraia wa nchi hiyo kama zawadi.

Hata hivyo, Profesa Rwakabamba atakuwa amelazimika kuukana uraia wa Tanzania kwa kuwa katiba ya nchi hairuhusu uraia wa nchi mbili.

Profesa Rwakabamba alipata elimu ya msingi huko Muleba na akajiunga na Shule ya Sekondari ya Ihungo.

Baada ya hapo, alijiunga na Chuo Kikuu cha Leeds, Uingereza na kupata Shahada ya Uhandisi mwaka 1971 na 1975 alipata Shahada ya Uzamivu katika fani hiyohiyo.

Chanzo: Mtanzania ateuliwa kuwa Waziri nchini Rwanda - SWAHILI TIMES
kuna umuhimu mkubwa sana kuhakiki majina ya watu wanaoopewa nyadhifa secta za serikali, hasa hayo majina ya kinyarubanja fulani hivi hayo.
 
mimi uzuli nishawahi kuishi kagera ukweli ni kwamba asilimia 50 ya wakazi wa muleba na bukoba wengi asili yao ni rwanda ila wakiwa hapa mjini wanajiita wahaya ,

ila sisi wataalamu huwa tunawatambua kwa kuangalia sura, macho na pua tukishawaona hapa mjini tunawajua wametokea wapi licha wakiwa hapa town wakijiita wahaya

Pa1 na yote hayo imekuingizia sh.ngap.?
 
kuna umuhimu mkubwa sana kuhakiki majina ya watu wanaoopewa nyadhifa secta za serikali, hasa hayo majina ya kinyarubanja fulani hivi hayo.

Hata hawa wakina mwa.... na wakina mwa... itabid tuwachunguze mana wako sekta nyeti watakua wamalawi au wazambia hawa
 
Tanzania kuna wanyarwanda wengi sana na wana vyeo vikubwa serikalini, baadhi in wale walioingia 1959 na walipewa uraia sema wakichoka wanaamua kuukana utanzania na kurudi Rwanda, binafsi nawajua wengi tu waliorudi kwao na kupewa position kubwa serikalini.
 
Back
Top Bottom