Rais Jakaya Mrisho Kikwete hoyee!

MR. MORRIS T. J.

JF-Expert Member
Apr 18, 2013
1,167
402
RAIS JK Huwa Ananikosha Sana Pale Anapoamua Kuwashushua Wazi Wazi Watendaji Wanaojifanya Wao Ndo Wao Hawataki Kusikia Ki2 Upinzani.

Mfano Steven Wasira Alinukuliwa Akidai Wapinzani Wanapenda Kwenda Ikulu Kunywa Juice Na Rais Na Safari Hii Hata Waandamane Usku Na Mchana Hatutawaita Ikulu, Baada Ya Maneno Hyo Wiki Iliyofuata Rais Aliwaalika Wapinzani Wake Kwenda Kuongea Nao Ikulu Na Wakakubaliana Na Rais Akasema Hoja Za Wapinzani Ni Za Msingi Akawashangaa Wabunge Wa Chama Chake Kuyakataa Mawazo Ya Wapinzani.

Juzi Tena Rais Kakutana Na Wapinzani Wake Wakakubaliana Kuwa Bmk Lisitishwe Hadi Mwakani Na Katiba Iliyo Ifanyiwe Marekebisho Jambo Ambalo Sita,wasira,lukuvi,hawakuwa Tayari Kabisa Bmk Kuahirishwa, Sasa Rais Kawakana Hadharani.

RAIS JK NI MSIKIVU SANA KWAHILI WACHA NIMPONGEZE,TUOMBE MUNGU TUSIPATE RAIS MKAIDI KAMA WASIRA JEURI KAMA SITA. IKIBIDI JK AONGEZEWE MIAKA MIWILI AKAMILISHE HUU MCHAKATO WA KATIBA MPYA. HEKO RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETEEEE, FAGILIA KIKWETEE WAA WAA WAAA
 
Waswahili ni watu wa ajabu sana, mnaweza mkapanga jambo vizuri asubuhi, jioni akakugeuka.

Sas Wasira,Chemba na Lukuvi wamegeukwa jioni
 
Kama umechunguza vizuri JK ni kiongozi mzuri sema misimamo ya chama chake na baadhi ya watumishi wake wanatumia makalio bado kufikiria katika kuongoza wananchi. Ila naamini atakumbukwa kama shujaa wa nchi kama ataendelea na msimamo huu wa kuwasikiliza wapinzani pale katiba huru itakapopatikana
 
unampongeza kwa lipi hasa..??????????? mtu ambaye anarejea matapishi na kusahau aliyoyanena nyuma.
 
unampongeza kwa lipi hasa..??????????? mtu ambaye anarejea matapishi na kusahau aliyoyanena nyuma.

Binadamu mwenye busara anapofanya kitu Fulani kiasha akagundua kuwa alitereza hujirudi na kusahihisha mahala alipokesea. Mhe. Rais, amesahihisha, tumpongeze badala ya kuendelea kumkashifu. Fagilia JK, wa waaaaaa
 
Jana tu nilipita kwenye uzi wa gazeti moja kumuomba radhi mkulu,nkasema jamaa ni muungwana,na ameudhibitisha uungwana wake kwa kuweka maslahi ya taifa kwanza,sio wachumia tumbo wengine walokuwa wakitaka kulazimisha mambo,kikwete ni kiongozi mzuri tatizo sera za ccm,leo amedhibitisha ni wakati wa wana ccm kubadilika ccm na kuiga mfano wa huyu jamaa ambaye dakika za kukuribia kumaliza mchezo anawasawazisha na kufanya mchezo uende extra time.mi sijari mamilion mangapi yameteketea heri tupate katiba bora ya miaka 50 ijayo WELLDONE MR RAIS
 
Huu ni upotoshaji!!!! Wanaostahili kupewa Oyeeeeeeeeee ni UKAWA na wananchi, siyo JK! JK amelazimika kunywea kutokana na mashinikizo ya wananchi! Mashinikizo ya UKAWA, Viongozi wa Dini k.mf Tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania, wana harakati, kesi zilizoko mahakamani, Jumuia ya Kimataifa n.k, yamemfanya JK kusalimu amri! Majuzi tu, yeye na Kamati yake Kuu ya CCM walikuwa mstari wa mbele kuunga mkono uhuni unaoendelea BMK!!!!!
 
Waswahili ni watu wa ajabu sana, mnaweza mkapanga jambo vizuri asubuhi, jioni akakugeuka.

Sas Wasira,Chemba na Lukuvi wamegeukwa jioni

Hao niwaharibifu tu hawana issue kaziyao kubwa ni kuvimbisha matumbo yaotu, na hawako kimaslahi ya nchi! na sasa ni kazi kwetu wa tanzania kuwatambua vizuri watu wa jinsi hiyo, na watu wa jinsi hiyo huruka yao kubwa ni unyonyaji.
 
Tunampongeza kwa kusikiliza malalamiko yalio ya wengi ukijumuisha na ukawa, na wengi tulilalamika kuhusiana na hu mchakato jinsi ulivyokuwa unaendeshwa ktk lile bunge la kuunda katiba mpya, kwa kweli lile bunge lilikuwa linaendeshwa ndivyo sivyo, kwamanahiyo sasa uamuzi alio chuwa raisi ni uamuzi wabusara. Ndiomana tunampongeza raisi, nafikiri imeeleweka!
 
Huu ni upotoshaji!!!! Wanaostahili kupewa Oyeeeeeeeeee ni UKAWA na wananchi, siyo JK! JK amelazimika kunywea kutokana na mashinikizo ya wananchi! Mashinikizo ya UKAWA, Viongozi wa Dini k.mf Tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania, wana harakati, kesi zilizoko mahakamani, Jumuia ya Kimataifa n.k, yamemfanya JK kusalimu amri! Majuzi tu, yeye na Kamati yake Kuu ya CCM walikuwa mstari wa mbele kuunga mkono uhuni unaoendelea BMK!!!!!

Wote ni wa kupewa pongezi na ametimiza azma yake alitamka Serikali tatu tusubiri yeye atoke.Kweli yametimia.Hongera JK.Hongera Ukawa.Hongera baraza la wakristu.
 
Binafsi nitofautiane na mleta uzi. Simpongezi na sintompongeza mkulu kamwe kwani kaenda kinyume na slogan yake inayosema "za kuambiwa, changanya na zako"!. Angewasikiliza ukawa angeokoa fedha za umma kwani angeliahirisha au kulivunjilia mbali.
Bado amemwacha mr. Six kuendelea badala ya kumterminate immediatelly. Na kuuwaumbua wenzake kina lukuvi, wasira na wale waliokuwa wanaapa kuipata katiba mpya sijapenda kwani walikuwa wanajitahidi kumharibia yale mema aliyoyatendea nchi hii. Kiukweli hukuwa msikivu kwani ungeweza kuyaepuka matumizi ya fedha za umma yasiyo na tija!. Hongereni ukawa kwa kusimama imara na kupelekea anguko kuu kwa kina nape.
 
Back
Top Bottom