Kwanini tusimpongeze Rais Magufuli kwa kununua ndege kwa Cash?

Kweli tumpongeze kwa kununua ndege kwa pesa ya madafu yenye uwezo wa kuchukua abiria 70 na inasifa ya kuwa na panga boi kwa mbele!! Teheeee
Ukiangalia kwenye picha ni kama abiria 132 hivi, ngoja ifike tuone. Kama ni abiria 70 basi ni wastage of resources maana hapo ndio aliposhindwa Precision Air kwa vile soko limebadilika linataka muda mfupi WA safari. Kumbuka wanaopanda ndege ni tabaka la juu pekee
 
MUNGU akubariki sana kwahili akupe ulinzi wake majungu n moja ya sehemu ya uongozi ukalinde NA damu ya Yesu


Tuwe na mtazamo angavu kidogo kwenye hilo, bila kujali pesa imetoka wapi lakini tuwe na kituo kwenye sifa zetu hizi na tuombe Mungu zisiwe na tatizo tutajuta na pesa tumeshapita yote

Wataalam wa fedha watatujia na mchanganuo wa kipi kilikuwa na nafuu kati ya kununua cash kwa pesa ya mkopo ama kulipa kidogo kidogo kwa pesa binafsi?

Kama wenzetu wote wananunua kwa kulipa kidogo kidogo kwanini sisi tukaamua kulipa cash?

Masharti na mikataba inaweza kuwa mizuri na ya wazi kabisa kama kukitokea tatizo ndani ya kipindi cha guarantee lakini utekelezaji wake una gharama kubwa

Waliowahi kununua vitu brand new vyenye guarantee halafu vikasumbua wanaweza kuwa mashuhuda wazuri wa ninachojaribu kukisema

Ukinunua unapewa na receipt na guarantee card ya miezi 12 (basic)lakini kikisumbua ndani ya wiki ukikirudisha ndio utajua nini maana ya guarantee!

Utaambiwa kiache mafundi wa Kampuni waje kukitazama unaambiwa uje baada ya muda fulani, unakuwa mpole na kuja baada ya huo muda na kupewa kifaa chako kikiwa kishatengenezwa, kikisumbua tena unarudisha, yani mpaka uje ubadilishiwe utakuwa umeshateseka sana na kutumia gharama kubwa na kama ndio umenunua kitu dar halafu unaishi mkoani ndio kabisa utajuta
 
Mkuu, kuna watu hawana shukrani hata kidogo. Muda wa uongozi wa Magufuli ukiisha watamkumbuka sana
 
Waziri amesema wamenunua "cash" ili kuokoa riba na waliweza "kunegotiate " bei kutoka bilioni 30+ mpaka bilioni 26 .Wamenunua zile ndege kwa kuwa zina uwezo wa kutua kwenye viwanja vyote vya changarawe na lami na pia ulaji wake wa mafuta ni mdogo kulinganisha na nyingine.
 
Kwa hili nampongeza, mimi ishu yangu ni kuwa kama anafanya mambo mazuri kwa nini anakandamiza demokrasia


Amegundua kua demokrasia za magharibi hazitufai, na zitamkwamisha kwenye Mipango yake.

Tunahitaji Demokrasia inayoendana na desturi zetu Kama waafrika /watanzania.
Ni Kama China ina Mfumo wake wa demokrasia ambao nao sio wa kubeza , china imefanikia sana si kiuchumi tu Bali hata kijamii .

Sisi tunapoiga demokrasia za magharibi , vyuo vikuu vya magharibi vinajifunza kuhusu demokrasia ya China Kama utaratibu unaofuata baada ubepari kuanguka!
 
Dash 8 Q400 inachukua abiria mwisho 78.Naona rais alitaka kununua ndege immediately.utaratibu mwingine wa ununuzi ungewezekana ile ndege zisingefika leo.saa nyungine huwa ni zali.Ndege za mara ya mwisho kununua precision walipata discount kubwa sababu kuna airline ilichomoa waka capitalize hapo.Ndege ya mwisho Bombardier cs 300 ya watu 150 nadhan inakuja kwa utaratibu tofauti na italetwa mwaka ujao
 
MUNGU akubariki sana kwahili akupe ulinzi wake majungu n moja ya sehemu ya uongozi ukalinde NA damu ya Yesu

Maana ya kununua cash ni kwamba kuna umuhimu wa haraka sana manunuzi kufanyika.... Rais hana fedha, fedha ni kodi ya wananchi km ameamua kuua Bunge lenye wawakilishi wa wananchi kupanga bajeti na ghafla Rais akawa ndie Msimamizi wa fedha Serikalini siyo shida kuamua ndege zinunuliwe km dharura potelea mbali madawa, mahitaji ya elimu etc. ameamua tuanza Na ndege mengine siyo ya haraka
 
Back
Top Bottom