Rais Dk. John Magufuli kuhamia Dodoma

SONGOKA

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
1,843
1,841
Nimepewa tetesi kuwa Rais Magufuli kakataa kuishi Dar na ameagiza kuhamishiwa Dodoma yalipo makao makuu ya nchi.

Mlio jikoni tupeni uhalisia wa hili.

Ikulu ndogo ya Chamwino imeanza kufanyiwa Usafi tayari Kumpokea Rais Magufuli. Inasemekana hata Waziri Mkuu ataapishwa katika hii Ikulu ndogo ya Chamwino.

Shughuli nyingi za Rais, zitafanyika kutokea kwenye hii Ikulu.
 
Hata ahamie mbinguni watanzania wanataka mabadiliko sio ujanja ujanja na danganya toto

Hueleweki mtanzania mkenya maana umekaa neutral, ukisikia mazuri ya Kenya unakuwa mkenya, ukiona zuri la huku unakuwa Mtz, hebu simama sehemu moja maana sisi Dual citizen
 
Nimepewa tetesi kuwa Rais Magufuri kakataa kuishi dar na ameagiza kuhamishiwa Dodoma yalipo makao makuu ya nchi.

mlio jikoni tupeni uhalisia wa hili

Nampa hongera kama ni kweli, lakini itakuwa ni mwendelezo wa kuigiliza aliyokuwa anayaamini Mheshimiwa Lowassa.
 
Ikulu ndogo ya Chamwino imeanza kufanyiwa Usafi tayari Kumpokea Rais Magufuli. Inasemekana hata Waziri Mkuu ataapishwa katika hii Ikulu ndogo ya Chamwino.

Shughuli nyingi za Rais, zitafanyika kutokea kwenye hii Ikulu.
 
Dodoma hakuna juice ya maembe huko, ni ukame mtupu. usafi ni kawaida ya ikulu akiingia rais mpya
 
Kabla ya kuanza bunge,lazima makazi yaandaliwe!,kwani kutakuwa na kazi ya kulihutubia bunge!,na kuwasilisha pendekezo la jina la Waziri Mkuu.
 
Nayo hii ni habari, hata huna uhakika, kwani ikulu ndogo huwa haendi Rais akiwa na shughuri Dodoma au ulitaka aingie Ikulu ikiwa chafu hiyo ya Dodoma
 
Ikulu ndogo ya Chamwino imeanza kufanyiwa Usafi tayari Kumpokea Rais Magufuli. Inasemekana hata Waziri Mkuu ataapishwa katika hii Ikulu ndogo ya Chamwino.

Shughuli nyingi za Rais, zitafanyika kutokea kwenye hii Ikulu.
Hata SHEMEJ shughuli nyingi alifanyia Dodoma (Chamwino)
 
Akifanya hivyo itakuwa vizuri sana maana maofisi mengi yatahamia huko!!
 
Mwende huko mtupunguzie foleni kwenye hili jiji, maana nyie na misafara yenu inachangia foleni
 
Hata ahamie mbinguni watanzania wanataka mabadiliko sio ujanja ujanja na danganya toto

Kwani ikulu ikiwa Dodoma ndio nini, suala LA ikulu iwepo wapi lilikuwa na nguvu kipindi mile cha miaka ya mwanzoni mwa Uhuru kwa sababu ambazo zipo wazi, sasa hivi halina mashiko.
 
Sawa lakini hata waliokaa ikulu ya magogoni walikuwa na sababu. Wale walioamua makao makuu kuhamia Ddm ingeku ni sasa wasingeamua hivo. It was an outcome of cold war and ubeberu. Iliaminika ddm ni salama. Lkn sasa kukua kwa tkngia si sabb tena
 
Wazo zuri lakini nahisi utekelezaji wake kwa sasa ni mgumu mno.

Akihama yeye lazima wizara zote zihamie Dodoma. Maana yake kutahitajika pesa nyingi sana. Anahitaji pesa hizo kwenye elimu, afya na miundombinu.
 
Back
Top Bottom