Rais Jakaya Kikwete atembelea mashamba ya mananasi Ghana

MAKOLE

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
618
280
Wakati nchi yetu ikiwa na Mikoa kibao yenye kutoa matunda mbalimbali yanayoozea shambani kwa kukosa soko, Rais wetu ametembelea shamba la mananasi huko Ghana baada ya kuonana na Raisi mpya wa Ghana.

Kwa mtazamo wangu, ziara hii ingefanywa na wakulima wa Chalinze ambao ndio wakulima wakubwa wa mananasi wakiongozana na Katibu wa wizara na maofisa wengine wa Kilimo, kuliko kufanywa na watu waliokwenda msibani ambapo sina hakika kama yupo mtaalamu wa kilimo miongoni mwao.

Rais wetu analitembelea shamba hilo ambalo Mwalimu Nyerere aliwahi kulitembelea katika miaka ya 1980, lakini hata hivyo hakuna jipya lililofanyika na ndio maana ziara kama hizi zinapaswa kufanywa na wahusika wa kilimo hicho pamoja na wataalamu badala ya wanasiasa.

source: Michuzi Blog.
 
Nakumbuka sana alipotembelea shamba la nyanya Brasil,nilitegemea sana angetembelea kiwanda cha ndege za Brasil ili apate challenge ya kuagiza ndege mpya hata 5 hivi......lakini si nyanya!
 
Kuna hatua mtu anafikia inabidi UMSAMEHE BURE......Kama miaka 7 hajaweza kusikia ushauri wa wataalam wake; wa wananchi wake na hata huko anakozurura kila siku kujifunza wenzake walivyo makini, huwezi kutegemea mabadiliko kwa sasa!!!! TUVUMILIE KIPINDI KIISHE; tumalize dozi yetu japo ndiyo hivyo ni CHUNGU!!!
 
Bila shaka anatamani abaki huko huko
G
H
A
N
Aendeleze ufisadi wake aliouzoea ila huko Nchi za magharibi hawawataki kutokana historia yake mbaya!
 
Msibani kkwenyewe kaenda yeye pamoja na membe, mi najiuliza kwani asingeweza kwenda mmojawapo na mwingine akabaki anfanya majukumu mengine ya ndani, mbona Obama alibaki anapiga kazi huku Clintony akiwa msibani?
 
Kuna siku alisafiri katika moja ya nchi za kusini mwa Afrika, akatembelea 'ranchi' za ng'ombe akashangaa sana ukubwa wa ng'ombe wale aliowaona, akasema, namnukuu, 'sijawahi kuona ng'ombe wakubwa kiasi hiki' na akauliza jinsi wanavyowatunza. Kwa tukio zuri alikuwa na mmoja wa wataalaamu wa mifugo akamwambia mzee Iringa kuna ng'ombe wakubwa kuliko hawa. Mkuu akabaki anashangaa hana cha kusema kusikia nchini kwake kuna ng'ombe wakubwa kuliko wale.

Yaani mkuu anajua shughuli zinazofanywa na nchi za watu kuliko nchini mwake. Ningemsifu kama angekuwa anavaa viatu vya tope kama mwalimu na kutembelea mashamba ya nyanya ya Iringa, mashamba ya mpunga ya Ifakara, sio kwenda nchi za watu kutumia kodi nyingi bila tija yoyote.

JK uone aibu sasa, umeshatalii vya kutosha hebu miaka iliyobaki tulia nyumbani, sio utoke ikulu ukiwa hujatuachia hata vijisenti kidogo vya kuendesha nchi.
 
Picha za mashamba aliyotembelea

ga4.jpg

ga5.jpg

ga6.jpg

ga5.jpg
 
Yanafanana kila kitu na haya ya hapa kwetu, hata pale Chalinze -Bagamoyo yapo mengi tu. Au mzee anahitaji kuwa mwekezaji mkubwa wa mananasi so amekwenda kupata maujuzi.
 
Angekuja hata huku kwetu Katavi eneo la maji moto ashangae kilimo cha mpunga, hata huo mpunga unaoskia wanauuita eti wa Mbeya unalimwa hapa kwetu Katavi eneo la Majimoto na kupelekwa Mbeya maana ndo hivo tulishacream kuwa mchele mzuri unatokea Mbeya.WanaKatavi tuamke sasa tulitangaze soko la mpunga wetu ili Rais wetu asije siku moja akaenda Uganda kushangaa kilimo ambacho hata hapa kwetu tunakifanya tena kwa ustadi
 
Duh! what a costly journey. Si angetembelea Del Monte plantations Kenya.

kenya akafanye nini na wao wametudharau kumbuka wale waliopata ajali juzi wameshachukuliwa kwa amri ya raisi wao kwa ndege ya jeshi kama vile huku hakuna hospital fikiria mtu amevunjika lakini wamemchukuwa utafikiri hatuna hospital .
wakati huo kumbuka walikuwa hospital kuu muhumbili.....hizo gharama za kwenda kuzika misiba yote aliohudhuria zingejenga au kununua x-rays ngapi?

 
Back
Top Bottom